in , , ,

Yanga wametolewa na kocha wao Sead Ramovic

Umewahi kwenda kwenye msiba wowote kisha ukawatazama wafiwa? Bila shaka unatambua huzuni wanazokuwa nazo. Mashabiki wa Yanga na wachezaji wao  ndiyo wanafaa kutupiwa jicho na kuonekana jinsi walivyo na msiba mzito baada ya kushindwa kutinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Wakicheza katika dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar Es salaam, Yanga walikuwa na kibarua kigumu cha kupata ushindi na alama tatu muhimu ambazo zingewapeleka katika hatua hiyo. Ushindi wao wa bao 1-0 ugenini siku chache zilizopita ulifufua matumaini yao kutinga robo fainali katika mchezo wa mwisho dhidi ya MC Alger. Hata hivyo wageni hao walitumia kila aina ya mbinu nzuri na chafu kuhakikisha Yanga hawapati bao lolote. Fuatana nami katika uchambuzi huu.

Mipango bila nyenzo

Yanga waliingia kwenye kiwanja wakiwa na washambuliaji watatu; Clement Mzize, Kennedy Musonda na Prince Dube. Wachezaji hawa wote wanaweza kucheza katika eneo la namba 9, hivyo mpango wa kocha ulikuwa kuwatia presha wapinzani wao kwa kuhakikisha anao wafungaji na yeyote kati yao wangeweza kutikisa nyavu. Wakati kocha Sead Ramovic akipanga hilo, akairudisha timu kwa Stephani Aziz Ki katika eneo la ubunifu akiwa peke yake. 

Pacome Zouzoua alianza mchezo huo akiwa benchi. Mwalimu alihitaji mabao bila kuelewa nyenzo ya kutengeneza mabao hayo. Mkakatiwa MC Alger ulikuwa ni kushughulika na Aziz Ki kuliko wachezaji wengine wowote. Aziz Ki ndiye nyenzo muhimu ya kutayarisha mabao, lakini ilihitaji msaada wa mshirika wake aliyekuwa benchi. 

Kazi ya Mudathir Yahya na Khalid Aucho ni kudhibiti tempo ya mchezo na kuelekeza namna timu inavyoweza kuwashambulia wapinzani. Hata hivyo wachezaji wawili hadi watatu walikuwa na kazi ya kumdhibiti Aziz Ki hali iliyosababisha akose nafasi za kupiga mashuti kuelekea langoni mwa adui. MC Alger walifahamu hatari wanayokabiliana nayo endapo wangelimwachia Aziz Ki kufanya atakavyo. Kazi yao ilikuwa kuua mipango yote iliyokuwa inapangwa na Aziz Ki hivyo kujikuta mipira haiendi kwa Dube, Mzize wala Musonda. 

Ukuta usiofanyiwa majaribio

Kucheza dhidi ya timu inayojilinda au kujihami kwa muda mwingi wa mchezo unahitaji wachezaji wabunifu ili waweze kupenya ngome yao. ukuta wa MC Alger ulijipanga kucheza kwa kushtukiza kipindi cha kwanza, kisha kipindi cha pili wakarudi nyuma zaidi kwa kuhakikisha wanacheza kwenye eneo lao na kuboresha mashambulizi ya kushtukiza. 

Hii ina maana nyenzo ya kocha wa Yanga ilikuwa Aziz Ki ilizingirwa kwa kuongezewa wachezaji wengine ambao waliziba mianya yote na kufanya ukuta uwe mgumu. Aziz Ki asingeweza kwenda kulia na kushoto akiwa mbunmifu peke yake. Kazi ya mwalimu ilikuwa kuona kasoro hii na kwamba mbunifu msaidizi alingekuwa ameongeza akili ya ziada katika kutengeneza njia za mabao. Hata Pacome Zouzoua alipoingizwa kipindi cha pili hakuweza kufanya maajabu yoyote kwa sababu alikuwa nje ya ‘rhythms’ ya timu na hivyo kazi ya kumdhibiti Aziz Ki iliendelea kwa urahisi mno akiwa ameathiriwa na uchezaji wa kihuni wa waaarabu. Je ni kwanini mwalimu alipunguza eneo la ubinufu au hakuwa na uelewa juu ya uchezaji wa timu za Kiarabu? 

Washambuliaji watatu bila ulinzi

Majaribio matatu yalifanywa na MC Alger yangeweza kuleta madhara kwa Yanga. MC Alger walielewa Yanga walitaka bao, na waliutaka mpira sana. MC Alger walichokifanya ni kuhakikisha wanaivuruga safu ya kiungo kwa sababu ilikuwa na upungufu wa ubunifu hivyo walikuwa wanafanya majaribio ya mipira mirefu ambapo mmojawapo nusura uzao bao baada ya Djigui Diara kuliacha lango nyuma zaidi. Washambuliaji watatu walipangwa kusaka mabao bila uwiano  wa ulinzi. Kwenye eneo la kusaidia ulinzi Clement Mzize pekee alikuwa na uwezo wa kushiriki hilo, lakini haikuwa rahisi kwa Musonda au Aziz Ki na Dube. Kwahiyo katika mfumo wa washambuliaji watatu na nyuma yao kiungo mmoja unajiulzia walimu alitaka kufunga dhidi ya timu iliyohitaji kuziba mianya tu? 

Wafungaji si lazima wawe wabunifu, lakini wabunifu ndiyo wanaweza kuwa wafungaji wazuri. Katika kikosi cha Yanga kuna wabunifu watatu wa Kimataifa, Aziz Ki, Pacome na Cletous Chama. Mchezo huo ulihitaji akili za wabunifu hawa kuliko washambuliaji watatu waliopewa jukumu la kuongoza safu ya ushambuliaji. Iliwezekana kuwapanga wote w atatu wkaiwa na mshambuliaji mmoja kwani mkakati wa MC Alger ulijulikana sio kushambulia bali kujihami na kuzuia Yanga wasifunge bao lolote. Hapa mwalimu alitakiwa kutafuta mabao kupitia viungo washambuliaji wake huku mshambuliaji akiwa Mzize pekee pale mbele.

Imani ya mashabiki kwa kocha

Kati ya mambo ambayo kocha wa Yanga anatakiwa kukabiliana nayo ni ukweli kwamba mashabiki wa Yanga ahwajaweka imani kubwa kwa mwalimu huyu. Huyu ni mwalimu ambaye wanamwona kama anafanya majaribio kwani Yanga wamekuwa na makocha wenye sifa kubwa na uwezo wa kuzichanga karata zao za ushindi. Katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Yanga wamevuna pointi 8 pekee. Kwa kuangalia uchezaji wa timu, mbinu na ushindi pamoja na nanamn anavyotangazwa kwenye vyombo vya habari kama kocha mzuri na mwenye ari, hilo halipingiki lakini bado anacho kibarua cha kushinda imani kwa mashabiki. Hata kama hawasemi lakini ni dhahiri kocha huyu anahitaji kufanya kazi kubw aya kushinda imani ya mashabiki. Tuwaombee safari nzuri katika mechi nyingine za  Ligi Kuu.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

Hesabu na vita ya Yanga zitatimia?

Tanzania Sports

Ujanja wa Eddie Howe una mipaka