Hakuna uhakika wa nani atakuwa bingwa wa Ligi Kuu Italia msimu huu. Hilo ni hitimisho ambalo limefanywa na TANZANIASPORTS kulingana na mchuano mkali uliopo katika Ligi Kuu Italia maarufu kama Serie A. Vigogo vya soka vinapambana kuhakikisha vinachukua ubingwa na uwezekano wa timu tatu hadi nne kuchukua ubingwa huo upo bayana. Katika uchambuzi uliofanywa unaonesha kuwa Ligi Kuu Italia msimu huu imeitupa mbali AC Milan katika kinyang’anyiro hicho. Baadhi ya vigogo ambavyo havipo kwenye mbio za ubingwa ni pamoja na Lazio, AC Milan, Juventus, Roma na Torino.
Kwa mfano AC Milan ili imalize kwenye nafasi nne za juu inatakiwa kupata pointi 9 kufikisha 60 ambazo zimeshafikiwa na klabu ya Bologna, na itatakiwa kuombea mabaya Juventus washindwe kupata ushindi katika mechi zao zilizobakia jambo ambalo huenda likawa gumu zaidi.
Vita ya Top Four
Katika vita hii timu nne zipo kwenye mpambano mkali w akumaliza nafasi hizo za juu ili ziweze kufuzu kwa mashindano ya Ligi ya Mabingwa msimu ujao. Inter Milana wanaongoza Ligi wakiwa na pointi 71 baada ya kucheza mechi 33 huku tofauti ya magoli ikiwa ni 40. Nafasi ya pili wamesimama vigogo Napoli wakiwa wamejikusanyia pointi 71 kutokana na michezo 33 huku tofauti ya mabao ikiwa ni 27. Atalanta wala wanashikilia nafasi ya tatu wakiwa na pointi 61, ni sawa na pointi 10 nyuma ya vinara wa Ligi hiyo. Nafasi ya nne inashikiliwa na Bologna ambayo ina pointi 60 kutokana na mechi 33. Katika nafasi hizi zipo timu kadhaa zenye uhakika wa kuingia na zingine kutoka. Nafasi ya kwanza na pili si rahisi kuondolewa lakini ya tatu ya Atalanta na ya Bologna lazima timu hizi zipiganie kubaki hapo.
Vita ya Euopa League
Baada ya nafasi nne za juu, sasa ni dhahiri wanaobakia wanatakiwa kupambana kuhakikisha wanaipata nafasi ya kuwakilisha mashindnao ya Europa League msimu ujao. Katika nafasi ya tano yupo Juventus ambayo imecheza mechi 32 na kupata pointi 59. Nafasi ya saba yupo AS Roma ambayo imejikusanyia pointi 57 katika mechi 33. Nafasi ya nane yupo Lazio ambaye amefanikiwa kukusanya pointi 56 kutokana na michezo 32. Nafasi ya tisa yupo Fiorentina mwenye pointi 53. AC Milana wanashikilia nafasi ya tisa wakiwa na pointi 51 kutoka na michezo yake 32. Torino wao wanashikilia nafasi ya kumi wakiwa na pointi 40 na wanazidiwa pointi 19 na Juventus. Kwahiyo vita ya kuwakilisha Europa League itabaki kwa vigogo wengine Juventus, AS Roma na Lazio. Wakati kwenye Conference League kitakuwa kibarua cha Fiorentina, AC Milan na Torino.
Bingwa Serie A
Kimahesabu Inter Milan na Napoli timu yoyote inaweza kuchukua ubingwa msimu huu. Timu zote mbili kama nilivyoeleza mawanzoni zina pointi sawa (71) ikiwa na maana nafasi ya kuchukua ubingwa iko mikononi mwa kila mmoja. Kilichobakia ni kuombea adui afungwe kwenye mechi zilizosalia. Wakati huo Atalanta atakuwa anawinda taji hilo kimya kimya, kwani anazo pointi 61 kwa kuzidiwa pointi 9 na vinara wa Ligi hiyo.
Ligi ya Mabingwa
Timu mbili zina uhakika wa kufuzu Ligi ya Mabingwa, Inter Milan na Napoli, huku nafasi mbili zilizobakia zitagombaniwa na Atalanta, Bologna na Juventus na Roma. Msimu huu Inter Milan imetinga hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa. Vijana wa Simeone Inzaghi wameendelea kuonesha makali yao katika Ligi ya nyumbani la Ligi ya Mabingwa ni wazi shughuli yao msimu huu ni kubwa.
Kupoteana kwa AC Milan
Kati ya timu ambazo zinasononesha ni AC Milan. Timu hiyo ni mabingwa mara 7 wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, lakini msimu huu inahangaika hata kupata nafasi ya kuwakilisha Italia kupitia Conference League au Europa League. Uwezekano wa AC Milan kufuzu Ligi ya Mabingwa hautakuja kirahisi kwa sababu wanazidiwa pointi 9 na Bologna huku katikati yao kukiwa na Juventus, Roma, Lazio na Fiorentina zinazowinda nafasi hiyo.
Simeone Inzaghi na mataji mawili
Hadi sasa Inter Milan haipo mbali na mataji mawili; Ligi Kuu Italia wanaongoza kileleni na Ligi ya Mabingwa Ulaya wapo nusu fainali. Hii ina maana kocha Simeone Inzaghi anaelekea kuwinda mataji mawili makubwa katika soka. Kuwatupa nje Bayern Munich kwenye mashindano ya Ulaya ni dhahiri imewajengea ari zaidi kuwa chachu katika uwezo wao. Ikumbukwe walishinda mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa ugenini Allianz Arena nchini Ujerumani na kudhihirisha kuwa wanaweza kushinda mchezo katika uwanja wowote. Sasa kimahesabu kuanzia Serie A hadi Ligi ya Mabingwa unaona bayana Inter Milan wamekaribia mataji mawili makubwa msimu huu.
Comments
Loading…