in , , ,

Pep Guardiola ataisukaje upya Man City?

Pep Guardiola ataisukaje upya Man City?

Lakini mkataba wa kocha huyo umebakiza miaka miwili tu, tayari vyombo vya habari vimeanza kunusa taarifa nyeti za juu nini kitafanyika kubaki au kuondoka klabuni hapo….

KEVIN DE BRYNE si mchezaji kinda tena. Bernado Silva na Riyadh Mahrez wanaweza kuondoka Man City, na nahodha wao Ilkay Gundogan hana uhakika wa wapi atacheza msimu ujao. Kwahiyo, swali kubwa linaloulizwa sasa ni namna gani Pep Guardiola ataisuka upya timu yake ya Manchester City baada ya kunyanyua kwapa mara tatu msimu huu?

Pep Guardiola amebakiza miaka miwili katika mkataba wake, lakini ana wachezaji wengi ambao hatima yao haijulikani. Pep Guardiola anaweza kukipangua na kusuka upya kikosi chake na mara nyingi amekuwa akitazama mbali sana katika mpango wa kujenga timu mpya. Watu wengi wanachosubiri sasa ni kuona namna gani kocha huyo ataunda kikosi kipya kwa ajili ya msimu ujao na ndani ya miaka miwili ili kutwaa mataji matatu tena kama ilivyokuwa kwa kikosi alichonacho sasa. 

Tanzania Sports

Swali jingine ni wachezaji gani watabaki katika kikosi chake na nani watauzwa au kupewa mkono wa kwaheri. Kikosi ambacho kilianza kwa kutwaa taji moja, kikaongeza la mawili, kisha kimeleta mengine matatu msimu huu baada ya kuandika historia yao ya kwanza kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya hapo Juni 10 mwaka 2023, bila shaka kinahitaji mabadiliko. 

Lakini mkataba wa kocha huyo umebakiza miaka miwili tu, tayari vyombo vya habari vimeanza kunusa taarifa nyeti za juu nini kitafanyika kubaki au kuondoka klabuni hapo. Wakati Kevin De Bruyne alipolazimika kutolewa uwanjani baada ya kuumia misuli katika kipindi cha kwanza dhidi ya Inter Milan kulikuwa na hofu inayomzunguka nyota huyo. 

Hofu hiyo ni mustakabali wake kwani ndiye alikuwa mchezaji aliyejengewa timu kumzunguka yeye. Hivyo kuumia katika kipinid cha kwanza kulileta fikra kuwa huenda ndiyo mwisho wa nyota huyo katika soka. De Bruyne anatarajiwa kutimiza miaka 32 mwezi huu, ikiwa ni ujumbe anazidi kuongeza umri. 

Gaurdiola anatamani kuendelea kutwaa mataji lakini kibarua kigumu alichonacho sasa ni kumtengeneza Kevin De Bruyne mwingine yaani mchezaji tegemeo ambaye anakuwa msingi na muundo wa timu unamzunguka yeye. De Bruyne ndiye mgongo wa timu, kila mipango na mifumo inayopangwa yeye ndiye anayeibeba maono na namna timu inavyopaswa kucheza,kushambulia,kutafuta ushindi na aina ya wachezaji ambao wanamudu kucheza naye. 

Lakini kutolewa kipindi cha kwanza kwa kuumia ni ujumbe kuwa mambo yamefika tamati. Hivyo ni sawa na kusema kutakuwa na Manchester City bila Kevin De Bruyne, lakini kuumia misuli ni matokeo ya namna alivyo mchezaji muhimu katika mafanikio ya timu hiyo. Kevin ametengeneza mabao mengi kuliko mchezaji yeyote EPL, amekuwa mchezaji wa kikosi cha kwanza tangu alipojiunga na Man City kwa ada ya pauni milioni 55 mwaka 2015.

De Bruyne hayuko peke yake wa kufikiriwa Man City bila yeye. Kyle Walker, licha ya kuwa mchezaji mwenye kasi zaidi kuliko wote katika kikosi cha Man City, hivi karibuni ametimiza miaka 33. Hata chezaji aliyeibuka kuwa kipenzi kwa sasa John Stones akitoka beki hadi kuwa kiungo mkabaji anatarajiwa kutimiza miaka 30 mwakani. 

Halafu kuna swali jingine la nani ataondoka klabuni. Wakati Guardiola ameweka wazi kwamba anataka kuongeza nguvu katika kusaka mafanikio zaidi, bila kujali itakuwa na wachezaji gani au itaongozwa na nani kiwanjani licha ya Ilkay Gundogan kuibuka shujaa wa fainali ya kombe la FA kwa kufunga mara mbili, naye hatima yake haijulikani. Nyota huyo toka Ujerumani anamaliza mkataba wake mwezi huu wa Juni.

Tanzania Sports

Katika orodha hiyo yupo Mreno Bernado Silva huenda naye akaondoka klabuni hapo, huku nyota toka Algeria Riyadh Mahrez mwenye umri wa miaka 32 amewekewa dau kubwa na klabu ya Al Ahli ya Saudi Arabia ili akacheze Ligi Kuu ya nchi hiyo maarufu kama Saudi Pro League. Kwahiyo unaweza kuona wachezaji wengi waliofanikisha Man City kutwaa mataji matatu msimu huu hatima yao haijulikani klabuni.  

Bila kocha huyu na uwepo wa wachezaji hao pamoja na fedha nyingi wanazopata kutoka kwa mmiliki wake Sheikh Mansour bila shaka isingewezekana kwa timu hiyo kushinda mataji matatu. Kadiri muda unavyokwenda, Man City wanaonesha kuwa ni timu isiyojengwa kwa kutegemea mchezaji mmoja au kundi Fulani la wachezaji. Kimsingi Man City haina mwenyewe, wachezaji wanakuja kucheza na kuondoka lakini hakuna msingi wa kuwajenga wachezaji tegemeo. Hilo lina maana Man City wanakwenda sokoni tena kuingiza wachezaji wapya.

Turudi mwaka  2017 wakati beki mkongwe wa kulia raia wa Argentina Pablo Zabaleta alipokuwa anastaafu, ilionekana kuwa vigumu kumpata mwingine kwenye nafasi hiyo aliyoimiliki kwa muda mrefu. Wengi waliamini huenda ingekuwa pigo kubwa kwa Man City kumpoteza beki huyo. Lakini ujio wa Kyle Walker kutoka Totteham Hotspurs uliziba pengo lote lililoachwa na Zabaleta na kuongeza uimara zaidi. 

Guardiola amekuwa akibadilisha badilisha mara kwa mara wachezaji na kuwaruhusu kuondoka kama alivyofanya kwa Sergio Kun Aguero. John Stones anacheza nafasi ya kiungo kwa sasa. Mshambuliaji anarudi nyuma na kucheza nafasi ya nambari tisa feki. Sasa Erling Haaland amerudisha nafasi ya nambari tisa halisi. Kwahiyo mkusanyiko wa kikosi cha sasa hautegemei kuyumba ikiwa mmoja ataondoka au kuondolewa kwa sababu za kiufundi. Akiondoka mmoja anaingizwa mwingine kuboresha mbinu zao, inakuwa timu ambayo haina mwenyewe.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Kylian Mbappe na Neymar

Kirusi cha Mbappe kimerudi tena sokoni

Tanzania Sports

Ligi Kuu Tanzania kama Umoja wa Mataifa