in , , ,

Ni kama Arsenal wamepewa ubingwa UEFA

KAMA kuna timu imekuwa gumzo kwenye hatua ya nusu fainali basi Arsenal ndiyo imepewa nafasi kubwa kwneye mijadala ya kandanda barani Ulaya. Washindani wengine wa Ligi ya Mabingwa Ulaya ni PSG ya Ufaransa, Inter Milan ya Italia na Barcelona ya Hispania. Katika orodha hii Barcelona si mgeni kwenye mashindano hayo wala suala la ubingwa. Barcelona wanayo rekodi ya kutwaa mataji ya Ulaya. 

Kwa muda miaka 10 na zaidi hawajachukua ubingwa huu kama ilivyo kwa Inter Milan ambayo imeishi miaka 15 bila ubingwa. PSG hii ni mara yao kwanza kufikiria kutwaa taji hili wakiwa na matumaini makubwa baada ya kutinga nusu fainali. Misimu mingine walipewa nafasi ya kufanya vizuri kwenye mashindano lakini si kuibuka mabingwa. Kilicholeta tofauti msimu huu ni aina ya kocha waliyenaye na kikosi alichokitengeneza. 

Luis Enrique ni kocha wa zamani wa AS Roma, Barcelona na timu ya Taifa ya Hispania anao uzoefu mkubwa kwneye mashindano ya Ulaya. Ameifikisha PSG katika hatua ya nusu fainali kwa aina yake. PSG wanacheza kandanda safi lakini wanayo changamoto ya kulinda lango lao, ni sababu hiyo waliruhusu mabao mawili ndani ya dakika mbili kwenye pambano la marudiano dhidi ya Aston Villa. Pamoja na sifa zote wanazopewa PSG, Inter Milan na Barcelona kuna wengine wanatazama nusu fainali hii kwa jicho ala aina yake. 

Miongoni mwao wapo makocha ambao wanachambua timu zilizopo nusu fainali hasa Arsenal na kuelezea kuwa inawakilisha soka la Kiingereza. Walimu mbalimbali wanakiri kuwa mashindano ya UEFA Mwaka huu yameileta Arsenal na kuwapa heshima kwenye ulimwengu wa kandanda na kwamba halitakuwa jambo la kushangaza ikiwa watakuwa mabingwa wa mashindano hayo. 

Vituo vya redio, Televisheni, magazeti, mitandaoni yaani kila mahali inazungumzwa Arsenal kwa namna chanya na pongezi nyingi zinakwenda kwa benchi la ufundi.

Je kwanini ni rahisi kwa Arsenal?

Ifahamike kwenye mashindano ya UEFA, Real Madrid ndiyo timu inayoongoza kwa kutwaa mataji mengi zaidi. Madrid wameshinda UEFA mara 15 huku wakifuatiwa na timu zilizoshinda mara 7 na nyingine 5. 

Wataalamu wa soka wanasema ikiwa kwenye mashindano hayo Real Madrid imetolewa basi uwezekano wa kila timu zilizobaki kutwaa ubingwa ni rahisi. Inasmekana kuwa ikiwa Real Madrid ikitinga nusu fainali, huwa inakuwa vigumu kuiondoa mashindano, na endapo itaondolewa katika hatua hiyo basi timu zinakuwa na ahueni mkubwa. Lakini kama Real Madrid ikitinga hatua ya fainali maana yake ubingwa unahesabika kuwa ni mali yao. inasemwa Real Madrid wakiliona kombe la UEFA basi damu zao zinawasha kunyakua.

Hata hivyo msimu huu Real Madrid imetupwa nje ya mashindano na Arsenal katika hatua ya robo fainali hivyo kujiandikia rekodi ya pili ya kutuipa timu hiyo kwenye mashindano ya UEFA kila wanapokutana. Mara ya kwanza walikutana mwaka 2006 ambapo Arsenal iliifunga Real Madrid 1-0 na kutinga hatua ya fainali ambako walifungwa na Barcelona kwa bao la lala salama la Juliano Belleti. 

“Msimu huu Arsenal wameboresha uwezo wao katika kujilinda. Wao ni timu ya Uingereza na inawakilisha soka la EPL. Timu pekee ambayo inacheza vema ni Manchester City kwa sababu ya mtindo wa Pep Guardiola. Lakini kama uwezo kuwakilisha EPL, Arsenal wameonesha na wana kila sababu ya kupambana vyema kwenye mechi zilizobaki,” ni moja ya kauli zinazovuma kwenye mijadala ya soka.

Kimsingi ni rahisi kwa Arsenal kutwaa taji hilo kwa sababu Real Madrid haipo mashindanoni. Arsenal wana kila sifa ya kuwa mabingwa wa Ulaya kwa uwezo wao, kiufundi na uimara wa wachezaji wao. Hii ni sifa muhimu kutwaa ubingwa, kujilinda vizuri na kufunga mabao.

Je Arsenal wanaweza kuwafunga PSG?

PSG walifungwa mabao mawili ndani ya dakika 2 kwenye mchezo wao wa robo fainali dhidi ya Aston Villa. Uchezaji wao unaonesha kuwa hawana ngome ngumu kama ya Arsenal, kwahiyo wanaweza kuruhusu mabao muda wowote. Kulingana na wataalamu wa mchezo wa soka wanasema, “kwa kuzichambua timu zote mbili, zinafanana, lakini Arsenal wana jambo lingine la ziada kwa kipindi hiki. 

Arsenal wana ubora na nguvu za miili ya wachezaji wao, wanacheza pamoja kama timu yenye muunganiko imara, wanashambulia pamoja, wanajilinda pamoja na mechi zao zina kasi kila wanapocheza. Si suala la kukamia timu fulani lakini wao wanacheza kwa kasi mechi zote, hilo litakuwa faida kwao kwa vile wamezoea. Kwahiyo hii ni mechi nzuri ambayo mashabiki wataona mchezo mzuri,” amesema mmoja wa wataalamu aliyezungumza na TANZANISPORTS.

Tofauti ya Arsenal na PSG ni ipi?

Kwanza wanatofautiana katika suala la mipango ya mechi. Arsenal wanajikusanya wote, wanasogea eneo la katikati ya dimba, wanashirikiana kwa kulinda na kushambulia. Ni kama timu ambayo inacheza ‘Total Football’ ya Waholanzi enzi hizo. Uchezaji wao unawapa nafasi nzuri ya kujenga ushirikiano. Kama timu, wanaweza kwenda kulinda,kucheza kiungo na kadhalika. Safu ya ushambuliaji inabadilika badilika kwa sababu hawana mshambuliaji kamili kwahiyo kunakuwa na mabadiliko ya ndani kutokana na kasi zao.

PSG wanategemea kasi binafsi ya wachezaji wao hasa Ousmane Dembele, kisha kwenye kiungo wanategemea uimara wa Vitinha na umahiri wa golikipa wao Donnaruma. Lakini kwa vile nao wanacheza mchezo wa kasi, ni dhahiri watakuwa na wakati mgumu kuhakikisha wanawazuia Asrenal kucheza kwa mtindo huo. 

Maeneo mawili ya PSG yenye hatari ni winga wa kulia na kushoto. Huko wanaweza kuwaathiri Arsenal lakini si rahisi kukabiliana na walinzi wao wa pembeni. Kwa maana hiyo tofauti yao kubwa ipo kwenye uwajibikaji yaani jinsi timu inavyocheza kushambulia na kujilinda. Suala la kujihami Arsenal si habari tena, wanao uwezo wakujihami kwa kiasi kikubwa kuliko PSG.  Tofauti hizi ndizo zitafafanua michezo yote miwili.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

70 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

Ubingwa Serie A bado mbichi

Tanzania Sports

Fainali ya Kibabe Ligi Mabingwa Afrika