in , , ,

Harry Kane amebeba mizigo ya England

Wachezaji wengi wa England hawajafanikiwa kutikisa Ligi za nje ya EPL…

UAMUZI wa kuhamia Bundesliga umechangiwa na mambo mengi, ikiwemo sababu za kimpira, kiuchumi na changamoto mpya. Harry Kane anakuwa mshambuliaji nambari moja katika klabu ya Bayern Munich, lakini amebeba mzigo mzito sana wa wachezaji wa England. Kane ameondoka Tottenham Hotspurs mahali ambako Wajerumani wamewahi kuwapa kipaji cha Christian Ziege. 

Huyu Ziege na Umit Davala wa Uturuki walikuwa maarufu kwa kunyoa nywele mtindo wa Kiduku. Umahiri wa Christian Ziege unakumbukwa sawa na Umit Davala. Hata hivyo Ziege hakuwa mfalme wa Hotspurs kama ilivyokuwa kwa Harry Kane. 

Mshambuliaji huyo na nahodha wa England amejiunga na mabingwa wa Bundesliga msimu uliopita Bayern Munich huku akiacha gumzo kubwa juu ya uamuzi wake. Mshambuliaji wa zamani wa Liverpool, Real Madrid na Manchester United, Michael Owen alieleza kuwa uamuzi wa Harry Kane haukuwa ukieleweka kwa sababu Bayern Munich haikuwa timu ya kuhamia kwani ndiyo kinara wa Bundesliga na hakuna uwezekano wa Ligi hiyo kutawaliwa na timu zingine ni mgumu. Owen anaamini Bundesliga ni ya timu moja hivyo halijawa chaguo sahihi kwa nyota huyo wa England. 

Tanzania Sports
VALLETTA, MALTA – JUNE 16: Harry Kane of England looks on prior to the UEFA EURO 2024 qualifying round group C match between Malta and England at Ta’ Qali Stadium on June 16, 2023 in Valletta, Malta. (Photo by Mike Hewitt/Getty Images)

Kwa maoni ya Owen ni afadhali Harry Kane angejiunga na Real Madrid ambako wanaweza kupata changamoto toka kwa Barcelona na kukosa ubingwa. Kwahiyo Bayern Munich kuna uhakika wa kutwaa taji la Bundesliga na hakuna changamoto. Kwa upande wake Alain Shearer ambaye ndiye mfungaji mwenye mabao mengi EPL katika historia imekuwa shangwe kwake kwani rekodi zake hazitavunjwa. Yeye hajali mahali alikokwenda Harry Kane bali kuondolewa mshambuliaji aliyetishia kuvunja rekodi zake za upachikaji wa mabao EPL. 

Hata hivyo Harry Kane kama walivyo wachezaji wengi wa England anakabiliwa na mzigo mzito kuonesha umahiri wa vipaji vya watoto wa Malkia. Historia ya England ni wachezaji wachache sana wameng’ara nje ya EPL. Kane ametua katika klabu ambayo ilimwinua Owen Hargreaves kabla ya kuhamia Manchester United. 

Hargreaves alikuwa mmoja wachezaji wenye vipaji na watulivu dimbani alipokuwa Bayern Munich. Alicheza kiungo cha kati na winga wa kulia kadiri kocha alivyoamua. Pengine ndiye mchezaji ambaye alionesha umahiri zaidi katika kikosi cha Bayern Munich akiwa mzaliwa wa England. Hali kadhalika wapo wengine ambao walicheza Serie A, kama vile Paul Gaza na hivi sasa ,. 

Wachezaji wengi wa England hawajafanikiwa kutikisa Ligi za nje ya EPL. Ukienda Lque 1 kule Ufaransa utakutana na majina ya wachezaji kutoka mataifa ya Afrika masharibi, Amerika kusini, na mengine ya Ulaya, lakini nyota wa England hawajafua dafu. Vilevile La Liga, David Beckham alikuwa nyota wa Real Madrid, lakini hakuwa mchezaji aliyetikisa ndani ya dimba, labda nje ya uwanja katika mauzo ya jezi. Steve McManaman huenda ndiye mchezaji mwenye mafanikio nje ya EPL kwani alitwaa Uefa akiwa Real Madrid pamoja na mataji mengine. 

Beki wa kati Jonathan Woodgate ambaye alitoka Hotspurs kwenda Real Madrid hakuwa na lolote la kujivunia, ni sababu moja tu inawea kutumika kama kisingizio yaani majeraha yalimwandama. Kwa upande mwingine kila kona ya Ligi Kubwa za Ulaya, wachezaji wazaliwa wa  England hajachachafya. Wengi wao wanacheza Ligi ya nyumbani kwao EPL. Michael Owen naye aliwahi kucheza real Madrid kwa msimu mmoja kabla ya kuuzwa kwenda Newcastle United. Naye hakung’ara La Liga kama ilivyokuwa EPL.

Kwa upande mwingine utaona kuwa Harry Kane kama nahodha wa England amebeba mzigo mkubwa wa kueneza vipaji vya England. Vilevile katika umri wa miaka 30 ni wazi hana cha kuthibitisha katika soka, na hivyo anataka kupata motisha ya kazi yake ya kutandaza kandanda. Uhakika wa kunyakua taji la EPL umekuwa mgumu kupitia Tottenham Hotspurs, kwahiyo njia pekee ilikuwa kukubaliana na ofay a Bayern Munich pamoja na marupurupu atakayolipwa. Wachezaji wa EPL wanamtazama nahodha wao kama mchezaji mwenye mafanikio. 

Manahodha wenzake wamewahi kufurukuta na kunyakua mataji hali iliyowapa uhuru wakiwa kikosi cha timu ya Taifa. Hivi sasa Harry Kane anataka kuongeza taji kwenye historia ya maisha yake. Kubaki England kusingempa kombe lolote kwa vile Spurs haionekani kuwa timu inayopigania ubingwa. Kufika hapo utaona kabisa uamuzi wa Harry Kane pia umeambatana na mzigo wa kutangaza vipaji vya wachezaji wa England nje ya Ligi yao. Bila shaka matumaini ya kutetea ubingwa msimu huu ni makubwa lakini changamoto zingalipo. 

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

Kwanini Liverpool wamemsajili Wataru Endo?

Tanzania Sports

Simba wanamaanisha kwa mbili hizi au bado?