in , , ,

Klabu EPL zapinga marufuku..

KLABU za Ligi Kuu ya England (EPL) zimepiga kura kupinga marufuku iliyoandaliwa kuzuia klabu zenye uhusiano kukopeshana wachezaji kwenye dirisha dogo la Januari mwakani.

Klabu zimepinga vikali pia mpango wa kuharakisha marufuku hiyo kutumika mapema kwa wachezaji wanaotakiwa kuingia kwenye ligi hiyo ya juu zaidi nchini England kutoka klabu yoyote yenye uhusiano na klabu takaji.

Mtandao wa The Athletic uliripoti mwezi huu kwamba klabu zote 20 zingepiga kura kupinga pendekezo hilo kwenye mkutano wa wadau.. hatua hiyo ya muda ilipendekezwa kwa ajili ya kulinda uadilifu wa kimashindano na kutoa muda wa kutafuta suluhu ya kudumu katika eneo hilo.

Kura hizo zilizopigwa katika Hoteli ya Churchil, Portman Square, London Jumanne zilitakiwa kuwa zaidi ya theuthi (klanu 14) ili pendekezo kupita au kukataliwa. Klabu 12 ziliunga mkono hivyo ependekezo husika kukwama, hivyo kanuni zitabaki zile zile hadi itakapoamuliwa vinginevyo.

Kwa sasa hakuna vizuizi kwa mchezaji yeyote kuuzwa katika dirisha kubwa au dogo au kufanyika makubaliano baina ya klabu kwa mchezaji kutolewa au kuchukuliwa kwa mkopo miongoni mwa klabu zenye umiliki mmoja, madhali inakubalika ndiyo thamani na uungwana katika soko.

Pamekuwapo tetesi kwamba Ruben Neves angehama kwa mkopo kutoka Al Hilal kuja Newcastle United — klabu mbili zinazomilikiwa na kampuni ya Saudi Arabia ya Public Investment Fund (PIF) — Januari mwakani. Hata hivyo, The Athletic ikaripoti Jumanne hii kwamba Neves hangetarajiwa kuhama kutokana na pendekezo tajwa.

Mpango huo haukuwa ukilengwa kimahsusi kumzuia Neves, bali ni sehemu ya mpango mpana zaidi unaotaka kuzuia klabu zenye uhusiano kufanya mipango kama hiyo. Klabu zenye uhusiano na nyingine nje ni pamoja na Manchester City, Chelsea, na nyingine kadhaa za EPL.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

Everton kupokwa pointi mtikisiko

Tanzania Sports

Ulafi EPL utawagharimu, huku hatima ya Man City..