in

Kwaheri ‘Genius’ Calinhos mwalimu wa viungo VPL

Carlos Carmo

Carlos Carmo ni maarufu kwa jina la Calinhos raia wa Angola. Calinhos si mchezaji wa Yanga tena. Hivi karibuni Yanga walitangaza kufikia makubaliano ya kuvunja mkataba na kiungo wake nyota Calinhos. Haijaelezwa bayana sababu za kuvunjwa mkataba huo lakini pande zote mbili zimekubaliana.

Tetesi zinasema kuwa Carlinhos alikuwa haipendezwi na mifumo ua maisha ikiwemo vyakula. Lakini kubwa zaidi Calinhos alikuwa anakabiliwa na tatizo la lugha, kwa sababu yeye alikuwa anazungumza zaidi kireno ambacho hakifahamiki miongoni mwa wachezaji wenzake pamoja na watanzania kwa ujumla.

Licha ya kuondoka uchezaji wake ulikuwa unasisimua kutokana na matukio yake kusaidia klabu hiyo ya jangwani kuibuka na pointi kwenye michezo anayocheza.

Je ni sababu zipi zinamfanya nyota huyo awe ‘genius’ na mwalimu wa viungo wengi wa soka nchini Tanzania? uchambuzi wa TanzaniaSports unabainisha mambo ya msingi ya Calinhos na namna yake ya kucheza soka.

Kwanza, Calinhos anacheza mchezo wa matokeo mazuri kwa timu. Yeye si mchezaji wa mtindo wa kanzu,chenga,tobo au kugeuka geuka kama wanavyofanya wachezaji wengi wa Kitanzania wanaocheza nafasi ya kiungo. Kazi yake anayopenda ni kusababisha madhara kwa timu pinzani kuanzia krosi,kona,adhabu ndogo yaani namna anavyouchukulia mpira na kuhudumia timu ni jambo la kipekee. Haonekani kucheza kwa mtindo wa kufurahisha jukwaa lakini yeye hucheza kwa mipango maalumu na anampoa kocha kitu adimu katika kikosi chake.

Pili, Calinhos ni kiungo wa pembeni kulia au kushoto, katikati na mshambuliaji wa pili. Calinhos anatumia akili kubwa uwanjani. Hatumii nguvu kubwa. Soka la kisasa linahitaji uchezaji wake. Hakai na mpira bila sababu. Akipata mpira mara moja anatoa pasi. Anabadili mwelekeo wa mashambulizi, mikato yake inaweza kwenda kulia au kushoto. Anapiga pasi ndefu na fupi za haraka zaidi. Anapishana na nguvu za mabeki au wapinzani wake uwanjani. Anaweka mpira kwenye njia na kuhakikisha unamfikia mlengwa hata kama yeye atakuwa amezuiwa.

Tatu, uwezo wake wa kujipanga na kuomba nafasi ni wa kipekee. Ni mchezaji ambaye atakuwa amepunguza mvuto wa Yanga kikosini na kiufundi. Anapokea na kutoa haraka ukimfikia mlengwa. Anacheza kwa faida na malengo, tofauti na wachezaji wetu wazawa wanakaa na mpira.

Nne, makosa ya mabeki wengi wa VPL walikuwa wanampania mno kiasi kwamba yeye alikuwa anapishana, hakutaka kupambana kimwili. Calinhos ukimfuata kwa nguvu kubwa anakupisha, anapitisha mpira katikati. Wanapopania kumchezea faulo alikuwa mwepesi kumshawishi mwamuzi ampendelee. Calinhos alikuja kutoa elimu kubwa. Unaweza kudhani anacheza kwa dharau lakini anajua tuna wachezaji wengi wenye ‘minguvu’ mingi mno dimbani kuliko maarifa.

Hakika huyu ni mchezaji ambaye alileta darasa kubwa kwa viungo wetu oamoja na sokala Tanzania kwa ujumla wake. Vilevile Calinhos anatuletea hoja, ni namna gani viungo wetu Salum Abubakar ‘Sure Boy’ na Feisal Salum, je kanzu,tobo na  vyenga zinasaidia nini ikiwa timu haipati ushindi? Zinasaidiaje timu kuondoka na pointi tatu? Kwanini kuwe na pasi za nyuma nyingi kuliko mbele?

Je, Feisal Salum na viungo wengine tunaamini wana vipaji vikubwa na tegemeo la taifa hili, je wametengeneza mabao mangapi kwa msimu huu au misimu mitatu iliyopita? Kama hakuna basi ni changamoto yao, wanatakiwa kubadilika. Kama yapo basi iwe heri zaidi.

Tanzania Sports
Yanga vs Simba

Je, viungo wetu wshambuliaji wanajifunza nini kwa Calinhos? Je, wanayaona malengo yake kila mechi anayopewa kucheza? Simaanishi kila kiungo mshambuliaji awe anacheza kama Calinhos bali kuchota maarifa kucheza kwa malengo zaidi. Vipaji vyao vitumike kutengeneza nafasi za mabao,kufunga na kujiwekea takwimu muhimu zenye faida kwa timu.

Inaweezerkana Yanga wamejipanga kuishi bila nyota huyo kikosini, lakini ni aina ya wachezaji ambao walitakiwa kuzungukwa na timu ambayo inapiga pasi fupi fupi na kumpa uhuru wa kuhatarisha lango la adui. Lakini kama Calinhos angekuwa anacheza soka linalolingana na kikosi cha Dodoma Mji au Simba ambazo zinapiga pasi fupi fupi na kumiliki mpira kwa kiwango kikubwa, nina uhakika kiungo huyo angekuwa hatari zaidi. maarifa yake yangekuwa chachu ya kupata mabao mengi kupitia krosi na mipira yake ya adhabu na kona. Calinhos anakuongezea kitu maalumu katika timu yako kwahiyo si mchezaji wa kupuuzwa hata kidogo.

Ingawaje tetesi zinasema kuwa ikiwa Calinhos atasajiliwa na timu nyingine Tanzania basi Yanga wanataka kulipwa shilingi milioni 400. Zinabaki kuwa tetesi kwa sababu hadi leo Calinhos yuko kwao Angola na ikiwa ni kweli atatakiwa na klabu ya Tanzania ninaamini inapaswa kutpfumba macho kwenye uwekezaji huo.

Kwamba ikiwa Simba watahitaji huduma ya nyota huyo wasisite kutumbukiza uwekezaji wa milioni 400 ili kunufaika na uwezo wa kijana huyo kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Calinhos ataongeza maarifa ya kigeni ambayo hayajatumika kwa asilimia 100 pale Yanga. Ni suala la uamuzi tu kumchukua na kuruhusu wachezaji wasiohitajika kikosini kama vile Ibrahim Ajibu, Gadiel Michael au Miraji Ibrahim.

Report

Written by Mark Mpangala

*Markus Mpangala ni Mhariri, Mwandishi wa Makala Maalumu, Mwanahabari,Mwanablogu,Mwanafasihi na Mwanasafu, ambapo kwa kipindi cha miaka 12 amefanya kazi katika vyombo vya habari mbalimbali vikubwa na vidogo nchini Tanzania katika Michezo, Siasa, Elimu na utalii. Pia ni mchambuzi mchangiaji wa masuala ya siasa na utawala bora katika idhaa ya Kiswahili ya Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC SWAHILI). Ni mhariri na mhamasishaji wa usomaji wa vitabu*

What do you think?

70 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Kun" Aguero

Kichekesho kichungu usajili wa Kun Aguero

Harry Kane

Harry Kane bila mataji atadumu Spurs ?