Muda umewadia kwa maelfu ya mashabiki wa soka duniani kushuhudia fainali ya Ligi ya Mabingwa ambayo msimu huu inawakutanisha wababe wa soka wa Italia Inter Milan na mbabe wa soka wa Ufaransa PSG. Ni fainali ambayo imebeba taswira nyingi tofauti kuhusiana na vilabu vyenyewe kwa namna vilivyopambana hadi kufika fainali. TANZANIASPORTS inaangalia masuala muhimu yanayowapa nafasi ya kywaa ubingwa msimu huu.
Goli la mapema
Dakika 15 za kipindi cha kwanza zitakuwa ni zile za kusaka goli la kuongoza. Timu zote mbili yaani Inter Milan na PSG zina tabia ya kusaka goli la mapema ili kujiweka sawa katika mchezo. PSG walifungwa 1-0 na Liverpool wakiwa nyumbani, lakini kwenye mchezo wa marudiano walipachika goli la mapema na kwuachanganya kabisa Liverpool kisha kuwatupa nje ya mashindano kwa njia ya matuta.

Katika mchezo dhidi ya Arsenal, PSG walitumia njia hiyo katika kupachika goli la mapema na kuwachanganya wapinzani wao. Inter Milan waliwashangaza Bayern Munich, wakapachika goli mapema katika ushindi wao wa 2-1 wakiwa ugenini, kabla ya kulazimishwa suluhu wakiwa Giuseppe Meaza nchini Italia. Goli la mapema dhidi ya Barcelona liliwapa nafasi ya kuongoza na kuatwala mchezo kabla ya kumalizika kwa 3-3 wakiwa ugenini. Katika mchezo wa marudiano Inter Milan walifunga goli la mapema katika mchezo uliokuja kumalizika kwa 4-3 kwenye hatua ya nusu fainali. Kwahiyo fainali hii inazikutanisha timu zenye tabia zinazofanana katika dakika 15 za kwanza. Hivyo basi itakuwa shughuli pevu.
Ulinzi silaha ya kwanza
Inter Milan iliruhusu mabao 6 katika mechi mbili za nusu fainali dhidi ya Barcelona. Kikosi cha Simone Inzaghi kilionekana kushindwa kukabiliana na ubunifu walionao Barcelona wakati wanaposaka goli. Pengine wanaweza kujitetea walifungwa mabao hayo kutokana na umahiri wa wapinzani wao, lakini hii ishara mbaya kwa timu inayopigania kuchukua taji la Ulaya. PSG hawana wachezaji wakali kama Barcelona, lakini endapo Inter Milan itashindwa kuweka mkakati wa ulinzi itajikuta inaruhusu mabao mengi kwani Wafaransa hao si haba kwenye kupachika mabao mengi. PSG kwa upande wao wana safu kali ya ulinzi lakini haijawahi kukumbana na mtihani mgumu wa kukabiliana na washambuliaji wenye uchu kama wa Inter Milan. Safu ya ushambuliaji ya Inter Milan inaongozwa na Marcus Thuram na Lautaro Martinez ambao wamekuwa mwiba kuanzia Ligi kuu hadi mashindano ya Ulaya. Kwahiyo PSG wanaingia fainali hii kukabiliana na timu yenye uwezo wa kufunga mabao manne (4) katika mechi moja, kwani walifanya hivyo dhidi ya timu mahiri ya Barcelona.
Inter Milan wanakabiliana na mtihani mwingine, katika safu yao ya ulinzi kuna wachezaji wenye umri mkubwa zaidi, ambao bila shaka wanaweza kukutana na kibarua kigumu cha kuwadhibiti wachezaji chipukizi wa PSG ambao wanasifika kwa kasi. Umri ni miongoni mwa sababu iliyochangia wachezaji chipukizi wa Barcelona kupachika mabao mengi dhidi ya Inter Milan, sababu walinzi wao wana umri miaka 30 na mwingine 38, hali ambayo inatishia uimara wao wa kunyakua taji hili. Anaywez akujilinda katika fainali hii ndiye ataibuka kinara.
Wageni na wenyeji
Ni timu ambayo imetinga fainali hizo kw amara ya kwanza katika historia yake na haijawahi kunyakua taji la UEFA. Pia PSG inawakilisha ugeni wa timu za Ufaransa ambazo hazijachukua taji hilo kwa muda mrefu. Lakini kw aupande wao Inter Milan, ni timu mwenyeji kwenye fainali za UEFA huku ikitoka kukumbuka fainali yao ya mwisho walifungwa 1-0 na Manchester City. Pia taji la mwisho la UEFA walitwaa miaka 15 iliyopita, kwahiyo wanaingia kwneye fainali hizi wkaiw ana usongo wa hali ya juu.
Umahiri wa kocha
Simone Inzaghi anataka kuwa kocha mwneye taji la UEFA. Katika maisha yake ya uchezaji wa soka hayana simulizi nyingi nzuri na za kuvutia. Lakini kwenye kazi ya ukocha simulizi yake inavutia mno na kazi yake imeonesha kuwa kama wasemavyo wataalamu wa masuala ya kiroho, Mungu hakunyimi kila kitu. Simone Inzaghi hakupewa miguu mitamu ya kucheza soka, lakinia amepewa kipaji kikubwa na maarifa makubwa ya kufundisha mchezo huo na kuipa mafanikio klabu ya Inter Milan. Umahiri wa kocha huyu unasifika kila kona ya dunia na kwamba ameifanya Inter Milan kila mchezaji ni beki, kipa, mshambuliaji, kiungo na winga. Kifupi wachezaji wake wapo tayari kuchezeshwa katika nafasi yoyote ili kuipa mafanikio klabu yao. Inter Milan inaongozwa na wachezaji wakongwe na vijana ambao wametengeneza uwiano mzuri kwenye uchezaji wao. Kocha wao amekuwa akiipanga timu yake kulinda lango kwanza, kisha wote kwa pamoja wanatakiwa kwenda kushambulia kwa nguvu. Ni sababu hii mabeki wake wa kati na pembeni wamejikuta wakiwa wamepachika mabao kwenye mazingira ambayo hayakutarajiwa. Pengine mabeki wangefunga mabao kwenye mipira ya faulo ndogo, kona au penati, lakini wamepachika mabao katika mipira ya krosi na pasi za kawaida. Hapo ndipo inapooneshwa kuwa Inzaghi ameifanya Inter Milan kuwa timu ambayo wachezaji wake wanachezesha kila idara na wanakwenda pamoja.
PSG inaundwa na wachezaji chipukizi na wenye uchu wa ushindi. Kocha Luis Enrique ameipata timu yake vyema kwa kuhakikisha viungo wanagusa na kuachia vyema huku wakiwa na uwezo w akufunga mabao wakati wowote. Enrique ameifikisha fainali ya UEFA baada ya kuondokewa na staa wao Kylian Mbappe. PSG wanacheza kana kwamba hawana pengo la staa wao, lakini hata mabeki wao wanaweza kufunga mabao kama washambuliaji wa kawaida. Achraf Hakimi alikuwa nyota wa mchezo kwenye nusu fainali baada ya kupachika bao kwa PSG akiwa katika eneo la mshambuliaji. Kimsingi Hakimi ni beki wa kulia, unaweza kujiuliza alifikaje kwenye eneo la mshambuliaji (namba 9) na kuapchika bao zuri kuliko washambuliaji wake.Hiyo ina maana katika fainali ya msimu huu; kazi ipo.


Comments
Loading…