in , , , ,

Hesabu na vita ya Yanga zitatimia?

TIMU mbili Yanga na MC Alger ya Algeria zote zinatupia jicho nafasi moja, hili ni sawa na waombaji wa ajira laki mbili wanaogambania nafasi elfu kumi na nne nchini Tanzania. Nafasi ni finyu lakini lazima ipatikane na Yanga wana kila sababu ya kupiga hesabu zao vizuri. Ushindi wa 1-0 waliopata Yanga wakiwa ugenini dhidi ya wenyeji wao Al Hilal umeibuia matumaini ya kufuzu hatua ya robo fainali. Bao la kiungo mshambuliaji Stephani Aziz Ki liliwapa ari kubwa Yanga ambao walikuwa wakiusaka ushindi kwa udi na uvumba huku wkaiwa na uchungu wa kufungwa katika mchezo wa kwanza mabao 2-0 kwenye dimba la Benjamin Mkapa. Yanga wanaanza safari ya kuwinda robo fainali watakapokuwa wenyeji kwenye mchezo wa mwisho dhidi ya MC Alger ya Algeria kwenye dimba la Benjamin Mkapa.

Je ni ipi nafais ya MC Alger?

Wageni wajao wa Yanga wanashikilia nafasi ya pili wakiwa na pointi 8. Nafasi ya kwanza inashikiliwa na Al Hilal ambayo kimahesabu imefuzu robo fainali baada ya kuvuna pointi 10. MC Alger wao wanahitaji sare ya aina yoyote ili waweze kufuzu robo fainali kwani watakuwa na pointi 9 moja zaidi ya washindani wao Yanga ambao watafikisha pointi 8. Kwa vyovyote vile MC Alger wanatakiwa kutofungwa kwneye mchezo huo wa marudiano jambo ambalo linaonekana kuwa gumu.

Yanga wanapita kwa njia gani?

Hakuna namna ambayo Yanga watafanya zaidi ya kuibuka na ushindi. Ni ushindi pekee ndiyo utawapa nafasi ya kufuzu orbo fainali. Haitajalisha ushindi wa idadi ngapi ya mabao lakini alama tatu zitawawezesha kufikisha 10 mbili zaidi ya MC Alger. Njia ya kwanza ni kuhamkikisha wanaifunga MC Alger kuanzia nje ya uwanja na ndani ya kiwanja, kiufundi, maarifa, kasi na ubora ndivyo vitu vitakavyoivusha timu hiyo. Katika mchezo wa kwanza Yanga walifungwa na MC Alger hivyo watakuwa na kazi mbili; kulipiza kisasi cha kufungwa na kutafuta pointi tatu muhimu za kwenda robo fainali. 

Vita kali

Kucheza na timu za Waarabu inajulikana kila mchezo ni vita kali sana. mchezo huu unatarajiwa kutawaliwa na kila aina ya vita, kuanzia vita vyua makocha, vita vya wachezaji, vita vya mashabiki na kila aina ya uhasama. Huu ndiyo mchezo ambao Yanga wanaweza kuita ni fainali yao kwenye Ligi ya Mabingwa. 

Kama walicheza vizuri dhidi ya Mamelodi Sundowns msimu uliopita kwa vita vikali vilivyoshuhudiwa na kufanya mchezo wao kuwa maarufu zaidi kusini mwa jangwa la sahara. Katika mchezo huu MC Alger watakuwa na mbinu zao zilezile za kujihami kwa kiasi kikubwa kwa sababu watakuwa na jukumu la kulinda alama yao moja isipokwe. 

Wao alama moja tu itawapeleka robo fainali kwahiyo watakuwa katika vita vikali ambavyo vitaweza kuwachanganya Yanga. Kwa utamaduni watimu za Kiarabu, kupoteza muda, kumtia shinikizo refa, kutafuta faulo. Kuwasababishia adhabu ya kazi njano au nyekundu. Kifupi utakuwa mchezo wenyekila aina ya vituko, hamasa na presha kubwa kwa wachezaji na benchi la ufundi pamoja na viongozi wao. 

Zawadi kwa mashabiki

Hakuna ubishi yale majivuno ya Yanga yalipungua tangu kuondoka kwa Miguel Gamondi. Mashabiki wa Yanga hawakumjua Sead Ramovic na hawakuelewa watafikishwa wapi kisoka, na zaidi hawakujua uwezo wake katika kusimamia timu. Akiwa amepoteza michezo ya awali, mchezo huu una maana kubwa kwake katika kujenga imani kwa mashabiki. 

Ni mchezo ambao unahitajika zaidi ili kuwapa zawadi mashabiki. Yanga wakishinda itakuwa zawadi kubwa sana kwa mashabiki wao na kurudishia imani na kujiamini tena kwa jinsi timu yao inavyoweza kushughulikia furaha zao na kuwarudishia. Viongozi wa Yanga nao wanatakiwa kuelewa mchezo huo utakuwa zawadi kwa mashabiki na kuthibitisha uamuzi wao wa kubadilisha kocha katikati ya mashindano.

Presha ya watani

Hakuna kitu kizuri kwa timu za Yanga na Simba kama kushindana na kufanya vizuri kimataifa. Simba wametangulia robo fainali kwenye mashindano ya Kombe la Shirikisho baada ya kutoka suluhu na Bravos ya Angola. Sasa kwa hali ya ushabiki lazima watani wataniane. Simba watakuwa na kila sababu ya kuwacheka wenzao Yanga. Hali kadhalika Yanga watakuwa na kila sababu ya kuwadhihirishia Simba kuwa wao wapo Ligi ya Mabingwa na wanaweza kupindua meza vizuri. Presha ya watani itawapa motisha Yanga ili wadhihirishe ubora wao kimataifa. Kufika hapo, ndipo vita ilipo.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

10 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

CAF na shangwe za Watanzania kama Wabrazil