in , , ,

Arsenal wamerejesha ile soka, wanautaka ubingwa

Wakubwa wa soka wa London Kaskazini – Arsenal, wanaonekana kurejea kwa nguvu na ile soka kali ya ushindani na inanekana kwamba tam,aa yao ya kuutaka ubingwa wa England ni kubwa.

Hivyo ndivyo inavyoonekana na kuleta hisia za aina yake, wakicheza soka ya nguvu na kukamiana kwenye kukaba na kushambulia kwa nguvu, hata kama kuna makosa ya hap ana pale ambayo katika soka hayakosekani.

Soka hiyo imerudi Arsenal, wachezaji wakionekana kutumia nguvu na kuvuja ‘jasho na damu’, wakijitoa kwa kila namna kwa ajili ya timu na inaonekana ni sawa.

Msimu huu, Kocha Mikel Arteta ameonekana kutaka wachezaji wake kutumia pia akili zaidi, kuwa na udhibiti na uvumilivu kwenye mpango wa mechi ili kuepuka zile nyakati zinazoweza kuwagharimu. Hata hivyo, kiasi fulani cha nguvu ya hisia, iwe kwa uzuri au la, kinaipasa timu hii ya Arsenal.

Arteta anasifu jinsi wachezaji wake “walivyoweka moyo na roho katika kila mpira.” Uwanja wote uliguswa na kuwashwa kwa hilo, Arsenal walipokuwa nyumbani Emirates wakikabiliana na Liverpool usiku wa kuamkia Jumatatu.

Tanzania Sports
Arsenal

Umati wa washabiki pale Emirates walishangilia kwa sauti kubwa, kuonesha kuridhishwa kwao na jinsi Declan Rice alivyokuwa akitumia umahiri pale kati, akifanikiwa mara nyingi kila alipouweka mguu wake kwenye mpira. Ikawa hivyo tena kwa jinsi Gabriel alivyokua akiukimbiza mpira kwa kasi upande ule wa kushoto.

Wakafika mahali wakamwimbia yule ambaye hakupata kusifiwa hapo, Jorginho, ambaye alikuwa mchezaji bora mno katika moja ya mechi chache sana kwake kuanza. Wakalipuka wakati aliyecheza namba tisa, yaani pale kati mbele, Kai Havertz alivyoiyumbisha beki ya Liverpool, akiwa mzuri mno kwenye ile ‘kazi chafu’.

Kwa jinsi wacheezaji walivyotawala na kuonesha uwezo mkubwa kwa muda mwingi wa kipindi cha kwanza na baadaye kuingia kipindi cha pili kwa nguvu, Arsenal walipiga hatua kubwa. Walitoa kile Mikel Arteta anachoita “watu wetu” kuwaamini Arsenal tena.

Imechukua muda kufanya hivyo katika wakati huu wa aina yake wa msimu, lakini hisia mwishoni zilikuwa nzuri na walipata walichokitaka – ushindi wa 3-1. Jorginho, kwa ushawishi na uzoefu wake, alielezea saikolojia ya timu kuwa ni “kukua”, akiongeza kwam,ba walifanikiwa kukabiliana na hali mbalimbali za kisaikolojia kadiri mechi ilivyoendelea.

“Udhibiti si neno hasa nilipendalo,” Arteta anasema. “Napenda utawala na kutoruhusu timu kupumua kuliko kudhibiti. Kwamba ni eneo gani la uwanja hilo linatokea kwangu ni muhimu zaidi, lakini tunaweza kuwasumbua kwenye maeneo ya wazi na kutengeneza mazingira mengi mazuri na tofauti ya kucheza.”

Arsenal walianza kwa kasi mechi ile, wakisogeza mashambulizi haraka haraka na kuufanya mchezo uwe wa kasi. Walifanya vyuema na kwa hakika katika ile nusu ya kwanza wangeweza kupata zaidi ya bao moja. Havertz alipewa pande na Martin Odegaard akiwa kwenye sehemu nzuri mno, akajikusanya lakini akampigia moja kwa moja kipa Alisson aliyeuchukua mpira kirahisi tu.

Kwa bahati, udhaifu wa ghafla wa kipa huyo ulimruhusu Bukayo Saka kutumbukiza mpira wavuni na Arsenal wakawa wanaongoza 1-0 hadi karibu na mwisho kwabisa wa kipindi cha kwanza pale William Saliba na David Raya waliposhindwa kuokoa mpira kwa njia yoyote kiasi cha kutumbukia wavuni mwao na kwenda mapumziko wakiwa sare ya 1-1, Arsenal wakisikitika mno.

Eneo jingine muhimu lilikuwa kwenye vyumba vya kubadili nguo, ambapo walirejea yaliyotokea na kuweka mikakati ya kipindi cha pili, Jorgino akielezea hali ile kama: “Tulikwenda vyumba vya kubadilishia nguo, tukazungumza, tukasema hatukutakiwa kushusha nguvu ya timu.”

Kwamba walidhamiria kwamba lile bao la kusawazisha haikutakiwa kuwaathiri kwa namna hasi, maana timu ilicheza vyema muda mwingi. Arteta akaongeza: “Tulisema, ikiwa mnataka kuwapiga, lazima mteseke.”

Kweli, kipindi cha pili vijana wakajituma na washabiki wakawa nyuma ya kwa kushangilia sana kuwapa moyo na wakapata mabao mengine mawili kupitia kwa Martinelli na Trossard, wakifikisha alama 49 karibu zaidi na Libverpool wenye alama 51 kwa idadi sawa ya mechi 23. Nafasi ya tatu wamo Manchester City nay a nne ni Aston Villa, kwa kadiri ya takwimu za Jumatatu Februari 5, asubuhi.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

SIMBA SC NGOMA NGUMU NBC PL

Tanzania Sports

KUELEKEA FAINALI YA AFCON 2023