in , , , ,

Everton kupokwa pointi mtikisiko

City, Chelsea huenda wakapata tetemeko….

Baada ya Everton kuwa wa kwanza kuadhibiwa kwa kupokwa pointi 10 kutokana na kwenda kinyume cha kanuni za fedha, kilichobaki ni kusubiri tu kuona nani watafuata.

Wataalamu wa miamba wanajua kwamba kuna kile kinachoweza kutokea kama mtikisiko Fulani kabla ya tetemeko hasa kutokea. Hicho ndicho kinafikiriwa sasa kwamba ya Everton ulikuwa mtikisiko kidogo tun a huenda tetemeko hasa likawajia Manchester City na Chelsea.

City wameshitakiwa kwa makosa ya kwenda kinyume na kanuni za Ligi Kuu ya England (EPL) zaidi ya mara 100 katika miaka kadhaa. Chelsea wapo kwenye uchunguzi wakidaiwa kufanya makosa hayo kati yam waka 2012 na 2019 na Guardian lilibainisha wiki hii kwamba kulikuwapo malipo ya siri yenye thamani ya makumi ya mamilioni ya pauni yaliyofanywa na kampuni zinazomilikiwa na Roman Abramovich.

Mwanasheria nguli wa michezo, Catherine Forshaw anaamini kwamba City na Chelsea watakuwa wanahofia kupata adhabu kali zaidi – ikiwa ni pamoja na uwezekano wa kushushwa daraja.

Tanzania Sports

“Ikiwa u mwanasheria katika klabu hizi, lazima neva zikucheze baada ya uamuzi,” anasema Forshaw, anayefanya kazi katika kampuni ya uwakili wa michezo ya Barbanes, akiwa na uzoefu mkubwa wa kushauri taasisi zinazosimamia michezo kitaifa na klabu za soka.

“Sasa upo tayari mfano wa kufuata. Na kwa kulinganisha na Chelsea na Manchester Cit, basi Everton wanaweza kuwa wamepata adhabu ndogo zaidi. Kwa hiyo nadhani kwamba kushushwa daraja ni suala linalowezekana,” anasema.

Mwanasheria mwingine mkubwa wa soka, Nii Anteson, anagusia kifungu cha 107 na 108 cha kurasa 41 za hukumu dhidi ya Everton, akisema kinaelekea vitazingatiwa katika kesi zijazo.

Palikuwa na msisitizo kwa Everton juu ya haja ya kutenda kwa nia njema kabisa na kuiambia klabu hiyo kwamba taarifa ilizotoa kimsingi hazikuwa sahihi na hawakuwa waaminifu.

Katika uamuzi madai ya Everton kwamba walitenda kama ambavyo mhasibu wa kodi angefanya kwa ajili ya kumweka mteja wake pazuri kuhusiana na kodi na mwakilishi wa Everton akadai kwamba kazi yake ilikuwa kulinda au kutafsiei kanuni za PSR kwa faida ya mwajiri wake.

Tanzania Sports

Manchester City msimu uliopita walitwaa mataji matatu na Chelsea ambao hawakufanya vizuri sana wamo kwenye hali mbaya zaidi ya Everton kuhusiana na uvunjaji kanuni husika, ambapo Everton walikwenda kwenye kupata kiwango cha juu zaidi cha hasara kinachoruhusiwa, pauni milioni 105 katika kipindi cha miaka mitatu.

City wanashitakiwa kwa mengi, ikiwa ni pamoja na kushindwa kutoa takwimu sahihi kuhusiana na hali ya kiuchumi ya klabu hiyo, kutokutoa takwimu sahihi za malipo ya kocha na wachezaji, kuvunja kanuni za uungwana katika matumizi ya fedha na kutokutoa ushirikiano kwa Bodi ya Ligi Kuu katika uchunguzi wake. Wanakana kufanya lolote baya na kwamba wana Ushahidi wa kutosha juu ya hilo.

Suala la Chelsea ni tofauti, ambapo utawala mpya ulioingia klabuni hapo hivi karibuni umefunua na kuweka wazi udhaifu walioukuta klabuni hapo. Atenson anasema kuna ufanano Fulani kwa klabu zote hizo – kuvunja kanuni. Kilichopo sasa ni Manchester City na Chelsea kusubiri Bodi ya EPL itafanya nini, lakini moja ni wazi kwenye klabu zote mbili kwamba kijacho kitawatoka.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

Siri tano za Postecoglo ndani ya EPL?

Tanzania Sports

Klabu EPL zapinga marufuku..