in , , ,

Arsenal walihitaji majibu ya ujasiri na uthubutu

Ukimya katika Elland Road ni nadra. Ukilianzisha, basi ujue inakula kwako, Mwanzo ilikuwa kelele kama ilivyotarajiwa, huku akili na uwezo wa Arsenal vikifanyiwa mtihani mzito na mashabiki wanaojulikana kwa kufanya kila wawezalo kuisukuma timu yao na kuingia vichwani mwa wapinzani.
“Mtaharibu,” walidokeza mashabiki wa Leeds pande zote za uwanja. Ndiyo maana kilichotokea baadaye kilikuwa cha kuzingatiwa sana—Arsenal walifanya kile ambacho kila timu yenye ndoto kubwa hulazimika kufanya katika nyakati muhimu, shinikizo likiwaka kama lilivyokuwa kwa wiki kadhaa zilizopita.

Arsenal walipata mchanganyiko sahihi wa ujasiri, kujitoa na umakini uliowapa uongozi uliopunguza sauti ya Elland Road. Pointi tatu zilipoonekana salama, mvua ilianza kugonga paa la uwanja kwa kishindo cha chuma, na mazingira yakapoa kwa gumzo hafifu huku Arsenal wakitandaza mpira wakisaka mabao zaidi. Huo ni udhibiti wa ugenini wa darasani.

Ushindi huo ulitokana na pengo la ubora walilolizalisha kwa njia mbili—kwanza, kuendana kimwili na jitihada za Leeds zilizojaa nguvu na mbio; pili, kuonyesha kiwango cha ufundi kilichowezesha wao kutawala na kuibuka na ushindi mnono. Kijumla na kibinafsi, mechi hii ilipaza sauti ya ‘majibu’. Lilikuwa hitaji la msingi baada ya michezo mitatu ya ligi ambapo pointi saba zilipotea.

Declan Rice alizungumza kwa niaba ya kikosi alipofafanua walivyojaribu kugawa na kudhibiti maumivu hayo. “Sisi sote ni watu wazima na tumepitia mengi kiasi cha kujua kwamba michezo mitatu iliyopita tumepata tu pengo,” alisema katika mahojiano na Sky Sports baada ya mechi. “Tulijua lazima tutoke hapo na pointi tatu.”

Martin Zubimendi, aliyekuwa amehusishwa na mabao mawili ya Manchester United wikiendi iliyopita, alionyesha dhamira ya kujirekebisha kupitia shangwe yake ya furaha. Kichwa chake kilichofungua bao kilishuhudia pia akili ya kusoma mchezo na harakati zake. Bao hilo lilitengenezwa na pasi safi kutoka kwa Noni Madueke. Baada ya Bukayo Saka kupata mshtuko mdogo wakati wa mazoezi ya kabla ya mechi, Madueke alipandishwa ghafla kuanza mechi ya Ligi Kuu kwa mara ya nane msimu huu.

Katika ushindi wa Jumatano wa 3-2 dhidi ya Kairat, Madueke alipiga shuti lililozua mizaha mitandaoni, watu wakitania lilikuwa likielekea nchi au alama tofauti. Lakini Elland Road, Madueke alichukua jukumu la kutengeneza nafasi kutoka upande wa kulia, na kufikia mapumziko, mipira miwili yake ilikuwa imechangia uongozi wa 2-0.

Kona yake ilimchanganya kipa Karl Darlow, aliyepiga mpira karibu na mstari wa goli licha ya wachezaji watatu waliokuwa karibu naye wote kuvaa jezi nyeupe. Arsenal wamekuwa karibu kufunga moja kwa moja kutokana na kona msimu huu, Saka na Rice wakikaribia kwa mipira yao sahihi chini ya mtambaa panya. Madueke aliikaribia zaidi—na wenzake walimpongeza bila shaka kwamba lilikuwa bao lake bora.

Baada ya kuonja adhabu ya kona kipindi cha kwanza, Leeds walikabili changamoto tofauti kipindi cha pili, Mikel Arteta alipobadilisha washambuliaji kadhaa na mchezo wa wazi wenye akili ukazaa matunda. Kilichovutia zaidi, nahodha Martin Ødegaard—aliyelazimika kukubali benchi—aliingia badala ya Kai Havertz aliyerejea, na mpango wa Arteta ukafanya kazi: nguvu za Havertz zilikuwa muhimu kukabili uchezaji wa moja kwa moja uliotarajiwa, na Ødegaard akaingia akiwa mbichi, huru, na kufurahia dakika zake.

Farasi kwa uwanja wao—Arsenal wakakimbia na mchezo. Ødegaard alihusika katika mabao mawili. Kwanza alimpa nafasi Gabriel Martinelli, Mbrazili akampita mlinzi wa Leeds kama anasubiri basi la KAUDO, akakata nyuma na kutoa krosi maridadi kwa Viktor Gyökeres kuumalizia. Kisha Ødegaard akamsaidia Gabriel Jesus, ambaye kwa miguu yake ya kucheza SAMBA,alimdanganya mlinzi kabla ya kuupiga mpira kona ya mbali.

Kwa jumla, hii ilikuwa tiba tamu na yenye ufanisi kwa timu iliyohitaji zaidi kutoka kwa safu yake ya ushambuliaji.

Kwa heshima ya mashabiki wa Leeds, waliimba mvua ikinyesha kuhusu kubaki ligi licha ya kipigo cha 0-4. Kijana mmoja akipita alisikika akipaza, “Waingieni!” Ni suala la mtazamo. Wanajua lazima waandike kando matokeo dhidi ya Arsenal msimu huu.
Lakini kwa wageni, kwa namna yake, huu unaweza kuwa mchezo wa kubadili mwelekeo wa msimu. Bila shaka wangehisi kuta zikisogea kama mambo yasingeenda vizuri.

“Tunaongelea kelele,” alisema Arteta baada ya mechi, “lakini hii pia ilikuwa kelele nzuri—chanya sana. Kila mara tunapenda kuzungumzia kelele nyingine.
“Matarajio ni kushinda kila mechi. Tunashindana na wapinzani wakubwa sana, na hilo linapaswa kutupa nguvu na hamu ya kushinda. Tulitaka kuonyesha ni kwa kiasi gani tulitamani ushindi huu.”

Arsenal walihitaji kuonyesha uso tofauti baada ya kukatishwa tamaa na kukosolewa. Hawakuweza kuruhusu mashaka yaote mizizi. Walijibu kwa kila njia.

Report

Written by Israel Saria

I have been involved with sports in Tanzania as a Volleyball Coach for many years—and was a Tanzania Amateur Volleyball Association (TAVA) leader. I studied sports management at Leipzig University in Germany and understand the science behind sports. That led me to work as a football pundit, with the BBC ( Swahili service) in London. That experience and exposure took me to covering the 2010, World Cup in South Africa. This provided me with a great insight into international level football commentary and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics.I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany, Italy, Belgium, Ireland, France, Kenya etc, and visited almost all of the key football stadiums across United Kingdom, and Europe.

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

Arsenal kuwa mabingwa-ni mapema sana

Tanzania Sports

Miaka 3 sasa: mashtaka dhidi ya Man City vipi?