in , , , ,

SAUDI PRO LEAGUE WANALETA VILIO EPL

Hilo lina maana wanaponunua mastaa kama Ruben Neves maana yake wanapunguza mvuto wa Ligi ya EPL….

ALEXANDER Ceferin, Rais wa Shirikisho la Soka Ulaya ni miongoni mwa wadau wa mpira wa miguu ambaye amesikika kulalamikia mwenendo wa matajiri wanaomiliki timu za Saudi Arabia kuwanunua wachezaji wa vilabu vya nchi wanachama wake.

 Pesa nyingi ya Waarabu imetua Ligi ya England ambako mastaa wanapewa ofa nono kujiunga na Ligi Kuu ya Saudi Arabia maarufu kama Saudi Pro League.

Mwingine aliyesikika akilalamika mikakati ya Saudi Pro League ni Nyota wa zamani wa Manchester United, Gary Neville. Wadau hawa wawili wanaungana na wengineo ambao wanalia lia juu ya hatua za Saudi Arabia. 

Wengi wanapendekeza kuwa Saudi Arabia haipaswi kununua mastaa wa EPL na Ligi zingine za Ulaya, badala yake wanatakiwa kuwa na mfumo madhubuti wa kujenga vituo vya kuibua vipaji vya soka kuliko kununua kwa kasi.

Wapinzani wa Sera ya Saudi Pro League wanataka kuona timu za huko zikimiliki Akademi za soka ili kukuza mchezo huo unaopendwa duniani. 

Kimsingi wadau wa mpira wa miguu England wamepata mshtuko wa kasi ya matajiri wa timu za Saudi Pro League kumwaga fedha kununua wachezaji wa EPL. Hilo lina maana wanaponunua mastaa kama Ruben Neves maana yake wanapunguza mvuto wa Ligi ya EPL. 

Fikiria Bernardo Silva amewekewa dau nono kujiunga Saudi Pro League. Kwa vyovyote mastaa wanaotaka Pesa lazima wazifuate Arabuni. 

Hata hivyo, vilio vinavyotolewa na wadau wa mpira wa England havizingatii ukweli wa mambo. Mfano kuwashauri Saudi Arabia wajenge kwanza Akademi za kuzalisha vipaji ni hadaa kwa sababu kila Ligi kuu imekuwa ikihujumu nyingine kwa kunyakua mastaa wao. Ni Sababu hiyo hata Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron akilazimika kuingilia Kati usajili wa Kylian Mbappe ambaye alitaka kuondoka PSG na kwenda Real Madrid. 

Rais Macron alidaiwa kumwambia Mbappe kuwa ndiye nembo ya Ligi Kuu ya Ufaransa hivyo alipaswa kubaki Ligue 1 kuongezea mvuto wa Ligi hiyo. Mbappe alikubali licha ya fedha nyingi alizoahidiwa kusaini mkataba mpya.

Sasa basi tukirudi EPL, mwaka 1992 ilifanyiwa mabadiliko mbalimbali ili kuwa na mvuto Ulaya na duniani. EPL ikaipiku Ligi maarufu wakati ule La Liga(Hispania), Serie A (Italia), Ereviside (Uholanzi) na Ligue 1(Ufaransa). 

Timu za EPL zilivamia soko la usajili kwa nguvu za Pesa na kuwanunua wachezaji mbalimbali duniani. Si wachezaji tu, bali wale wenye vipaji vikubwa na maarufu pamoja na kuajiriwa makocha wa ngazi za juu. 

Timu za EPL zilitumia pesa nyingi na matanuzi yak sokoni yalitikisa katika soka. Lakini Sasa EPL imetishika na ujio wa kasi ya matajiri wa timu za Saudi Pro League. Matajiri wenye pesa za mafuta. Saudi Arabia inafanya kile kilichofanywa na timu za EPL. Miaka 30 iliyopita Ligi ya EPL Ilifanya kama Saudia wanavyofanya, waliwanunua wachezaji wengi bora kwa lengo la kudhoofisha ligi nyingine, na wakafanikiwa sasa wanalia lia nini? 

Waswahili wanasema kila zama na kitabu chake. Sasa Saudi Pro League wanaleta kitabu chao kukuza Ligi yao.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

MALAIKA WA YANGA KULINDA MAKOMBE YA NABI?

Tanzania Sports

Kwanini Ilkay Gündogan amechagua Barcelona?