in , , ,

Fainali ya Kibabe Ligi Mabingwa Afrika

HATIMAYE mbio za kuwania taji la Ligi ya Mabingwa Afrika inakaribia kufika tamati huku timu zitakazokutana kwenye michezo ya fainali zimejulikana kuwa ni Mamelodi Sundowns ya Afrika kusini na Pyramids Fc ya Misri. 

Timu hizo zilifuzu hatua ya fainali wikiendi hii baada ya kushuhudia mechi kali na kusisimua pamoja na kujaa ufundi wa hali ya juu kutoka kwa pande zote mbili. Michezo ya Nusu Fainali ilikuwa kivutio cha aina yake huku timu zote zikionesha na kueleza sababu za wao kutinga hatua hiyo kwenye mashindano ya CAF. Haikuwa nusu fainali rahisi kwa pande zote mbili ambapo timu zilihitaji nguvu ya ziada ziweze kufuzu fainali hiyo.

Fainali ya mgeni na mwenyeji

Pyramids fc ni klabu ya Misri. Timu hii imefuzu hatua ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa mara ya kwanza katika historia yake. Ni sawa na kusema katika mchezo wa fainali utashuhudia mgeni katika mchezo wa soka dhidi ya mwenyeji wa mashindano hayo. Mamelodi Sundowns si wageni wa mashindano hayo, wakiwa na rekodi ya kutwaa kombe hilo chini ya kocha mahiri duniani Pitso Mosimane. 

Tanzania Sports

Katika fainali hii inakwenda kushuhudia mgeni Pyramids akiwa anapambana na timu kubwa ama dude la kutisha ambalo limekuwa jinamizi kwa klabu nyingi za Misri, Mamdelodi Sundowns. Timu ya Mamelodi Sundwosn imewahi kuichabanga National Al Ahly ya Misri kwa mabao 5-1 katika moja ya mechi walizowahi kukutana kwenye mashindano ya CAF. Kwahiyo Pyramids wanakwenda kuvaana na timu inayogopeka Afrika na yenye sifa ya kushinda mchezo mahali popote pale.

Vita vya Misri na Afrika Kusini

Kama kuna vita vya mafanikio katika klabu za Afrika basi pande mbili kutoka Afrika kaskazini na Afrika ya kusini au nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara. Katika mashindano ya CAF timu za Afrika kaskazini ambazo sehemu kubwa ni za Waarabu zimekuwa na mafanikio makubwa na washindani wao mara nyingi wamekuwa timu za kutoka Kusini mwa Jangwa la Sahara. 

Miaka ya 1990 na mwanzoni mwa 2000 timu nyingi za Afrika Magharibi kama vile nchi za Ghana, Nigeria, Cameroon, Benin, Ivory Coast, Togo na nyinginezo zilikuwa zikitamba kwneye mashindano ya CAF. Chukua mfano Enyimba FC ya Nigeria, namna ilivyowahi kutetemesha vigogo wa soka barani Afrika ,lakini ikaja kupotea. 

Nyingine Asec Mimosas ambayo ilikuwa kinara wa kuibua vipaji vilivyotamba barani Ulaya na walikuwa wababe wa soka katika mashindano ya CAF. Ushindani ule ukahamia nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara, Simba imezietetemesha timu kadhaa za Misri kama vile Al Ahly, Zamalek, Arab Cotractors, Ismailia na kadhalika. 

Kwa miaka ya karibuni vita vya soka kati ya Afrika Kusini na timu za Misri vimekuwa vikubwa. Timu zinashindana, zinchapana mabao, zinatoana kwenye mashindano na za zinakuwa na bajeti nzuri kiuchumi, pamoja na malipo ya mishahara minono. Mamelodi Sundowns ni miongoni mwa timu zenye fedha nyingi na tahamani yake imekuwa kubwa kadiri wanavyosonga mbele. 

Ni timu yenye ukwasi wa kutosha na inaweza kupambana na Al Ahly sokoni pale inapomtaka mchezaji mahiri. Al Ahly ina misuli mikubwa ya fedha sawa na Zamalek, Al Masry, Pyramids na nyingine, ni sawa na kusema timu za Misri au Afrika kaskazini zina ukwasi mkubwa. Hata hivyo Mamelodi imeonesha yenyewe ni mbabe wa timu za Misri na aimefanya hivi kwa kuivua ubingwa Al Ahly baada ya kutoa sare 1-1 kwenye mchezo wao wa marudiano katika dimba la Kimataifa ya Cairo (Cairo International Stadium). 

Pyramids wao wametinga fainali hiyo baada ya kuwatoa wababe wengine kutoka Afrika kusini, Orland Pirates kwa mabao 3-2. Katika mchezo huo uliokuwa na ushindani mkali, ulionekana kama vile ungemalizika kwa sare 2-2 lakini Fiston Mayele alipachika bao la ushindi na kuivusha timu yake kwenye fainali. Kwahiyo nusu fainali ya pili ilihusisha timu toka Misri dhidi ya Afrika Kusini.

Fainali ya pili kwa Miguel Cardoso

Kocha wa Mamelodi Sundowns, Miguel Cardoso ameandika rekodi ya kipekee baada ya kuifikisha timu yake katika hatua ya fainali ilikuwa ni mwaka wa pili mfululizo. Msimu uliopita Miguel Cardoso alikuwa kocha wa Esperance ya Tunisia ambapo walitinga hatua ya fainali kabla ya kufungwa na Al Ahly ya Misri. 

Uwezo wake wa kusoma mchezo na kupanga timu umekuwa sifa ya pekee. Miguel Cardoso alichukua nafasi ya Rhulani Mokwena ambaye alishindwa kuipata taji la Afrika klabu hiyo baada ya kuishia hatua ya nusu fainali. Katika hali ya kusisimua ni kwamba kwenye hatua ya Nusu fainali Mamelodi walitupwa nje na Esperance msimu uliopita wakiwa na Miguel Cardoso. 

Mabosi wa Mamelodi waliamua kumwajiri Cardoso kuchukua nafasi ya Rhulani Mokwena. Hii inakuwa fainali ya pili ambapo Crdoso anakwenda kukabiliana na timu nyingine ya Misri kama ilivyokuwa msimu uliopita alipokabiliana na Al Ahly. 

Je msimu huu Miguel Cardoso atafuta machozi yake na kufikia rekodi ya Pitso Mosimane kunyakua taji la Ligi ya Mabingwa Afrika? Kwa hakika hili ndilo linalosubiriwa na ndiyo sababu ya kuajiriwa kwake katika kikosi cha Masandawana. Ni jambo la kusubiri na kuona.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

68 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

Ni kama Arsenal wamepewa ubingwa UEFA

Tanzania Sports

Nuno Santo alivyoiokoa Nottingham Forest