Michezo yote 10 ya wiki ya tano ya EPL imeshachezwa. Kwenye makala hii mwandishi wetu amechagua kikosi cha wachezaji 11 waliofanya vizuri kwenye michezo ya EPL wiki hii.

 

Golikipa: JACK BUTLAND (Stoke City)

Ingawa aliruhusu mabao mawili kwenye mchezo dhidi ya Arsenal hapo juzi lakini kiwango alichokionyesha kilipunguza idadi ya magoli ambayo timu yake ilikuwa hatarini kuruhusu dhidi ya Arsenal waliopiga mashuti 12 yaliyolenga lango.

 

Mlinzi wa Kulia: RITCHIE DE LAET (Leicester City)

 RITCHIE DE LAET
RITCHIE DE LAET

Mlinzi huyu wa kulia wa Leicester alikuwa sehemu kubwa ya mafanikio ya Leicester kwenye mchezo dhidi ya Aston Villa ambapo timu yake iliibuka na ushindi wa 3-1. Alipandisha mashambulizi ya kutosha upande wa kulia na alilinda vizuri.

advertisement
Advertisement

 

Mlinzi wa Kati: JOHN STONES (Everton)

 

Chelsea walipiga mashuti mawili tu yaliyolenga goli kwenye mchezo dhidi ya Everton hapo juzi.OHN STONES

JOHN STONES
JOHN STONES

kuyazima mashambulizi ya Chelsea na huenda ameongeza uwezekano wa kuendelea kufuatiliwa na Jose Mourinho.

 

Mlinzi wa Kati: DALEY BLIND (Manchester United)

Aliifungia bao la kuongoza Manchester United kwa utulivu wa hali ya juu. Hata hivyo hicho sicho kinachomuweka kwenye kikosi hiki. Kinachomuweka hapa ni namna alivyoweza kumtuliza Benteke ingawa alifunga bao baadae.

 

Mlinzi wa Kushoto: BRENDAN GALLOWAY (Everton)

Mlinzi huyu wa pembeni alikuwa mwiba upande wa kushoto hasa kwenye mashambulizi. Krosi nzuri aliyompigia Steven Naismith ilizaa bao la kwanza na pia alifanikiwa kumuweka Costa chini ya ulinzi kwenye mipira ya adhabu na kona.

 

Kiungo wa Kati: FRANCIS COQUELIN (Arsenal)

FRANCIS COQUELIN
FRANCIS COQUELIN

Aliitendea vyema nafasi ya kiungo mkabaji kwa kuzuia mashambulizi ya Stoke City na kuanzisha mashambulizi ya Arsenal. Ingawa Carzola aling’aa zaidi yake kwenye upande wa mashambulizi lakini Coquelin alisimama kama injini ya timu.

 

Kiungo wa Kati: WES HOOLAHAN (Norwich)

Ubunifu wa ziada aliokuwa nao kwenye mchezo dhidi ya Bournemouth ulimuwezesha kutoa pasi nzuri ya bao na kufunga jingine kwa ustadi. Nafikiri kila aliyetazama mchezo ule lazima amtaje Hoolahan kuwa nyota wa mchezo.

 

Kiungo wa Kulia: RYAD MAHREZ (Leicester City)

RYAD MAHREZ
RYAD MAHREZ

Pasi mbili za magoli alizotoa kwenye mchezo dhidi ya Aston Villa hapo juzi zilitosha kabisa kumuwezesha kuwepo kwenye kikosi hiki. Hata hivyo takwimu hizi pekee hazitoshi kuelezea kiwango cha kustaajabisha alichokionyesha.

 

Kiungo wa Kushoto: DIMITR PAYET (West Ham)

Aliwasumbua mno walinzi wa Newcastle kwa takribani dakika zote za mchezo. Akafunga goli la mbali katika kipindi cha kwanza kabla ya kuongeza la pili kwenye kipindi cha pili na kujiweka kwenye nafasi ya nyota wa mchezo huo.

 

Kiungo Mshambuliaji: STEVEN NAISMITH (Everton)

STEVEN NAISMITH
STEVEN NAISMITH

Huyu ni nyota wa wiki EPL. Magoli matatu aliyowafunga Chelsea yalitokana na uwezo wake na morali aliyokuwa nayo kwenye mchezo huo baada ya kuingia kuchukua nafasi ya Muhamed Besic kwenye dakika za mapema.

 

Mshambuliaji: ODION IGHALO (Watford)

Mshambuliaji huyu wa timu ya taifa ya Nigeria alijaribu kujiweka kwenye sehemu nzuri za kupokea mipira ndani ya eneo la hatari la wapinzani.  Juhudi zake zilitosha kumpatia bao lililoipatia alama tatu timu yake dhidi ya Swansea City.

 

Report

Written by Kassim

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

KASHFA YA MLUNGULA FIFA:

Tanzania Sports

MATOKEO LIGI YA MABINGWA ULAYA