in , , ,

Miguel Cardoso kupona rungu la Mamelodi ?

Kufungwa jumla ya mabao 3-2 na timu ngeni kwenye mashindano ya Ligi Mabingwa Afrika na kukosa ubingwa huo ni ishara ya kufeli kwa kocha wa Mamelodi Sundowns kulingana na vigezo vya timu hiyo. Mamelodi Sundowns ni timu yenye matarajio ya hali ya juu na kocha anapoajiriwa anapewa malengo ya kutimiza. 

Malengo ya Mamelodi Sundowns msimu huu yalikuwa kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Afrika. Isivyo bahati msimu huu umemamlizika kwa klabu hiyo kutoshinda taji lolote.

TANZANIASPORTS inafahamu kuwa mashindano ya Ligi ya Mabingwa kwa Mamemlodi Sundowns ni muhimu na ndicho fahari yao kutwaa taji hilo. 

Pia inafahamu kuwa maudhi waliyopata mashabiki wa Mamelodi Sundowns ni kufungwa na timu ngeni, Pyramids ambayo imeshiriki mara tatu tu kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa. Ikiwa na maana msimu ni wa tatu kwa klabu hiyo kushiriki Ligi ya Mabingwa. Lakini Mamelodi wana uzoefu mkubwa katika Ligi ya Mabingwa na wameshacheza fainali tatu sasa. 

Makosa ya Cardoso

Kama kuna kosa ambalo kocha Sundowns amelianzisha ni kitendo chake cha kumweka benchi mshambuliaji wa klabu hiyo Themba Zwane pamoja na Peter Shalulile. Katika mechi akdhaa Themba Zwane amesugua benchi, huku mwenzake Peter Shalulile akianzia benchi na kupewa dakika chache uwanjani. Jambo hilo limemletea ugomvi na mashabiki ambao wanaamini kocha huyo ndiye chanzo cha timu yao kukosa ubingwa msimu huu.

Nyota wa zamani wa Mamelodi Sundowns Joel Masilela ameiambia jarida la The KickOff kuwa kocha Miguel Cardoso anatakiwa kufukuzwa katika kibarua chake kwa kuendelea kmweka benchi Themba Zwane bila sababu zozote za kiufundi. 

Nyota mwingine wa zamani wa Kaizer Chiefs, Doctor Khumalo aliiambia Goal South Africa, kuwa Miguel Cardoso ndiye sababu ya timu hiyo kukosa ubingwa. Khumalo alisema kuwa Mamelodi Sundowns  walihitaji mchezaji wa kutuliza mchezo wa timu na kuwadhibiti wapinzani wao kutokea eneo la kiungo.

Kocha huyo amelalamikiwa kuwapendelea Tashreeq Mathews na Jayden Adams badala ya kupanga mshambuliaji wa magoli Shalulile na Zwane. Pengine sifa ambayo anatakiwa kupewa ni kuifikisha fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambayo walikosa tangu mwaka 2016 ambapo walichukua taji hilo chini ya kocha Pitso Mosimane.

Rungu la mabosi wa Sundowns

Rekodi za mabosi wa Mamelodi Sundowns nazo zinamnyima nafasi ya kuendelea kubakia kikosini hapo. Miguel Cardoso alijiunga na Mamemlodi Sundowns akitokea klabu ya Esperance ya Tunisia. Msimu mmoja nyuma aliwaongoza Esparance kuwatupa nje Mamelodi Sundowns katika hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika. 

Licha ya kutinga fainali hiyo Esperance ilifungwa na Al Ahly ya Misri. Mabosi wa Mamelodi waliamua kumwajiri kocha huyo kama njia ya kutaka makombe ya CAF kuwasili klabuni hapo na wakamtupia virago kocha Rhulani Mokwema kwa madai ya kushindwa kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Afrik mara mbili. 

Chini ya Rhulani Mokwena, Mamelodi Sundowns iliishia nusu fainali mara mbili; nusu fainali ya kwanza ilikuwa msimu wa 2022/2023 ambapo walitupwa nje ya Wydad Casablanca ya Morocco na msimu uliopita walitolewa na Esperance ya Tunisia. Kwenye benchi la Mamelodi Sundwons kwa sasa lipo chini ya Miaguel Cardoso, Paulo Cardoso na Steve Komphela.

Mashabiki na wadau wa soka wameshauri kuwa Thlopie Motsepe anatakiwa kumtimua kocha huyo pamoja na Afisa Mtendaji mkuu, Berg Flemming kuwa wamechangia timu yao kukosa ubingwa.

Kibarua cha makocha Sundowns

Makocha wengi katika klabu ya Mamelodi wamekuwa wakifukuzwa kwa kile kinachosemekana kushindwa kufikia malengo ya klabu. Tangu kuondoka kwa Pitson Mosimame hakuna kocha ambaye amefanikiwa kufikia rekodi yake kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Afrika. Bahati mbaya zaidi msimu huu Mamemlodi wamemaliza patupu hali ambayo inawachanganya mashabiki wa soka nchini humo. Kutokana na hali hiyo swali linalobakia sasa ni kama Miguel Cardoso ataepuka rungu la mabosi wa Mamelodi. Vigezo vilivyotumika kuwafukuza makocha waliopita vimetimia kwa Miguel Cardoso , ni suala la viongozi kuchukua hatua na kutekeleza. 

Kama uongozi wa Mamelodi utashindwa kumwadhibu kocha huyo kwa kumfukuza maana yake kuanzia Afisa mtendaji mkuu Ber Flemming walikuwa wanaonea makocha wazawa akina Steve Komphela na Rhulani Mokwema sababu ya rangi na utaifa wao. Hapo ndipo ulipo mtego kwa Mamelodi, huku amshabiki na wadau wa soka wakiendelea kulalamikia kazi ya Cardoso katika klabu hiyo haina mafanikio katika msimu wake wa kwanza. Hadi sasa uongozi wa Mamelodi haijasema lolote tangu wapoteze fainali ya Ligi ya Mabingwa mbele ya Pyramids.

Report

Written by Israel Saria

I have been involved with sports in Tanzania as a Volleyball Coach for many years—and was a Tanzania Amateur Volleyball Association (TAVA) leader. I studied sports management at Leipzig University in Germany and understand the science behind sports. That led me to work as a football pundit, with the BBC ( Swahili service) in London. That experience and exposure took me to covering the 2010, World Cup in South Africa. This provided me with a great insight into international level football commentary and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics.I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany, Italy, Belgium, Ireland, France, Kenya etc, and visited almost all of the key football stadiums across United Kingdom, and Europe.

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

Inter Milan, PSG ulikuwa ufundi na umri

Tanzania Sports

Ni ipi taswira ya Kombe la Dunia la klabu?