in , , , , ,

Bingwa mpya Ulaya, historia mpya

MASHINDANO ya Ligi ya Mabingwa Ulaya yamefika hatua ya Nusu Fainali. Ushindani mkubwa umeoneshwa katika mechi za robo fainali ambapo bingwa mtetezi Real Madrid alikubali kipigo cha jumla ya mabao 5-1. Katika mechi za robo fainali kumeshuhudiwa mtanange wa nguvu na kuwapa burudani mashabiki wake. Real Madrid waliufunga uwanja wao wa Santiago Bernabeu lakini hawakufua dafu wala kuepuka kipigo kutoka kwa Arsenal. Hekaha za wachezaji, makocha na mashabiki walioimba wimbo wa ‘remontada’ wakimaanisha ‘comeback’ hakusikilizwa na Arsenal na badala yake ukawa mwendelezo kipigo. Kuna Inter Milan,halafu kuna PSG na Barcelona ambazo zote zimetinga nusu fainali msumu.

TANZANIASPORTS inatanabaisha kuwa mashindano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu yanakwenda kuandika bingwa mpya katika historia mpya. Michuano ya mwaka huu imekuwa ya aina huku mashabiki wakiwa wamefurahia rekodi zilizowekwa kwenye mashindano.

BINGWA MPYA

Ligi ya Mabingwa Ulaya inatarajiwa kupokea bingwa mpya kwa sababu muundo wa mashindano hayo umebadilishwa kutoka ule uliozoeleka. Katika mashindnao ya msimu huu timu zilishiriki kwa mfumo wa Ligi ambapo Liverpool ilikuwa kinara katika Ligi hiyo. Mfumo wa sasa ulizikutanisha timu ambazo hazikuwahi kukutana wala kuota kama zitaweza kuchuana kwenye Ligi ya Mabingwa. Licha ya kuongoza Ligi hiyo, Liverpool iliambulia kichapo kutoka kwa wakali wa Ligi Kuu Ufaransa, PSG wakiwa chini ya kocha Luis Enrique. Kwahiyo msimu huu bingwa mpya anapatikana kwa mfumo mpya.

MATOKEO YA KUSTAAJABISHA

Bayern Munich waliingia kwenye dimba la Giseppe Meazza wakiwa na matumaini ya kufuzu nusu fainali na kulipiza kisasi baada ya kuchapwa mabao 2-1 kwenye mchezo wa kwanza na Inter Milan. Vijana wa Simeone Inzaghi waliibuka vinara kwenye mchezo wa kwanza baada ya kushinda mabao 2-1 kwenye dimba la Allianz Arena nchini Ujerumani. Vijana wa Vincent Kompany waliingia kwneye dimba la Giuseppe Meazza kwenye mchezo wa marudiano wakiwa na shauku ya kupata ushindi lakini wakajikuta wakilazimishwa sare 2-2. Kwa matokeo hayo Inter Milan ikapasua anga na kuwakilisha wakali wa Ligi ya Italia.

Borrusia Dortmund walikuwa wamepoteza kwa mabao 4-1 katika mchezo wa kwanza dhidi ya Barcelona. Wakiwa kwenye dimba la nyumbani walionesha kiwango bora zaidi kwa kuichapa Barcelona mabao 3-1. Hata hivyo ushindi hawakuwasaidia kuibuka na ushindi kwenda nusu fainali. Barcelona waliibuka na ushindi w ajumla ya mabao 5-4.

Real Madrid bingwa mtetezi aliambulia kipigo kikali cha mabao 2-1 kutoka kwa washika bunduki wa London, Arsena. Kwa ushindi huo Arsenal wamedumisha rekodi yao ya kutofungwa na Real Madrid kwenye mashindano ya Ligi ya Mbaingwa.

NJAA YA MAKOMBE

Timu zote zilizotinga nusu fainali yaani Barcelona, PSG, Arsenal na Inter Milan zina njaa ya kunyakua kombe hilo kwa udi na uvumba. Uwezo wao, nguvu zao, ari na maarifa waliyonayo yanaonesha dhahiri ni timu zilizojiandaa kwa shughuli pevu ya mashindano ya Ligi ya Mabingwa. Njaa ya makombe umekuja kutokana na muda ambao timu hizo zimekaa bila kutwaa taji hilo na ambazo hazijawahi kuchukua kabisa.

BARCELONA 

Tuanze na wakali hao wa Catalanyua. Barcelona wapo chini ya kocha Hansi Fliks.kwa kipindi cha miaka zaidi ya 10 Barcelona hawajatwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya. Makocha wamekuja na kuondoka lakini hakuna aliyewahi kufanikiwa kufikia rekodi ya Pep Guardiola. Hadi sasa Barcelona wameonesha kiu kubw aya kunyakua taji hilo.

ARSENAL

Katika ofisi za Shirikisho la soka barani Ulaya, jina la Arsenal lipo kama mshiriki ambaye amewahi kufika hatua ya fainali ya Ligi ya Mabingwa mara moja na akachapwa na Barcelona ya akina Samuel Eto’o. Arsenal ilikufa kwa kwa mabao 2-1 kwenye mchezo wa fainali ikiwa chini ya Arsene Wenger. Arsenal hajawahi kuchukua taji hilo, na ilipotea kwenye mashindano ya Ulaya kwa muda mrefu na sasa wameanza kunguruma tena na wameonesha shauku ya kunyakua taji hilo kwa mara ya kwanza.

PSG

Tanzania Sports

Kama ilivyo kwa klabu ya Arsenal, vigogo hawa soka wa Ufaransa hawajawahi kunyakua ubingwa UEFA licha ya kuwa na wachezaji mahiri kama vile Ronaldinho Guacho, Jay Jay Okocha, Lionel Messi, Neymar Junior, Thiago Motta, Thiago Silva, Zlatan Ibrahimovich na wengineo wengi. Lakini msimu wakiwa na kocha Luis Enrique wameonesha dhamira ya kutwaa taji hili kwa mara ya kwanza. PSG ndiyo timu iliyomtoa aliyekuwa kinara wa Ligi ya Mbaingwa Ulaya, Liverpool msimu huu ikiwa imejikusanyia pointi nyingi. Kikosi cha Arne Slots licha ya kuibuka na ushindi kwenye mchezo wa kwanza jijini Paris ililazimika kwenda hatua ya matuta baada ya kulambwa 1-0 kwenye dimba lao la Anfield. Lakini ili kufuzu nusu fainali waliitupa nje Aston Villa ya England.

INTER MILAN

Wazee wa mashindano ya Ulaya wamerudi tena ulingoni kwa hasira kali. Inter Milan haijatwaa taji la Ulaya zaidi ya miaka 10 hadi sasa. Safu yao ya ushambuliaji inaongozwa na Lautaro Martinez ambaye ni nahodha wao. Inter Milan inacheza soka la kasi mno na imekuwa miongoni mw atimu tishio kwenye mashindano ya mwaka huu. Kuitupa nje Bayern Munich si jambo jepesi, kama ilivyofanya Arsenal kuwatupa nje Real Madrid. 

USHINDANI WA LIGI TATU

Kwenye mashindano ya mwaka huu, shughuli pevu ilikuwa kwenye Ligi kuuu tatu; EPL, La Liga, na Bundesliga. Italia na PSG wamekuwa peke yao kwneye mashindnao ya Ulaya tofauti na washindani wao. Katika Ligi Kuu ya Ufaransa PSG ilikuwa ikiwakilisha kiupweke sawa na Inter Milan ya Italia. Bundesliga walikuwa na timu mbili katika hatua ya robo fainali, Borussia Dortmund na Bayern Munich. 

La Liga walikuwa na timu mbili katika hatua ya robo fainali; Barcelona na Real Madrid. Wakati EPL walikuwa na timu mbili, Aston villa na Arsenal. Katika hatua ya nusu fainali, La Liga wana timu moja, Barcelona, wakati EPL nao wamebakiza timu moja, Arsenal, huku timu za Bundesliga wakitupwa wote nje.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

Sababu za Amaan Complex kuwakilisha ‘Kwa Mkapa”

Tanzania Sports

Hasira za Man United sokoni