Ni muda ambao Mbwana Samatta anahitaji watu wa saikolojia haraka iwezekanavyo ili asitoke mchezoni.
Kuhama kwa mchezaji kutoka timu moja kwenda timu nyingine sio kitu cha ajabu sana lakini inatokana na namna unavyotoka ndani ya klabu hiyo.
Kelele nyingi hivi sasa zipo kwa mshambuliaji na nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Mbwana Samatta kuwa anatarajiwa kuondoka ndani ya Aston Villa.
Kuna kila sababu ya kukaa naye na kuongea naye mambo mengi, nafikiri wakala wake anafanya kitu kama hiki ili amjenge kiakili na kimawazo.
Huenda yupo katika wakati mgumu sana juu ya hamu ya kuchezo katika ligi bora kabisa kuwahi kutokea duniani ligi kuu ya England.
Kuachwa katika michezo miwili waliyocheza Aston Villa inawezekana ikawa kikwazo kikubwa.
Kocha wa Aston Villa Dean Smith alisema kuwa hakumjumuisha Samatta katika kikosi kilichocheza ligi dhidi ya Sheffield United F.C kutokana na kiwango duni alichoonesha mazoezini.
Hii pia itaweza kumuathiri na kumpoteza kabisa katika kile anachokifikiria juu ya maisha yake ya soka nchini England.
Wamesajiliwa wachezaji wawili katika nafasi yake akiwemo Traore ambaye aliwahi kucheza Chelsea huku bado Davies ameongezewa mkataba.
Anaweza akaangalia namna ya kupambana lakini kweli anaweza kuishi katika ndoto ? bado linakuwa swali ambalo yeye mwenyewe anaweza kulijibu.
Anaweza kupigania namba kama atabaki ila kwa muziki huu wa kuingiziwa wachezaji wapya katika nafasi yako huku washambuliaji wamefikia wanne ataweza kubaki hapo.
Inawezekana wakamtoa kwa mkopo au kweli wakamuuza, je roho yake iko tayari kupata maamuzi yoyote kutoka kwa uongozi wa Aston Villa.
Ikiwa siku ataambiwa na kocha Dean Smith aondoke klabuni hapo atalipokeaje ? au kama ashaambiwa amelipokeaje.
Baada ya kujua hayo yote basi inatakiwa watu wake wakae naye vizuri na wamueleze kuwa hakuna kingine kitakachompa faraja bali kupata nafasi ya kucheza kila wiki.
Wapi atapata nafasi hiyo, sasa ataangalia wapi ataenda kucheza, je atakubali kutolewa kwa mkopo ligi daraja la kwanza na atakubali kutia miguu huko.
Samatta na jopo lako unaweza kutegua kitendawili hiki kwa kutupa muelekeo wako mapema kama utaenda wapi au utabaki na utaweza kuhimili vishindo.
Tayari Fenerbahçe wameanza kutuma picha zisizo za kweli juu ya usajili wa nyota huyo wakimtaka atue hapo.
Lakini tetesi zinasema kuwa nyota huyo ataenda huko katika nchi ya Uturuki.
Unaweza ukajiuliza maswali mbalimbali huko anapoenda kuna faida kwake au anaedna kwakuwa amekosa chaguo sahihi.
Ni mwambie tu akafanye kazi kama atafanya vizuri zaidi ataweza kurudi nchini humo na akafanya maajabu wengi wasiamini.
Uwezo wa kucheza anao na imani yangu kuwa akienda Uturuki ataweza kurudisha tumaini lake na kufanya mazuri.
Ila kuna sehemu pia anaweza kwenda na akafanya vizuri, huko Ufaransa nako sehemu sahihi kwake ataweza kuwa bora.
Wakala wake wanakazi kubwa ya kuchambua ofa lakini wakati huo kumtafutia namna ya kucheza katika ligi tano bora ikiwemo hiyo ya Ufaransa.
Ni wakati sahihi wa kuchukua chako mapema Samatta sio kupoteza muda , kiwango unacho na umetuonesha namna gani unaweza usie moyo.
Samatta amefunga goli moja katika mechi 14 alizocheza akiwa na Aston Villa.
Hii inatofauti kidogo Simba amecheza michezo 25 amefunga magoli 13.
Wakati alipokuwa TP Mazembe amefunga magoli 60 kwa mechi 103, wakati huo KRC Genk kafunga magoli 43 ktika mechi 101.
Comments
Loading…