in , , ,

Siri tano za Postecoglo ndani ya EPL?

LIGI KUU England imejionea ingizo jipya katika mchuano wa kuwania ubingwa nchini humo. Klabu ya Tottenham Hotspurs ya London inaelekea kuwasha gari la ubingwa mapema kutoka na matokeo yao wanayopata kila mechi. Hata hivyo katika harekati za kusaka ubingwa kwa klabu hiyo zinamiminwa sifa nyingi kwenda kwa kocha wao Ange Postecoglo, ambaye amesifiwa kwa kuiongoza vizuri klabu hiyo. TANZANIASPORTS imeichunguza klabu ya Tottenham Hotspurs na kubaini mbinu kadhaa zinazomsaidia kocha Postecoglo kuwa moto wa ubingwa msimu huu. Hata hivyo swali linaloulizwa na wadau wa kandanda ni lileile kwamba ataweza kufika mwisho wa mechi 38 au atayumba kama ilivyokuwa kwa majirani zake wa London, Arsenal? Zifuatazo ni siri za uimara wa Spurs msimu huu.

KUAJIAMINI

Staa mpya wa Spurs James Maddison amekiri kuwa wachezaji wa klabu hiyo wanajiamini kwa sababu kocha wao amekuwa na mchango mkubwa katika hilo. “amesaidia kutujengea kujiamini. Anachoongea ni kusogeza mbele uwezo wetu. Anajiamini binafsi katika njia zake, anapoongea na wachezaji anaonekana ni mwanaume wa shoka na asiye na masihara. Ujumbe wake unafika vizuri.” Alikaririwa Maddison. Ukweli ukitazama uchezaji wao, wanaonekana kujiamini na kupangilia mbinu za kusaka ushindi. Hatua ya kujiamini ni kuimarisha uwezo wa wachezaji mmoja mmoja.

MWANAMKO MPYA

Kikosi cha Spurs ni kama kimeongezewa nguvu msimu huu kutokana na uchezaji wa kiungo wa Ivoy Coast, Bisouma na Msenegali Pape Sarr. Wachezaji wawili hawa wameongezewa nguvu na James Maddison ambaye amekuwa mhimili wa kikosi hicho. Watatu hawa wameifanya Spurs icheze kwa dakika 90 wakiwa katika kasi ileile, huku wakifurahia kutandaza kandanda. Ni kama vile kocha wao amewaambia wekeni mpira chini ili watawale mchezo na kusaka ushindi. Wachezaji Bisouma, Pape Sarr na Maddison wanapenda soka la pasi na kasi. Pape Sarr ana kasi na amekuwa chachu ya uimara wa Spurs upande wa winga wa kulia.

BILA MKUBWA

Wakiwa na nahodha wao mpya Hueng Son wamekuwa kama vile apo huru Zaidi kuliko walivyokuwa na Harry Kane. Tofauti ya Harry Kane na Son ilikuwa uchezaji wao. Son anacheza kwa kasi wakati Hartry Kane alitegemea matukio ya viungo kuongeza kasi yake. Son ni mshambuliaji ambaye anaibeba Spurs kwa uchezaji wa kasi muda wote wa mchezo. Faida waliyonayo Spurs ni pale Son anapokuwa mahiri ndani ya boksi na kusahauliwa na walinzi ambao wanashtukia akiwa ameshafunga bao. Mara kadhaa amefunga mabao ndani ya boksi kuliko alivyokuwa zamani akikimbia umbali mrefu na kulifikia lango au kumpa pasi Harry Kane. Kwa sasa Son anabaki kwenye eneo la hatari, lakini hakuna staa mkubwa ambaye anaweza kumzidi mwenzake. Inawezekana Son ni mkubwa wao, lakini angali mchezaji asiye na makubwa.

VIUNGO

Eneo la kiungo ndilo linalowapa Spurs kiburi cha kufikiria ubingwa msimu huu. Kuna kama vile utatu mtakatifu kati ya Bisouma,Sarr na Maddison. Kwenye eneo la ukabaji Bisouma anatawala dimba bila wasiwasi, amekuwa akijiamini na kuifanya kazi ya viungo washambuliaji kuwa rahisi. Ni sababu hiyo Pape Sarr huonekana mara kwa mara akiwa na madhara langoni mwa adui, hali kadhalika mashuti ya Maddison nje ya 18 nayo yamekuwa mwiba. Kwahiyo uzalishaji, ufungaji na ulinzi imara wa safu ya kiungo unaifanya Spurs iwe timu ya kuongelewa mara kwa mara msimu na kudhaniwa huenda wakatwaa taji la EPL.

MABAO YA SON

Spurs hawajapoteza mchezo wowote wa EPL. Na wamefunga magoli 20 na kujikusanyia pointi 23 katika michezo 9 waliyocheza. Pengine unaweza kusema Ligi bado mbichi, lakini dalili za wazi kuwa Spurs analeta ushindani. Mshambuliaji wao Son Hueng-Min amepachika mabao 7 msimu huu sawa na staa wa Newcastle, Alexandre Isak. Katika orodha hiyo Son amepitwa magoli mawili tu na kinara wa kufumani nyavu Erlin Haaland mwenye mabao 9. Kwa maana hiyo nyota huyo amekuwa chachu pia ya Spurs kuwa hapo ilipofika. Spurs wamewazidi mabingwa watetezi Manchester City kwa pointi 23, Baada ya jana kuwafunga Fulham mabao 2-0 na kushika uongozi wa EPL.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

Simba hao hapo, wanawinda dau la Rais Samia

Tanzania Sports

Everton kupokwa pointi mtikisiko