“born town vs bush stars”
Mzee Amri bawji sio jina maarufu kwa watanzania wengi wa kawaida ila kazi zake zimegusa hisia za watanzania wengi kwa kipindi kirefu. Mzee huyu alikuwa ni gwiji wa fasihi nchini Tanzania hususani kwenye kipengele cha riwaya na pia alikuwa mzalishaji wa filamu nchini Tanzania. mzee huyu alikuwa ni mwenyeji wa tanga na alifariki mnamo februari 21 mwaka huu katika hospitali ya maarufu ya Bombo iliyoko katika mji wa Tanga. Kiukweli huyu mzee alikuwa ni mjasiriamali ambaye alijua kutumia kipaji chake kutengeneza ajira kwa watu wengi katika nyakati zake. Angekuwa yuko ughaibuni basi leo hii angekuwa anatajwa daraja moja na watu kama akina Walt Disnep muasisi wa eneo maarufu la starehe linalofahamika kama DISNEYLAND.
Mwaka 1973 yeye pamoja na ndugu yake aitwaye Saady Bawji waliasisi jarida la SANI. Waliliasisi huku wakishirikiana na kijana mwenzao Nico Ye Mbajo. Jarida hili lilidumu mpaka mnamo mwaka 2013 ambapo jarida hili lilikufa kwa mujibu wa vyanzo vya taarifa ambavyo nimevipitia. Kuasisi kwao huku kwa jarida hili natumai ndiko kutawafanya wakumbukwe Zaidi na wadau wa burudani hususani wale ambao walikuwepo katika nyakati hizo. Jarida lao lilikuwa maarufu sana na lilisomwa maeneo mbalimbali ya nchi. Katika nyakati hizo ambazo mimi nilikuwa mdogo nakiri wazi kwamba nilikuwa mfuatiliaji mzuri wa majarida hayo na visa vingi navikumbuka mpaka hivi leo.
Mojawapo ya wahusika ambao waliutumia ufundi wa kifasihi kuwachora ni pamoja na Mzee sani(Babu sani), sokomoko, Pimbi, Prof ndumilakuwili, lodi lofa, mzee meko, Madenge, baba madenge, mama madenge, komredi kipepe,, bob mazishi, zena, betina, mwinyi mpeku, mzee kifimbo cheza, bob mazishi na wengineo. Wahusika hawa walikuwa maarufu sana na nakumbuka nyakati nilipokuwa mdogo tulikuwa tuki shuleni tunataniana kwa kupeana majina yanayotokana na wahusika waliopatikana kutoka katika jarida hilo.
Visa ambavyo vilikuwa vinapatikana katika jarida la SANI vilikuwa ni visa ambavyo vilikuwa vinagusa maisha ya watanzania wa kawaida katika nyakati hizo na hali hiyo ilipelekea jarida hilo kupendwa sana. Jarida hilo kwa nyakati hizo nlikuwa najitahidi kwa kila hali lisinikose hata toleo moja kwani kuna nilikuwa naburudika sana kusoma matoleo ya majarida hayo
Kwa hakika mzee wetu huyu kwa nyakati hizo alikuwa “ahead of the time” kama wasemavyo wazungu kwani aliweza kutumia kipawa chake kuweza kutengeneza matukio ya kisanaa ambayo yalikuwa yanaakisi hali ama fursa ambazo zitakazokuja kutokea siku za usoni. Alitumia wahusika wa zena na betiba kujaribu kuwaamsha wakina dada waanze kuangalia fursa katika michezo kwa kuonyesha kwamba kuna fursa katika mchezo wa ndondi kwa wanawake. Nyakati hizo anawachora wahusika hao huku Tanzania hakukuwa na wapiganaji magwiji wa kike kwa hiyo alikuwa anatumia njia ya kifasihi kuwahamasisha. Huko ughaibuni kulikuwa na wapiganaji kama akina Leila Ali ambaye alikuwa ni binti wa gwiji wa masumbwi duniani hayati Muhammad Ali.
Alitumia katuni maarufu kwa wakati huo za “born town vs bush stars” kujaribu kuonyesha mpambano wa mechi ambazo zilikuwa zinachezwa kati ya timu mbili ambazo zilikuwa hasimun timu moja ambayo ilikuwa ni timu ya watu wa kijiji na timu nyingine ni ya watu wa mjini. Katika mpambano huo mara kadhaa timu ya kijijini ndio ilikuwa inaibuka mshindi.
Katika katuni ambayo nilkuwa siisahau katika simulizi za “born town vs bush stars” ni kisa cha mapungo ambaye alikuwa ni mchezaji wa bush stars na chepe ambaye alikuwa ni mchezaji wa born town kwenda kucheza ulaya. Katika katuni hizo mapungo alisajiliwa na kikosi cha real Madrid katika zama za Galacticos na chepe kwenda kucheza timu ya Barcelona. Wachezaji hao walifanikiwa huko uhispania na kupata mikataba na viwango vyao viliwasaidia kupata namba za kudumu kwenye vikosi hivyo ila baadaye walikuja kuvurunda kutokana na tabia zao za nje ya uwanja.
Leo hii dalili zipo wazi za ndoto za mzee bwaji kufanikiwa licha ya kwamba hartuna wachezaji ambao wanacheza timu ya Real Madrid na Barcelona ila tuna wachezaji wa kitanzania ambao wanacheza ulaya. Nakumbuka aliyewahi kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa Tanzania aliwahi kushangaa kwa nini mchezaji wa yanga Salum Fei Toto kwa nini hachezei Barcelona. Aliposema kauli ile alishutumiwa sana ila kwa waliomuelewa vizuri mzee Bawji walijua hilo jambo liko njiani kwa mtanzania kuchezea Barcelona.
Comments
Loading…