Newcastle United
INGEKUWA nyumbani Tanzania tungesema muosha huoshwa. Ndicho kilichtokea kwenye mchezo kati ya Newcastle United na Bournemouth wikiendi hii. Katika mchezo huo Newcaster United ilibugizwa mabao 4-1 huku maelfu ya mashabiki wao hawakuamini kipigo hicho. Wakati wa mchezo huo niliwazingatia wachambuzi wa wawili Alain Shearer na Stev McManaman ambao waliuchambua mchezo huo na kwanini Newcastle walichapwa. Katika mchezo huo kuna mambo kadhaa yamejitokeza ambayo msomaji wa TANZANIASPORTS anapaswa kufahamu mambo muhimu yaliyotokeza kwenye mchezo huo.
Ujanja wa Eddie Howe…
Katika michezo kadhaa ya hivi karibuni kocha wa Newcastler United ameonesha uimara katika kuongoza timu hiyo. Kiufundi aliwazidi washindani wake kwenye michezo iliyopita wakiwemo Man United na Arsenal. Hata hivyo katika mchezo wake dhidi ya Bornemouth alijikuta akizidiwa maarifa katika ulinzi wa kushoto na kulia, kwani wapinzani wake walitumia zaidi eneo kushoto kwenda katikati ya 18. Wachezaji wa Bornemouth walikuwa wakicheza mchezo wa ajabu kidogo, kwani muda mwingi walikuwa wakiwalazimisha beki wa kushoto wa Newcastle kukosa nafasi ya kuungana na Gordon upande wao. Hali hiyo ilimlazimu Gordon kurudi nyuma zaidi na kushindwa kutekeleza jukumu la kushambulia. Upande huo Bournemouth walihakikisha wanadhibiti nyendo zote za kuandaa mashambulizi dhidi yao.
Kasi ya mchezo
Newcastle United huwa wanakabiliana na wapinzani wa aina yeyote lakini katika mchezo wao Bournemouth walijikuta wakizidiwa katika eneo la kasi ya mchezo. Viungo wao Joelinton na Bruno Guimares hawakuweza kukimbizana na vijana wa Bournemouth. Kutokana na kasi hiyo safu ya kiungo ya Newcastle united ilijikuta ikirudi nyuma kufuata mipira zaidi. Katika kasi hiyo, Bournemouth walikuwa imara katika upigaji w apasi za haraka na spidi.
Joelington na Bruno wlaijikuta wakilambwa kadi za njano kutokana na kucheza rafu mara kwa mara. Joelington aliingia kwenye ugomvi mara nyingi na kuonywa na mwamuzi. Kiufundi Joelington anapenda kucheza kibabe, ana matumizi makubwa ya nguvu. Katika timu hiyo ukiwakamata wachezaji watatu; Bruno, Joelington na Gordon, basi timu yao inashindwa kuwapeleika moto wapinzani wao na mshambuliaji wao Alexandre Isak anakosa makali ya kupachika mabao kwani wapishi wake wazingirwa kila upande.
Silaha tatu za Bournemouth

Justin Kluivert aliondoka na mpira katika uwanja wa St. James Park baada ya kutupia mabao matatu kati ya manne. Huyu ni mtoto wa aliyekuwa mshambuliaji hatari wa Barcelona, Patrick Klutivert wa Uholanzi. Justin alerthi kipaji cha baba yake, lakini yeye anajua kupiga mashuti makali kuliko mzazi wake. umahiri wa Patrick Kluivert ulikuwa kwenye mabao ya vichwa, na alitamba katika klabu na timu ya taifa huku akipikiwa krosi nyingi za mabao.
Katika mchezo wa Bournemouth na Newcastle United Justin Kluivert, Jebbison na Dango walikuwa wachezaji hatari zaidi. Cha kushangaza ni kwamba wachezaji hawa walikuwa wakipokea pasi walikwenda kwenye kona (maungio) ya 18 na eneo la hatari. Kwenye eneo hilo ndipo mipango ilikuwa inasukwa kwa pasi za haraka na zenye kasi kubwa. Wakati Jebbison na Kluivert wakitaka kuipenya ngome ya Newcastle United, Dango alikuwa na jukumu la kuingia kwenye boksi kungojea mip[ira ya pasi yenye kasi kutoka kwa Kluivert. Jambo lingine lililojitokeza ni aina ya ufungaji wa mabao ya Bournemouth. Mashuti makali toka nje ya 18 yalionesha soka la kibabe na lile la zamani ambalo linawafanya mabeki washindwa kuwakabili washambuliaji hivyo hujielekeza kwenye mwelekeo wa mpira.
Newcastle walikwamia hapa
Tatizo la Newcastle ya Eddie Howe wanashindwa sana kucheza dhidi ya viungo visheti. Hawa ni viungo wabunifu ambao wanamuono wa mbali katika usakataji wa kandanda na upachikaji wa mabao. Mabeki wa Newcastle muda mwingi wakiingia kwenye eneo lao la ulinzi walikuwa watengeneza mistari miwili kuzuia nafasi (zonal marking) badala ya kuzuia mchezaji mmoja mmoja.
Bournemouth walikuwa na silaha ya kuhakikisha wanawashtukiza kwa kupiga mashuti makali lango ambapo golikip wa Newcastle anakuwa anemzingiwa na mabeki wake hivyo kushindwa kufanya tathmini ya haraka juu ya mweleko wa mpira. Uzuiaji wa timu ya Newcastle United ni ule wa nafasi, ndiyo maana walijikuta wakifungwa katika mazingira ambayo hawakutarajia na kuwaachia majonzi mashabiki wao waliofurika kwenye uwanja wa St. James Park.
Uchungu wa Alain Shearer
Ni kazi ngumu kuchambua timu unayopenda na kukiri madhaifu yake. Alain Shearer aliketi kwenye kiti cha studio za televisheni akiwa ametulia lakini kamera zilionesha sura ya ndani kabisa kukosa amani ya kipigo kikali cha mabao 4-1. Shearer alikuwa nahodha wa Newcastle Unted wakati wa ujana wake hadi alipoelekea kustaafu. Alicheza kwa mafanikio lakini kwenye dimba la St. James Park. Katika uchambuzi wake alikiri Bournemouth kuwazidi maarifa viungo wa Newcastle, eneo ambalo linapaswa kutafutiwa mpango wa pili kusaka ushindi. Viungo wa Newcastle wakibanwa na wapinzani hawa wanavurugwa na kucheza kwa hasira na hivyo kulambwa kadi za njano. Hicho kilichotokea, na hivyo Eddie Howe atarudi kwenye meza yake ya mipango; je ana plan B yoyote ya kushinda anapokutana na timu kama Bournemouth? Tusubiri.
Comments
Loading…