in , ,

NILICHOKIONA KWENYE MECHI YA YANGA NA STAND UNITED

Kikosi cha timu ya Yanga

Stand United waliamini kupitia mpira wa wazi ( Open Football ).

Ni madhara makubwa sana timu yako inapokuwa inacheza mpira wa wazi (
Open football ) huku wakiwa na beki isiyokuwa dhabiti kujilinda.

Siku zote unapocheza Mpira wa wazi ( open football ) .Unakuwa
unaruhusu njia nyingi za mipira kuwa wazi.

Ndicho kitu ambacho kilitokea, Yanga mara nyingi wamekuwa
Wakitengeneza nafasi nyingi za kushambulia kupitia eneo la pembeni.

Kwa Stand United kucheza mpira wa wazi( open football ) kuliwapa
nafasi kubwa Yanga kupata njia za kupitishia mipira na wakawa wanapita
pembeni kama kawaida.

Kitu cha muhimu ambacho Kiliwasaidia sana Yanga, ni kuwachezesha
washambuliaji wawili pale mbele. Hii iliwapa faida mbili.

Faida ya kwanza waliyopata Yanga, ni kwamba siku zote unategemea timu
yako itengeneze mashambulizi kupitia pembeni ili ipige krosi basi timu
yako Inahitaji mshambuliaji ambaye anauwezo wa kucheza mipira ya juu (
yani kwa vichwa) na hapa alikuwepo Ngoma.

Faida ya pili ni kwamba siku zote mipira ya krosi inapokuja eneo la
kumi na nane mwa adui yako, ili unufaike unatakiwa uwe na watu wengi
katika eneo lile ambao watakuwa na uwezo wa kuitumia mipira inayofika
pale na kuzagaa.

Tumekuwa tukimwangalia Tambwe alihangaika kupata magoli na hii ni
kutokana na kwamba amekuwa akicheza peke yake lile eneo la mbele, hata
mipira mingi ya krosi inapokuwa inakuja kwake anakuwa hana uwezo wa
kuokoa vizuri.

Faida nyingine ambayo Yanga walinufaika kuwachezesha Ngoma na Chirwa
ni kwamba wote wawili kwa kushirikiana na Msuva walikuwa
wanabadilishana vizuri eneo la pembeni.

Kuna wakati Chirwa alipokuwa anakuja kulia, Msuva alikuwa anaingia
eneo la kumi na nane la Stand.Vivyo hivo kwa Ngoma.

Udhaifu pekee kwa mabeki wa Stand United ulikuwa maeneo mawili.

Eneo la kwanza aina ya kukaba, walikuwa wanakabia macho zaidi.Siku
zote ili Unyime mijongeo (movements) ya Yanga pembeni ambapo ndipo
kuna ubora wao, unatakiwa uwakabe Man to Man (Mtu na mtu) washambulia
wa pembeni wa Yanga, goli la pili la Yanga mabeki wa Stand United
walikuwa wanamsindikiza kwa macho Msuva ambaye alikuwa huru kuanzia
anapata mpira kutoka kwa Chirwa mpaka anaenda kufunga.

Udhaifu wa pili wa mabeki wa Stand United ulikuwa katika kuzuia mipira
ya krosi.Ukiachana na kwamba hawakuwa na uwezo wa kucheza vizuri
mipira ya krosi, pia hawakuwa wanajipanga vizuri mipira ya krosi.

Eneo jingine ambalo lilikuwa na udhaifu mkubwa kwa Yanga lilikuwa eneo
la Golikipa. Kuna makosa binafs ambayo alikuwa akiyafanya golikipa
ambayo yaliigharimu timu.

Kwa mfano, Goli la kwanza la Ngoma kwa kiasi kikubwa lilisababisha na
kosa lake la kuutokea ule mpira.

Unajua kwenye kanuni za kudaka mipira ya krosi au kona, kipa
anapoamua kufanya maamuzi ya kutokea krosi kwenda kuidaka anatakiwa
moja awe na uhakika wa kuidaka ile krosi, mbili asisite kwenye
maamuzi yake ya kwenda kuudaka ule mpira.

Makosa haya pia yalionekana kwenye goli la Nadir Haroub.

Matokeo haya kwa kiasi kikubwa yatawaongezea morali katika vita yao ya
ubingwa na moja kwa moja yanaipa presha Simba kwenye yao dhidi ya
Majimaji ambapo kwa kiasi kikubwa watacheza wakijua kuwa Yanga
wameshinda mechi dhidi ya Stand United hivo presha kubwa itakuwa kati
yao zaidi kwenye mechi dhidi ya Majimaji.

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

Chelsea safi, Arsenal mh!

Serengeti boys

SERENGETI BOYS YAFUZU FAINALI ZA KOMBE LA MATAIFA YA AFRIKA