Katika chumba cha makombe cha klabu ya Nottingham Forest kuna mawili ambayo yanatengeneza historia yao. kwenye chumba cha timu hiyo kuna makombe mawili ya Ulaya yakiwa yanatumika kama nyenzo ya kuhamasisha wachezaji wanaosajiliwa na wa sasa. Hata hivyo kwenye chumba hicho hakuna kombe la FA.
Taji la mwisho la Nottingham Forest walichukua mwaka 1959 wakiwa chini ya kocha Brian Clough ambaye alifariki dunia mwaka 2004. Hata hivyo Nottingham Forest wanayo fursa ya kutwaa taji la FA endapo wataishinda Manchester City katika mchezo wa nusu fainali jumapili wiki hii. Kisha watakwenda kushinda mchezo wa fainali na kunyakua kombe hilo ambalo litakuwa fursa kwao kwa msimu mzuri walionao hadi sasa.
Forest wanavaa jezi zao zenye nyota mbili kuashiria mataji mawili ya Ulaya. Lakini tangu walipichukua makombe hayo hawajarudi tena kwenye ubora wao na kujinyakulia taji lingine. Katika mchezo wa soka wakati mwingine timu inaweza kupotea katika ramani yamafanikio kwa muda mrefu.
Pia huchukua muda mrefu sana kwa timu kurudi kwenye mafanikio kwa sababu mbalimbali ikiwemo mabadiliko ya uongozi, kukosa wachezaji mahiri, ukosefu wa bajeti kwa maana ya uwekezaji hafifu. Lakini msimu huu Nottingham Forrest wana fursa ya kuandika historia nyingine ikiwa watafanikiwa kuntaa taji la FA.
Ili kuwa na bahati ya kutwaa kombe hilo, wafanyakazi wa Nottingham Forest wamefanya kazi ya ziada katika kipindi cha Paska baada ya kukusanya soksi na vitu vingine na kwenda kutoa msaada kwenye vituo vya kulelea watoto takribani 1,000. Kipindi cha pasaka kulikuwa na watazamaji wengi waliovunja rekodi ya kutembelea Makumbusho ya Nottingham Forest.
Wiki chache zijazo kuanzia sasa watu wataanza kusikia habari za upanuzi wa uwanja wa klabu hiyo. Ingawaje akili za klabu zimeelekezwa kwenye mechi za EPL na FA zilizopo mkononi mwao lakini klabu hiyo imeweka bayana mipango yake ya ndani na mashabiki na wanachama watafahamishwa hivi karibuni. Nottingham Forest wanatupia jicho kombe la FA kama ndilo ambalo kocha wao shujaa Brian Cliugh hakuwahi kulichukua na wanapanga mikakati ya kufuzu kwa mashindano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.
Katika klabu ya Nottingham Forest wanafahamu kuwa mashindano ya Ligi ya Mabingwa ndiyo yalimpa hshima shujaa wao Brian Clough na sasa wamebakiza hatua chache kutimiza ndoto zao; kurudi kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa na kutwaa kombe la FA. Kwa sasa wanafundishwa na kocha Nuno Espirino Santo raia wa Ureno.
Matumaini makubw aya mashabiki na wanachama wa Nottingham Forest yapo mikononi mwa kocha huyo. Huyu nidye kocha anayeonekana kama Malaika mwokozi kwao, kuliko yule aliyekuwa akiufndisha Tottenham Hotspurs akionekana kama mzimu tu. Katika kazi ya ukocha upo wakati kocha anafundisha timu huku akiwa na matokeo mabaya sana klabuni kwake. Lakini tangu alipotua Nottingham Forest amekuwa kocha anayeishi katika ndoto zake na anautamani ukocha wake kila muda ulete furaha kwake na watu wengine wanaoizunguka klabu hiyo. Matumaini yao yatimizwe kutokana na utaalamu wake.

Nuno Espirito Santo ndiye anayeheshimika zaidi Nottingham Forest kwa sababu ameifanya timu iwe hatari na sasa inagombania nafasi nne za juu ili kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Maelfu ya mashabiki wa Nottingham Forest wanaamini timu yao itatinga fainali ya FA kwenye dimba la Wembley. Matumaini yao ni makubwa na sababu kubwa ni Nuno Espirito Santo amewafanya waamini inawezekana katika jitihada zao.
“Tunajihisi kwenda Wembley, ni kama zimebaki saa 48 kutinga fainali Wembley, kwanza ni heshima kwa klabu yetu, ni mafanikio makubwa kwa sababu klabu hii imewahi kufanya mambo makubwa sana na yote yanaonekana bayana. Kwahiyo tupo tayari kwa kupokea furaha hii, tunaamini kuna kitu tunakwenda kukiweka kwenye chumba cha makumbusho, lazima tujivunie kuwa Nottingham Forest” alisema mtumishi mmoja wa klabu hiyo.
Nuno Espirito Santo si kocha mwenye makeke kwenye vyombo vya habari. Waandishi hawamtaki sana kwa sababu hawapi mada za kuzungumzia au hatengenezi vichwa vya habari vya vyombo vyao. Kwahiyo wanamwona kama mtu mkimya ambaye hana muda wa kuzungumza zungumza. Ni kocha ambaye anatajwa kuzungumza kupitia macho yake kwani huangalia vitu vingi katika timu yake bila kuzungumza au kuweka wazi maoni yake.
Daima amekuwa mtu mwenye tabasamu, kila wakati na haijalishi ni mgumu au mzuri, yeye hutabasamu. Ndani ya Nottingham Forest amekuwa maarufu kwa mtu mwema na mzuri kwa kila anachokifanya na kuwaachia wengine somo muhimu na deni la kuishi katika wema. Hapendelei kutawala kila sehemu. Mara nyingi anafanya kazi ya kuhakikisha anadhibiti hisia za wachezaji pale anapoona furaha imepitiliza kuliko kazi.
Kwa mfano aliwasilisha maombi ya kupunguza muda wa kuwatumia wachezaji kwenye shughuliza vyombo vya habari kama vile mahojiano na vitu vingine, sababu ya kufanya hivyo ni anataka kuwasimamia wachezaji hao katika maezoezi na ufundi na kwamba akili zao zielekezwe kwenye eneo hilo kuliko kuitwa kuzungumza na vyombo vya habari kuhusu mechi yao na Manchester City jumapili hii.
“Wachezaji wote wataambatana na timu kuelekea kwenye mchezo. Baadhi wataachwa jukwaani, lakini ni muhimu sana kuwa pamoja kama timu.” Alisema Nuno
Uamuzi huo umekuja baada ya kocha huyo kuwakosa wachezaji wake wawili, Ryan Yates na Neco Williams ambao wanatumikia adhabu ya kadi.
Kimsingi kocha huyu anatupia jicho kufuzu Ligi ya Mabingwa msimu ujao, huku akiungwa mkono na mmiliki wa klabu hiyo Evangelos Marinakis. Nuno ampenia kufuzu Ligi ya Mabingwa kuliko kufikiria kutwaa taji la FA. Endapo klabu yake itafuzu kwa mashindano ya Ulaya mfano Europa League watapata kiasi cha pauni milioni 90 msimu ujao ambazo zinaweza kutumika kuimarisha kikosi chao kwa kuleta wachezaji wapya.
Lakini mchezo wa soka umebeba hisia nyingi kwani Nottingham Forest walilikosa kombe la FA mwaka 1991 na tangu hapo hawajawahi kutinga fainali ya kombe hilo. Kwahiyo inawezekana pia FA inaweza kuwaletea kumbukumbu nzuri.
Comments
Loading…