in , ,

NILICHOKIONA KWENYE MECHI ZA UEFA.


JUVENTUS vs BARCELONA

Kuna vingi ambavyo viliibeba Juventus na kuonekana ndiyo timu
iliyostahili ushindi wa goli 3-0 katika uwanja wao wa nyuma.

Silaha yao kubwa ilikuwa mbinu bora za mwalimu Massimiliano Allegri,
alihakikisha kila timu yake ilipokuwa inapata mpira ilikuwa
inashambulia kwa nguvu. Mbinu yake ya kuhakikisha Juventus wanamiliki
mpira kwa nidhamu kipindi walipokuwa wanakuwa na mpira na kukaba
vizuri kipindi walipokuwa hawana mpira ilikuwa silaha nzuri kwao.

Kwa Barcelona kutumia mfumo wa 4-3-3 kulikuwa hakuna tatizo, tatizo
lilikuja kwa aina ya baadhi ya wachezaji waliokuwa wanatumika katika
mchezo huo. Mfano kumwanzisha Mascherano katika eneo la kiungo wa
ulinzi lilikuwa na hasara kubwa sana kwa sababu hakutosha kuziba vyema
pengo la Sergio. Mascherano ni mzuri katika jukumu la ulinzi hivo hii
iliwapa kazi sana Barcelona kwenda mbele kwa sababu hakukuwepo na mtu
wa kuisukuma timu kwenda mbele na Mascherano hakuwa na uwezo mkubwa wa
kuditacte tempo ya mchezo.

Mathiew alikuwa beki ambaye alipata kazi kubwa sana na hakuwa imara
vya kutosha kumzuia Juan Cuadrado.

Paolo Dyabala alionekana ni mkubwa mbele ya babu zake ambao alikuwa
nao uwanjani. Tulitegemea Messi ndiye atakuwa mfalme wa mechi hii
lakini, Dyabal akageuza mategemeo yetu.

Kuna wakati waweza ukatamani asistafu na aendelea kuwepo golini na
mkongonjo wake. Buffon hakupi nafasi ya kutabiri ni lini atastaafu ,
kila muda anaendelea kuwa bora zaidi.

Pengine Higuain hakufunga lakini mmoja ya wachezaji ambao walitimiza
majukumu yao kwa kiwango ƙkikubwa ni Higuain . Alifanikiwa kwa kiasi
kikubwa kuwakimbiza na kuwachosha mabeki wa Barcelona.

BORRUSIA DORTMUND vs MONACO.

Tukio la mlipuko wa bomu siku ya juzi ambalo lilisababisha tukio la
mchezaji wa Borrussia Dortmund, Marc Bartra kujeruhiwa ni matukio
ambayo yaliwaweka Dortmund katika mazingira mabaya ya mchezo wa jana.
Kiakili hawakuwa vizuri, ilikuwa ngumu kwao kusahau tukio la mlipuko
wa bomu na kibaya zaidi mchezaji wao mmoja alikuwa amejeruhiwa kwenye
tukio hilo. Hayakuwa mazingira mazuri kuelekea mchezo huo.

Mara ya mwisho kwa Dortmund kuanza na mabeki watatu ilikuwa miezi
miwili iliyopita. Ilikuwa karata mbaya kwa kocha wao kuanzisha mfumo
huo kwao kwani ulionekana mgeni kwao ingawa haikuwa mara ya kwanza
kwao kuutumia. Kitu hiki kilisababisha beki yao kuwa mbovu na
ikashindwa kuhimili mashambulizi ya Monaco.

Kitu ambacho Monaco wanavutia ni kwamba , kikosi chao kinawachezaji
wengi ambao ni vijana wenye umri mdogo lakini wanavyopigana ni tofauti
na umri wao na hawaonekani kuogopa kitu chochote wakiwa uwanjani ,
njaa ya mafanikio iliyo katika mishipa yao ya damu ndicho kitu ambacho
kiliwafanya wapate ushindi ƴugenini.

Kasi ya Mbappe inamsaada mkubwa kwake na timu yake. Kasi hii
inamsababisha yeye kuwa na uwezo wa kufunga. Umri wake bado ni mdogo
na ana muda mrefu kwake kujifunza vitu vingi ili awe bora. Ukiachana
na Mbappe, jana Thomas Lamar na Bernado Silva walicheza vizuri pia.

BAYERN MUNICH vs REAL MADRID

Neur ni mhimili mkubwa sana wa Bayern Munich, jana alifanikiwa
kupunguza idadi kubwa ya magoli ambayo yalionekana ya wazi sana.
Kipindi cha kwanza kilikuwa cha FC Bayern Munich.

Goli la Vidal lilituaminisha kuwa kuna kitu kikubwa Bayern Munich
wanaweza kukifanya dhidi ya Real Madrid . Lakini kuna vitu ambavyo
vilirudisha nyuma mapambano ya Fc Bayern Munich na kuwapa nguvu mpya
ya kupigana Real Madrid.

Kukosa Penalti kuliwarudisha nyuma Bayern Munich na kitu ambacho
kilikuja kumaliza kabisaa nguvu ya kupambana ni kaɗi nyekundu ya
Martinez.

Kaɗi hii nyekundu ilisababisha pengo kubwa sana katika eneo la kiungo
wa ukabaji na kuwanya Real Madrid kupata nguvu.

Ronaldo alionesha umuhimu wake sehemu ambayo alihitajika sana. Kitu
kizuri kuhusu Real Madrid ni kwamba walikuwa na Ronaldo halafu Bayern
walikuwa hawana Lewandosky.

Benzema ni muda wake kumwachia Morata nafasi.

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

ASANTE TFF NA MARCH, APRIL IBEBE MAY

Serengeti boys

KUNA SIKU MOJA TU YA MBALAMWEZI, NYOTA NA JUA KUNG’AA KWA PAMOJA