in

Ukubwa wa sifa za makocha ni ubora wa Ligi Kuu Bara 

Makocha wanaomiminika kuzinoa timu za Ligi Kuu Tanzania Bara wamekuwa wakipanda sifa  siku hadi siku. Wengi wao ni wale ambao wamekuwa wakitafuta fursa ya kutoka kwa maana ya  kujtengeneza wasifu wao na uzoefu katika soka la Afrika.  

Ndio maana makocha wengi wanaoajiriwa katika klabu na timu za Taifa kuna kipengele cha  uzoefu wa soka la Afrika. Ligi Kuu Bara imeshuhudia makocha wengi wakitua nchini. Wapo  makocha waliofanikiwa na wengine wameshindwa. Wapo walioweka rekodi za aina yake na  ambazo zinatumika kuwapima wengine. Makocha kama Trott Moloto, Jack  Chamangwana, George Lwandamina, James Siang’a, Razak Siwa,  

Aliyekuwa kocha wa mabingwa wa soka nchini Simba, Didier Da Rosa Gomes ameteuliwa kuwa  kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Mauritania. Sven Vandenboeck aliyeacha mikoba kwa Gomes  pale Simba ni kocha wa klabu kongwe ya FAR Rabat. 

Katika msimu wa 2021/2022 benchi la ufundi la Yanga nalo lina makocha wakubwa kocha  mkuu Nasredine Nabi raia wa Tunisia na msaidizi wake Cedric Kaze raia wa Burundi.  

Hawa ni makocha wenye leseni ya juu ya Shirikisho la Soka barani CAF wakiwa wanakiongoza  kikosi cha Yanga huku kocha wa makipa Razak Siwe ni raia wa Kenya. Ukiangalia ukubwa wa  sifa za makocha waliowahi kufundisha Simba na Yanga utaona kuna mabadiliko kila wakati pale  wanapoteuliwa.  

Tanzania Sports
Wachezaji mahili wa Tanzania

Vilevile baadhi ya klabu za Ligi Kuu zimeajiri makocha wa kigeni, kutoka  Burundi,Kenya,Cameroon kwa kutaja chache. Joseph Omog raia wa Cameroon ni kocha mzoefu  wa Ligi ya Tanzania akiwa amezinoa Simba na Azam fc kwa nyakati tofauti kwa sasa anakinoa  kikosi cha Mtibwa Sugar ya Morogoro.  

Patrick Odhiambo anawanoa Biashara United huku raia mwenzake wa Kenya, John Baraza  akiwa kocha mkuu wa Kagera Sugar. Simba kwa sasa wananolewa na Pablo Franco Martin raia  wa Hispania.  

Ndiyo kusema makocha wengi wa kigeni waliopitia klabu za Tanzania. kuanzia makocha wa  makipa,viungo,wataalamu wa ufundi, wachambuzi wa mifumo,umahiri na masuala mengine  muhimu yamekuwa yakifanyika katika Ligi hii. 

Swali moja ambalo linaweza kuulizwa sasa ni je kuna umuhimu gani kuwa na makocha wa  kigeni? Ama makocha wa kigeni wanaleta kitu gani katika soka la Tanzania. ifahamike makocha  hawa wanakulia katika utamaduni na maarifa tofauti.  

Utamaduni wa soka la Tunisia na mifumo yake ni tofauti na Tanzania. Cedric Kaze akiwa na  uzoefu wa kufundisha kandanda Ujerumani na Barcelona pamoja na Burundi anayo maarifa  tofauti na utamaduni kuliko baadhi ya wazawa wetu. 

Unapokuwa na wataalamu wa kuchambua mifumo ya uchezaji wa adui na kuiwasilisha kwa  makocha wakuu ina maana kubwa katika ufundishaji wa kandanda nchini. Wachezaji wetu  wazawa wanachota maarifa kutoka kwa makocha mbalimbali kuanzia Afrika kusini,  Ubelgiji,Tunisia,Ufaransa,Serbia,Uingereza,Hispania na mataifa mengine ya kiafrika.  

Katika Ligi ya Tanzania iliyoshuhudia makocha mbalimbali wa kigeni inanufaika kutokana na  elimu zao, hivyo kupanda mbegu ya ufundi zaidi nje ya vipaji vyao wa kusakata soka.  

Kwa mfano timu ya Taifa ya soka inananolewa Kim Poulsen raia wa Denmar akisaidiwa na  makocha vijana wa Kitanzania Shadrack Nsajigwa na Ivo Mapunda. Kimsingi makocha wan je  tangu zama akina Victo Stanclescu na wengineo wametoa mchango mkubwa wa maarifa ya  ukocha.  

Kuwa na makocha wa kigeni ni faida kubwa kwa sababu wanapendekeza ujio wa vipaji vipya  kutoka nchi zao walizozaliwa ama waliokowahi kufundisha. Lakini pia makocha hawa  wanapoajiriwa katika klabu zingine huangaliwa wasifu wao na kuonekana walip[itia kufundisha  soka Tanzania.  

Makocha watatu wa Simba Sven, Patrick Aussems na Didier Gomes wote wamepata vibarua  katika nafasi nzuri. Sven alichukuliwa na timu kongwe barani Afrika, wakati Gomes alitua  Mauritani kuwa kocha wa timu ya taifa.  

Hii ina maana kwamba Ligi Kuu ya Tanzania imetoa mchango mkubwa kwa makocha hao  wakati ambao nao wametoa maarifa makubwa katika soka nchini. Kwenye diplomasia tunaweza  kutumia michezo kama sehemu ya kuitangaza nchi, ndiyo maana baadhi ya nchi huwatumia  wanamichezo kama nyenzo ya kujenga uhusiano bora wa kidiplomasia kati ya nchi wanakotoka  na kule wanakocheza.  

Gomes, Aussems, Sven, Nabi na wengineo wanakuwa mabalozi wazuri wa Ligi Kuu Tanzania.  hawa ni makocha ambao wanaitumia Ligi hii kupanda ngazi zaidi, huku wao wakitoa ujuzi wao  kwa wachezaji wa kitanzania. Wasifu mkubwa walionao makocha kwenye Ligi Kuu Bara ni  manufaa makubwa kwa wachezaji na ligi yetu wenyewe.  

Ni sehemu ambayo inanwavutia wachezaji wa kigeni kuja kutandaza soka hapa nchini. Kama  kina Trott Moloto walitua hapa ni nani anaweza kukataa kuinoa timu ambayo inatinga robo  fainali ya Ligi ya Mabingwa au uhakika wa kumjengea wasifu mzuri zaidi katika kazi? 

Ni kocha gani atakataa malipo yanayotolewa na timu za Tanzania ambapo katika ukanda wa  Afrika mashariki inatajwa kuwa na malipo mazuri kwa wachezaji na makocha kuliko wengine? 

Ni wakati wa makocha wazawa kuchota ujuzi. Ni wakati wa viongozi wa soka au watu wa mpira  kujifunza masuala muhimu ya uongozi wa soka kutoka kwa makocha wa kigeni. Ni wakati wa  kuwasikiliza mbinu za mafanikio katika kandanda. Ni wakati wa kuwaona wachezaji wetu  wakipiga hatua zaidi kutokana namaarifa wanayopata kutoka kwa makocha wao wa sasa. 

Ligi kuu Bara kadiri inavyovutia makocha wenye sifa kubwa ndivyo inavyopiga hatua na  kuonesha ubora wake kupitia mashindano ya kimataifa. Tukizingatia uwekezaji unaofanywa na 

wadhamini wa Ligi Kuu na Haki za Televisheni maana yake pesa zimeongezeka,ushindani  umeimarika na kuwanoa makocha,wachezaji na viongozi.

Report

Written by Mark Mpangala

*Markus Mpangala ni Mhariri, Mwandishi wa Makala Maalumu, Mwanahabari,Mwanablogu,Mwanafasihi na Mwanasafu, ambapo kwa kipindi cha miaka 12 amefanya kazi katika vyombo vya habari mbalimbali vikubwa na vidogo nchini Tanzania katika Michezo, Siasa, Elimu na utalii. Pia ni mchambuzi mchangiaji wa masuala ya siasa na utawala bora katika idhaa ya Kiswahili ya Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC SWAHILI). Ni mhariri na mhamasishaji wa usomaji wa vitabu*

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

Fahamu mambo muhimu Kombe la Dunia 2022

SSC

Simba katikati ya wababe wa soka Afrika