in , ,

Bahati iko mbali ya ubora wa Rhulani Mokwena? 

MSIMU wa Ligi Kuu Morocco umefika tamati, lakini moja ya mambo yanayosikitisha ni kuona kigogo wa soka nchini humo klabu ya Raja Casablanca ikiwa nafasi 6 kuliko inavyotegemewa. Raja Casablanca ni miongoni mwa timu zenye sifa nyingi lakini imekwama kupata nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao. 

Hata hivyo majirani zao Wyadad Casablanca watakuwa wawakilishi wa Morocco kwenye Ligi ya Mabingwa msimu ujao kwani wamemaliza nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu nchini humo. Wakati unawafikiria Raja Casablanca ni vyema ukageukia ndugu zao Wydad, ambao walilazimika kumwajiri Rhulani Mokwena kuwa kocha mkuu ili kuipa taji klabu hiyo. Jitihada za Rhulani Mokwena kuipaisha timu hiyo kimafanikio zimeishia katika nafais ya tatu. 

Viongozi na mashabiki wa Wydad Casablanca wana uhakika msimu ujao watakuwa kwenye Ligi ya Mabingwa lakini wamechukua uamuzi ambao unashangaza katika ulimwengu wa soka. Wakati Wydad wakimchukua Mokwena hawakuwa na makali yoyote ya kupambania ubingwa ama kushiriki mashindano ya Ligi ya Mabingwa. 

Jitihada za kocha huyo na benchi lake la ufundi lilimewawezesha kumaliza ligi wakiwa nafasi hiyo kutoka nafasi ya 6 waliyokuwa nayo awali. Kwahiyo kutinga katika tatu bora si hatua mbaya ama huwezi kusema kocha amefeli. 

Hata hivyo hivi karibuni Rhulani Mokwena akizungumza na vyombo vya habari alisema anaondoka katika klabu ya Wydad mara baada ya kukamilika msimu wa Ligi yao. Mokwena alisema anaamini klabu ya Wydad inahitaji kocha mkubwa kuzidi yeye ambaye anaweza kufanya mambo makubwa kuliko yeye. Kwenye mahojiano hayo alimsifia Rais wa klabu ya Wydad akisema ni kiongozi bora kuliko wote na anajua maana ya mpira. 

Kauli ya Mokwena iliibua hisia tofauti ambapo wengi wa wachambuzi walistaajabu kwani ilitolewa huku akiwa chini ya mkataba. Hata hivyo siku chache baadaye klabu ya Wydad ilithibitisha kuwa Rhulani Mokwena anaondoka klabu hapo na wao wataanza jukumu la kuajiri kocha mwingine. Haijafahamika kuwa kocha huyo anaatjiwa timu gani lakini upo uwezekano akarejea nchini kwao Afrika Kusini. 

Alipoondoka, pameng’ara

Kuna wakati unaweza kushangaa mchezaji fulani anaondoka katika klabu yake kwa madai haoni uwezekano wa kutwaa mataji makubwa. Mfano wa karibuni ni Kylian Mbappe aliondoka PSG msimu huu akiwa na ndoto za kuichezea Real Madrid na kutwaa Ligi ya Mabingwa Ulaya. Hata hivyo msimu wake wa kwanza ametwaa Super Cup ya UEFA na Super Copa, huku klabu yake mpya ikitupwa kwenye mashindnao ya Ulaya katika hatua ya robo fainali na Arsenal. Wenzake PSG wametinga nusu fainali na wamebakiza mguu mmoja kutinga hatua ya fainali ya Ligi ya Mabingwa. 

Mchezaji mwingine ni Michael Owen ambaye aliondoka Liverpool kufuata mataji ya UEFA katika klabu ya Real Madrid, lakini mwaka alioondoka ndiyo uliwapa Liverpool taji la Ligi ya Mabingwa. Yaani Owen hakutaka kuwepo klabuni hapo kwa msimu mpya hivyo alihamia Real Madrid, lakini kuondoka kwake alipishana na ubingwa wa UEFA ambao hajawahi kutwaa hadi leo. 

Jose Mourinho alifanya jitihada nyingi kuhakikisha Real Madrid inachukua makombe lakini alishindwa licha ya kuwa na kikosi kizuri na alitolewa nusu fainali kwa matuta. Kuondoka kwake nafasi yake ilikwenda kwa kocha mwingine, na kuanzia hapo Real imetesa kwenye mashindano ya UEFA kana kwamba Mourinho alikuwa kizuizi.

Kuondoka kwa Rhulani Mokwena katika klabu ya Mamelodi Sundowns kulimpa nafasi Miguel Cardoso. Tangu alipopokea mikoba ya kuinoa Mamelodi Sundowns kocha Miguel Cardoso ameandika rekodi ya kipekee baada ya kuifikisha timu yake katika hatua ya fainali ilikuwa ni mwaka wa pili mfululizo. 

Msimu uliopita Miguel Cardoso alikuwa kocha wa Esperance ya Tunisia ambapo walitinga hatua ya fainali kabla ya kufungwa na Al Ahly ya Misri. 

Uwezo wake wa kusoma mchezo na kupanga timu umekuwa sifa ya pekee.  Miguel Cardoso alichukua nafasi ya Rhulani Mokwena ambaye alishindwa kuipata taji la Afrika klabu hiyo baada ya kuishia hatua ya nusu fainali. 

Katika hali ya kusisimua ni kwamba kwenye hatua ya Nusu fainali Mamelodi walitupwa nje na Esperance msimu uliopita wakiwa na Miguel Cardoso. Mabosi wa Mamelodi waliamua kumwajiri Cardoso kuchukua nafasi ya Rhulani Mokwena. Hii inakuwa fainali ya pili ambapo Crdoso anakwenda kukabiliana na timu nyingine ya Misri kama ilivyokuwa msimu uliopita alipokabiliana na Al Ahly. 

Mwanafunzi wa Guardiola, Klopp

Pamoja na majaribio kadha ya kutwaa taji la Afrika lakini juhudi zake zilishindwa hadi alipohamia Wydad Casablanca ambako amedumu kwa msimu mmoja tu. Rhulani Mokwena ni mwanafunzi mahiri wa kocha Manchester City, Pep Guardiola. Pia ni mwanafunzi mzuri wa kocha mahiri Jurgen Klopp. Wakati Klopp alipokuwa kocha wa Liverpool, 

Rhulani Mokwena alipata bahati ya kutembelea klabu hapo na kujifunza masuala mbalimbali ya kiufundi. Mara kadhaa Mokwena alisema kupata nafasi ya kujifunza kupitia maandalizi na mazoezi ya Liverpool kulimpa wakati mzuri wa kupanga mbinu zake katika timu anayofundisha. Kwamba ufundishaji wa Jurgen Klopp ulikuwa unamvutia mno Mokwena, pamoja na mwingine Pep Guardiola. Timu ya Mokwena anapenda kuona inapiga basi nyingi za haraka, kasi na uwiano mzuri katika kujilinda. Ni timu ambayo inasisimua kuitazama inapofundishwa na Mokwena.

Hata hivyo licha ya kuwa karibu na makocha wakubwa duniani Rhulani Mokwena ametwaa taji la Ligi Kuu Afrika Kusini pekee na hajatamba Morocco katika msimu wake wa kwanza. Pili kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika hajafanikiwa kuandika jina lake kama mmoja wa makocha bingwa. Ni kama vile hana bahati licha ya kuwa kocha mwenye ubora na uwezo wa kuongoza timu.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

67 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

Fiston Mayele ubora unaibukia ‘uzeeni’

Tanzania Sports

Simba katika fainali kwa mkubwa mwenzake