in , ,

Arsenal kuwa mabingwa-ni mapema sana

Arteta: Gumzo la Arsenal kuwa mabingwa-mapema ‘linapeleka mwelekeo sehemu isiyo sahihi’

• Kocha asema sifa kutoka nje “haziongezi thamani”
• Arsenal, wakiwa mbele kwa pointi saba, wanamkaribisha Manchester United

Mikel Arteta amesema hakuna mtu mwenye msukumo, njaa na hamu ya kushinda Ligi Kuu msimu huu kuliko yeye, huku akiahidi kuwa wachezaji wake wa Arsenal hawatapoteza mwelekeo kwa mazungumzo ya kuwataja kama mabingwa-wateule.

Dalili kwa Arsenal ni nzuri sana licha ya wasiwasi usioepukika miongoni mwa mashabiki wao, ambao umejitokeza katika mechi mbili zilizopita za ligi—sare za 0-0 dhidi ya Liverpool na Nottingham Forest.

Arsenal wako kileleni wakiwa mbele kwa pointi saba wanapojiandaa kumenyana na Manchester United Jumapili; wana ulinzi bora zaidi kwa idadi ndogo ya mabao yaliyoruhusiwa na wameonyesha nguvu katika maeneo mengi mengine, yakiwemo mipira ya adhabu.

Pep Guardiola, ambaye Manchester City yake iko nafasi ya pili, aliielezea Arsenal Ijumaa kama “timu bora zaidi duniani,” na Arteta amesikia kauli kwamba ubingwa uko mikononi mwao. Arsenal mara ya mwisho walitwaa taji la ligi msimu wa 2003-04.

“Sidhani kama kuna mtu yeyote mwenye motisha, njaa na hamu kubwa zaidi kuliko mimi ya sisi kwenda hadi mwisho na kushinda,” Arteta alisema. “Lakini tunajua njia pekee ya kufanya hivyo ni kubaki makini, kuwa hapa sasa, na kufanya kila tunachopaswa kufanya leo… kisha tufanye vizuri zaidi kesho. Hicho ndicho kitu pekee tunachoweza kukidhibiti. Mengine yote ni mambo ambayo hayatuongezei thamani na yanaweza kupeleka umakini mahali pasipo sahihi.

“Ni kuzungumza kila siku kuhusu kile tunachopaswa kufanya, kile tunachofanya, na kile tunachoweza kuboresha. Tunajua itakuwa ngumu sana Jumapili na kama tutaanza kujiandaa Jumapili tutakuwa tumechelewa. Ndiyo maana tayari tulianza maandalizi baada ya ushindi wetu wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Inter Milan Jumanne.”

Arteta alisisitiza pia kuwa City, ambao hivi karibuni wameyumba, hawawezi kuandikwa nje ya mbio. “Huhitaji kurejea mbali kwenye historia ya klabu hiyo katika miaka 10 iliyopita na kile wanachoweza kufanya,” alisema. “Tunajua ni nini tunapaswa kuweza kufanya ili kushinda Ligi Kuu hii.”

Arteta ana sababu nyingine ya kuwa na matumaini kutokana na hali nzuri ya afya ya wachezaji wake. Riccardo Calafiori na Piero Hincapié walifanya mazoezi Ijumaa baada ya majeraha na, kulingana na kocha wao, wanaweza kupatikana dhidi ya United. Arsenal wanamsimamia kwa umakini Kai Havertz katika kurejea kwake baada ya kukaa nje kwa muda mrefu, lakini mchezaji pekee aliyethibitishwa kukosekana ni Max Dowman. Kwa miaka mingi imekuwa vigumu kubashiri vikosi vya Guardiola. Sasa, akiwa na uwigo mpana wa chaguo zenye ubora katika kila nafasi ndani ya timu yake.

“Hilo daima ni jambo chanya,” alisema. “Kwa wachezaji pia, kwa sababu inamaanisha wanapaswa kuinua viwango vyao mazoezini ili kustahili kucheza. Na tunapotaka kubadili mchezo tutakuwa na chaguo la kufanya hivyo. Hili ni jambo ambalo, katika miaka ya hivi karibuni, hatujalipata kwa sababu mbalimbali. Sasa tulipolipata, tunapaswa kuhakikisha tunalitumia kwa njia sahihi.”

Arteta ana historia kama mchezaji na kocha dhidi ya Michael Carrick, ambaye amerudi kwa awamu ya pili kama kocha wa mpito wa United. Mwishoni mwa awamu ya kwanza msimu wa 2021-22, timu ya Carrick iliifunga Arsenal ya Arteta 3-2 Old Trafford. “Yeye ni mmoja wa viungo namba 6 ninaowapenda zaidi,” Arteta alisema. “Ni mwenye akili sana na hakuonekana kuvunja jasho—alikuwa na udhibiti mkubwa wa mchezo. Kumbukumbu si nzuri [dhidi yake kama kocha], hivyo tunapaswa kuzibadilisha.”

Report

Written by Israel Saria

I have been involved with sports in Tanzania as a Volleyball Coach for many years—and was a Tanzania Amateur Volleyball Association (TAVA) leader. I studied sports management at Leipzig University in Germany and understand the science behind sports. That led me to work as a football pundit, with the BBC ( Swahili service) in London. That experience and exposure took me to covering the 2010, World Cup in South Africa. This provided me with a great insight into international level football commentary and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics.I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany, Italy, Belgium, Ireland, France, Kenya etc, and visited almost all of the key football stadiums across United Kingdom, and Europe.

What do you think?

69 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

Morocco yafikiria kuchukua hatua za kisheria

Tanzania Sports

Arsenal walihitaji majibu ya ujasiri na uthubutu