in , , , ,

Iwe kwaheri Carlo Ancelotti

Uwezekano  wa kocha wa Real Madrid Carlo Ancelotti kuongoza timu hiyo msimu ujao ni mdogo. Zipo sababu kadhaa amabzo zitamfukuzisha kocha huyo kutokana na namna uamuzi wake kwenye kikosi ulivyoathiri matokeo katika Ligi Kuu Hispania pamoja na Ligi ya Mabingwa. Sababu ya kuondoka kwa kocha huyo itakuwa ni kuachana naye na kupisha mawazo mapya hata kama atafanikiwa kutwaa taji lolote kati ya matatu anayoyawinda msimu huu. Real Madrid itakutana na Barcelona kwenye mchezo wa fainali ya Copa De Rey kisha ipo kwenye mbio za kuwania taji la La Liga dhidi ya wapinzani wao hao hao, pamoja na Atletico Madrid. Barcelona wanaongoza Ligi hiyo wakiwa na pointi 67 huku Real Madrid wakiwa na pointi 63. Katika mfululizo wa La Liga ni wazi vita vya ubingwa vipo kwa makocha watatu, Hans Flikcs wa Barcelona, Carlo Anelotti wa Real Madrid na Diego Simeone wa tletico Madrid. Je nini hasa kinaongeza joto la kuondolewa kocha huyo?

Mechi dhidi ya Valencia

Valencia ni miongoni mwa vigogo wa soka Hispania. Hii ni timu ngumu kukabiliana nayo hata kama inakuwa na msimu mbaya lakini mbele ya Real Madrid inakuwa timu isiyotabirika. Katika mchezo wa La Liga dhidi ya Valencia kulikuwa na kila sababu ya kuibuka na ushindi. Lakini kwa vile kocha Ancelotti alikuwa anafikiria mechi ya robo fainali dhidi ya Arsenal akafanya mabadiliko ya mapema katika dakika ya 75 ili kuwapumzisha baadhi ya nyota wake. 

Katika hizo hizo Hugo Durro akaipa bao la ushindi Valencia na kumalizika ukame wa zaidi ya mieizi 350 kushindwa kupata ushindi ugenini. Kwa namna timu ilivyocheza na mbinu za kocha zilionesha wazi uamuzi aliochukua uliathiri timu katika dakika 15 za mwisho wa mchezo huo. Ni kwamba ulikuwa uamuzi ambao umewaweka katika shinikizo kubwa kwani Valencia walicheza kwa kasi na kwa uhuru kwa sababu wachezaji muhimu na tishio wa Real Madrid walikuwa wametolewa. 

Kwa mazingira hayo Valencia walibadilika ghafla na kuutaka zaidi mchezo hivyo kusababisha ubao wa matokeo kusomeka 2-1. Kufungwa katika dimba la nyumbani kuliwashtua wapenzi wa timu hiyo na hivyo wakaelekea kwenye mechi ya Ligi ya Mbaingwa wakiwa majeruhi kwenye La Liga.

Arsenal wakatia chumvi kwenye kindonda

Wakati Real Madrid ikiingia uwanjani ilionekana kama vile watakuwa na mechi rahisi kwani wanahofiwa zaidi. Kudhihirisha hilo dakika 45 za kipindi cha kwanza zilimalizika huku timu zikitoka suluhu na kwamba Arsenal walikuwa wakicheza kwa woga wa aina fulani. Hata hivyo kila kitu kilibadilika katika kipindi cha pili kuanzia dakika ya 58 baada ya mpira wa adhabu ndogo wa kiungo Declan Rice kutinga wavuni katika mazingira yasiyotarajiwa.  

Bao hilo liliwashtua Real Madrid, huku eneo lao la kiungo kizidi kuyumba. Umahiri wa Real Madrid kwenye kipindi cha pili ulitoweka ghafla. Ikawa Real Madrid tofauti na ile ya kipindi cha kwanza ambayo ilipoteza nafasi nyingi za kufunga. Bao la pili kwa njia ileile liliwangusha Real Madrid na kabla hawajatulia wakapigwa bao la tatu. Acelotti alilipia gharama ya kupanga mchezaji ambaye hakuwa imara kwenye eneo la beki wa kushoto, David Alaba. Msimu huu David Alaba anabailiwa na majeraha ya mara kwa mara, huku Fran Garcia akiwa mchezaji anayetoa ushindani kwa Ferland Mendy. Fran Garcia ndiye beki wa kushoto ambaye anaonekana kuziba vyema eneo hilo, na hata alipoingia kuchukua nafasi ya Alaba ulikuwa uamuzi uliocheleweshwa na kocha mwenyewe. 

Katika msingi huo, eneo la kiungo wa pembeni kushoto lilikosa msisimko kwa sababu Alaba si mzuri katika kushambulia tofauti na nyakati za ujana wake. mabadiliko hayo pia hayakuwasaidia Madrid wkani Arsenal walikuwa kwneye kiwango bora na walifanikiwa kuidhibiti kila idara. Kama si umahiri wa Thibaus Cortoius huenda mabao mengi yangetinga kwenye lango la Real Madrid. Endapo Carlo Ancelotti atapoteza pambano dhidi ya Arsenal ni dhahiri sababu za kuondoka kwake zitaongezeka.

Uvumi usiokoma

Xabi Alonso ni jina la kocha anayehusishwa kwa muda mrefu kwenda kuinoa Real Madrid. Kwa sasa Alonso ni kocha wa Bayer Leverkusen akiwa ametoka kuipa ubingwa msimu uliopita. Jina la Alonso limekuwa likitajwa tangu msimu uliopita hivyo ni miaka miwili sasa kocha huyo amekuwa akitajwa kuchukua jukumu la kuwa kocha mkuu wa Real Madrid. Santiago Solari ni balozi wa Real Madrid katika shughuli za michezo, amekuwa akitajwa kama mmoja wa makocha wanaoweza kuchukua nafasi ya Ancelotti wakati wowote. 

Solari amewahi kuwa kocha wa muda klabuni hapo akichukua nafasi ya Julen Lopetegui ambaye aliondolewa kutokana na matokeo mabay. Hata hivyo Sntiago Solari naye hakudumu baada ya kuondolewa kwenye Ligi ya Mabingwa na Ajax Amsterdam. Zinedine Zidane ni jina lingine la kocha anayetarajiwa kurejea endapo Ancelotti ataondolewa. Zidane amewahi kuwa kocha wa klabu hiyo kwa awamu mbili; awamu ya kwanza alitwaa taji la Ligi ya Mabingwa mara tatu mfululizo na baadaye aliporejea hakufua dafu lakini timu yake ilibadilika vyema.

Kwenda Brazil

Kwa muda mrefu Carlo Ancelotti amekuwa akiwindwa na timu ya Taifa ya Brazil. Uongozi wa Brazil unatamani kumfanya Ancelotti kuwa kocha wa kwanza wa kigeni kukiongoza kikosi chao kwenye fainali za Kombe la Dunia. Uwezekano wa Ancelotti kwenda Brazil ni mkubwa mara baada ya kumalizika msimu huu, kwa sababu shuku ya kumwajiri imeongezekana. Doriva Junior ameondolewa kwenye kazi ya ukocha wa timu ya taifa ya Brazil hivyo nafasi hiyo ipo wazi na inahitaji kocha mpya. 

Kocha anayewindwa zaidi ni Carlo Ancelotti. Sababu hii inaweza kumfukuzisha Real Madrid kwani itakuwa ahueni kwao kupunguza kelele za Brazil kumtaka mwalimu huyo na hivyo kuleta kocha mpya wa kuwapa mawazo mapya. Real Madrid inaweza kutumia mwanya huo kumruhusu kuondoka iwe mapema ama baada ya fainali za Klabu Bingwa dunia zitakazofanyika mwezi Juni mwaka huu.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

30 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

Ange Postecoglou safari imewadia?

Mkurugenzi mkuu wa bodi ya utalii Tanzania, Ephraim Mafuru, akimkaribisha mmiliki wa timu ya Manchester United, Sir Jim Ratcliffe, Jijini Dar es Salaam, hivi karibuni.

Afrika ni soko jipya kubwa la michezo duniani