in

Chelsea na BlueCo sasa wako ‘Seriously’

Chelsea na wamiliki wao wa BlueCo sasa wanaanza kuelewa umuhimu wa kuwa na kocha mwenye hadhi kubwa, heshima na “aura” ndani ya klabu baada ya kumpata Xabi Alonso kama meneja mpya.

Mashabiki wengi wa Chelsea waliondoka mapema Wembley baada ya kushindwa na Manchester City kwenye fainali ya FA Cup, jambo lililoonyesha wazi jinsi hali ya hewa ndani ya klabu ilivyo mbaya kwa sasa. Hakukuwa na shangwe wala kuonyesha sapoti kwa wachezaji waliopoteza, ishara kwamba Alonso ana kazi kubwa ya kurudisha imani, umoja na ari ndani ya timu.

Watu wengi wanajiuliza kwanini Alonso amekubali kujiunga na Chelsea kwa mkataba wa miaka minne. Baada ya kupitia kipindi kigumu akiwa Real Madrid, ambapo alikumbana na nguvu ya baadhi ya wachezaji wakubwa na changamoto za kujenga mradi wake, wengi walidhani angeepuka mazingira yenye presha kama Stamford Bridge. Lakini Alonso anaamini bado ana uwezo wa kujijenga upya na kufanikiwa.

Kwa Chelsea, huu ni ushindi mkubwa sana. Tangu BlueCo ichukue klabu mwaka 2022, Alonso anakuwa meneja mwenye jina kubwa zaidi waliyewahi kumteua. Walivutiwa naye tangu alipokuwa akiiongoza Bayer Leverkusen na kutwaa ubingwa wa Bundesliga mwaka 2024 mbele ya Bayern Munich.

Kitu kilichowavutia zaidi viongozi wa Chelsea si uwezo wake wa kufundisha pekee, bali pia uongozi wake. Alonso amepewa rasmi cheo cha “manager” badala ya “head coach”, ishara kwamba klabu sasa inaamini umuhimu wa kumpa kocha mamlaka makubwa zaidi. Chelsea walifurahishwa sana alipoongelea suala la kujenga utamaduni wa ushindi na kuunda “mentality monsters” — wachezaji wenye tabia ya ushindi na moyo wa kupambana.

Kwa miaka ya karibuni, Chelsea walionekana kuamini kuwa makocha hawana athari kubwa sana kwenye matokeo ya timu, wakiegemea zaidi takwimu na mfumo wa usajili wa vijana. Lakini sasa wanaanza kuona kwamba makocha wakubwa huleta kitu kisichopimika kwa namba: uwepo wao, mvuto wao na heshima yao. Kwa kifupi, “aura”.

Ujio wa Alonso unaweza pia kusaidia kuvutia wachezaji wakubwa kujiunga na Chelsea, hata kama klabu hiyo inaweza kukosa kucheza UEFA Champions League kwa mara nyingine tena.

Chelsea pia wamekubali kimya kimya kuwa walifanya makosa katika miaka ya hivi karibuni, hasa kwenye sera yao ya kusajili vijana pekee. Alonso anaamini timu inahitaji mchanganyiko wa vipaji vya vijana na wachezaji wenye uzoefu ili kurudi kushindana na timu bora Ulaya.

Hata hivyo, Alonso haoni Chelsea kama timu iliyoharibika kabisa. Anaamini kikosi hiki kina vipaji vikubwa na kinahitaji maboresho machache tu — golikipa wa kiwango cha dunia, mabawa wenye makali zaidi, uimara kwenye safu ya ulinzi na msaada zaidi kwa mshambuliaji João Pedro.

Sasa jukumu kubwa kwa Chelsea ni kumpa Alonso muda, mamlaka na utulivu wa kujenga timu kwa mtindo wake. BlueCo wanaonekana kuelewa kuwa ili kujenga timu ya washindi, lazima kwanza umpe nguvu meneja mwenye uwezo wa kuiongoza.

Report

Written by Israel Saria

I have been involved with sports in Tanzania as a Volleyball Coach for many years—and was a Tanzania Amateur Volleyball Association (TAVA) leader. I studied sports management at Leipzig University in Germany and understand the science behind sports. That led me to work as a football pundit, with the BBC ( Swahili service) in London. That experience and exposure took me to covering the 2010, World Cup in South Africa. This provided me with a great insight into international level football commentary and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics.I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany, Italy, Belgium, Ireland, France, Kenya etc, and visited almost all of the key football stadiums across United Kingdom, and Europe.

What do you think?

64 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

Wako wapi makocha wazawa katika EPL?

Tanzania Sports

Arsenal Bingwa wa EPL