in

Harry Kane bila mataji atadumu Spurs ?

Harry Kane

UKIZUNGUMZIA washambuliaji mahiri EPL jina la Harry Kane litakuwa miongoni mwake. Jina lake si linatajwa kwa sababu ya uraia wake bali uwezo  wa kufunga mabao na kuibeba Tottenham Hotspurs kwa muda mrefu tangu alipoanza kung’ara kikosini.

Pamoja na umahiri wote huo Harry Kane anakabiliwa na ukata wa mataji. Akiwa na Spurs amechea fainali ya Ligi ya Mabingwa mara moja tu chini ya Mauricio Pochettino na kufungwa bao 1-0 na Liverpool.  Tangu hapo Spurs imepoteana kabisa na hata ilipokuwa  chini ya Jose Mourinho hakifua dafu kwenye mashindano ya ndani au kimataifa.

Mourinho ni kocha mkubwa na mwenye sifa kemukemu lakini alishindwa kuifikisha ngazi za juu timu hiyo. Kane amewahi kumsifia Mourinho lakini ukweli unabki bado hawakushinda chochote wakiwa klabuni hapo.

Mchezaji anacheza mpira ili ashinde medali za mataji, lakini kwa Harry Kane mambo yamekuwa magumu. Hakuna dalili za kushinda medali akiwa na Tottenham Hotspurs, na ndipo mjadala unaibuka iwapo ataendelea kusotea medali na matumaini hewa au ataamua kuhama ili kutafuta changamoto mpya na medali za makombe?

Kane amejitoa katika kikosi hicho mara nyingi akiwa chini ya makocha tofauti. Anacheza na wachezaji wenye vipaji ambao wanasaidia kupunguiza kazi yake lakini bado Spurs haionekani kama timu inayopigania medali za makombe yoyote.

Tanzania Sports
Bale na Kane washambuliaji hatari wa Spurs

Tanzaniasports imefanya tathmini na kuonesha kuwa Harry anaweza kupata nafasi ya kucheza katika timu kubwa na zenye ubora na uwezo wa kushinda medali za makombe kama vile Barcelona, Real Madrid, PSG,Manchester United,Liverpool,Bayern Munich,Juventus,Inter Milan kwa kuzitaja chache.

Kane anaweza kucheza pale PSG akichukua nafasi ya Mauro Icardi kuongoza safu ya ushambuliaji huku akizungukwa na Kylian Mbappe na Neymar Junior.

Kane anaweza kucheza mbele ya Cristiano Ronaldo katika safu ya ushambuliaji ya Juventus, wakashirikiana na nyota huyo bila kuyumbisha timu. Kane anaweza kucheza pamoja na Karim Benzema na kuisaidia Real Madrid kupachika mabao ya kutosha kwa sababu Benzema hucheza kama namba tisa mwenye jukumu la namba 10 na amekuwa mshirika mzuri wa kuwasaidia washambuliaji aliocheza nao.

Kane anaweza kucheza vizuri akiwa na Edinson Cavani pale Manchester United kwahiyo ana namba yake pale akiamua kwenda. Kane anaweza kucheza mbele ya Gabriel Jesus pale Man City chini ya Pep Guardiola. Kane anaweza kucheza mbele ya Roberto Firmino pale Liverpool.

Kwahiyo Kane ni mshambuliaji ambaye anaweza kuingia kwenye kikosi cha timu bila wasiwasi kwa sababu anajulikana kwa uwezo mkubwa wa kupachika mabao,kucheza kitimu na kusaidia ushindi wa timu.

Tetesi zinamhusisha Harry Kane na usajili wa fedha  nyingi, na ambako huenda timu itakayomsajili itatumia gharama kubwa kupata huduma zake. Inasemakana Kane anashinikiza kuuzwa kwa sababu anatamani kushinda medali za makombe kuliko kupigania timu ambayo haionekani kama itampatia hayo kwa miaka ya karibuni.

Kane amefunga mabao 122 katika mechi 336 katika jezi za Tottenham Hotspurs, ni mchezaji ambaye anaweza kuwindwa na timu nyingi ili akaendeleze upachikaji wa mabao na kuzipatia mataji kuliko Spurs.

Timu zinazoongoza kuwania huduma ya Kane ni Chelsea ambayo imetoka kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa katika mazingira magumu kwa sababu safu ya ushambuliaji wake haijawa hodari katika kupachika mabao. Chelsea wanategemea huduma za Tammy Abraham na Olivier Giroud lakini hawajapata nafasi ya kucheza na hawana rekodi nzuri kila wanapocheza pamoja na kukabiliwana na ukame wa mabao.

Man City nao ambao wamempoteza mshambuliaji wao Sergio Kun Aguero aliyemaliza mkataba wake na kujiunga na Barcelona wanataka kusajili mshambuliaji wa kuziba pengo hilo.

PSG ni klabu nyingine inayowinda huduma ya Harry Kane ambako inafundishwa na kocha wake wa zamani Mauricio Pochettino. Kocha huyo anaamini Kane anatakiwa kucheza timu kubwa na yenye mikakati na uhakika wa kushinda medali kuliko kutafuta nafasi ya kumaliza ‘Top Four’ au kushiriki mashindano ya Europa League.

Sababu nyingine inayomshinikiza Harry Kane kuondoka Spurs ni sintofahamu ya nafasi ya ukocha klabuni hapo. Tangu kufukuzwa Mourinho wameishi na kocha wa mpito Ryan Mason ambaye amemaliza muda wake. Kwa sasa makocha wanaotajwa kuinoa Spurs ni Antonio Conte ambaye ameondoka Inter Milan hivyo hana kazi kwa sasa.

Kufukuza makocha mara kwa mara kumechangia Spurs kuyumba na kushindwa kuwa timu inayopigania kushinda medali ya makombe yoyote EPL. Hawajashinda kombe lolote kwa miaka mingi huku kukiwa na dalili hizo kutoshinda kwa misimu ijayo kwa sababu hakujulikani ni wapi timu hiyo itakuwepo baada ya misimu miwili.

Haifahamiki kocha atakayekuja atakuwa na mikakati gani ya kushinda medali za makombe, pamoja na kuwabakiza nyota wenye mchango mkubwa kwa timu hiyo. Haifahamiki kama nyota hao akiwemo Harry Kane watakubali kufanya kazi kwa ufanisi chini ya kocha mpya na kuishi kwa matumaini bila kupata kombe huku umri wake ukiwa unamtupa mkono.

Kama Kane ataendelea kubaki Spurs maana yake amefuta fursa ya kutwaa medali za makombe, na atakuwa shuhuda wengine aliowazidi uwezo wakishangilia viwanjani kwa ushindi wao. Hadi sasa anao uamuzi abaki klabuni au aondoke kutafuta malisho mapya na yenye uhakika wa kutwaa makombe ya ndani na nje. Kama hataamua sasa, maana yake hadithi yake kwenye mchezo wa soka itaishia kwa uchungu kukosa medali ya makombe.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Carlos Carmo

Kwaheri ‘Genius’ Calinhos mwalimu wa viungo VPL

Diamond Platnumz

Muziki wa Bongofleva ni mkubwa kwa sasa