in

Aston Villa walivyowazidi kete wapinzani EPL

£28m Ollie Watkins

Aston Villa waliofaulu kubaki Ligi Kuu ya England (EPL) kwa kuponea kwenye tundu la sindano kushuka kiangazi hiki, wamefanikiwa kuwazidi kete wapinzani wao kwenye ligi hii maarufu zaidi duniani.

hilo ni katika kufanikiwa kumsajili Ollie Watkins kwa pauni milioni 28, baada ya kuwa taifa na dunia kukumbwa na kutikiswa na virusi vya Corona vinavyosababisha homa kali ya mapafu na kuua maelfu ya watu kiasi cha ligi kusimamishwa.

Ikiwa kulikuwapo shaka yoyote miongoni mwa watu wa nje juu ya matamanio ya Villa, au ikiwa wamiliki mabilionea Nassef Sawiris na Wes Edens wangeanza kukaza misuli yao ya kifedha, kumpata Watkins kwa kuvunja rekodi kumethibitisha kile walio ndani ya klabu walichokuwa wakijua tayari.

Ni dhamira ya hali ya juu kwa klabu hii ambayo Mtanzania wa kwanza kukipiga EPL, Mbwana Samatta anachezea, katika kujiimarisha tayari kwa mchakamchaka wa msimu mpya unaoanza wikiendi hii.

Ollie Watkins
Ollie Watkins

Wapo waliokuwa na wasiwasi kwamba Samatta amechagua klabu ambayo siyo na kwamba angeishia kushuka nayo katika msimu wake wa kwanza, lakini sasa kibao kimegeuka uzuri, ikionesha kwamba hii ni klabu inayomaanisha kazi au biashara ya ukweli.

Kutumia pauni milioni 28 kumpata mshambuliaji mwingine huyu ni onesho kwamba sasa ni kazi inaendelea ya kujiimarisha. Watkins na mwenzake Mattyu Cash aliyesajiliwa kwa pauni milioni 16 wametoka Ligi Daraja la Kwanza, hapa ikiwa ni maarufu kama Championship, lakini madili yao yalifikiwa kimsisimko.

Huu ni mwanzo tu, ambapo Villa wamewapiga washindani wao wengine wote kwenye uwaniaji wa mchezaji huyo mshambuliaji na imeonesha nguvu yao na wawekezaji – Sawiris, anayemiliki kampuni ya ujenzi ya Orascom Construction na ana hisa kwenye kampuni ya Adidas wakati Edens amewekeza kwenye klabu ya Milwaukee Bucks, kwa pamoja wakiwa na utajiri wa pauni bilioni 8.5.

Kwa kawaida, ni mambo tofauti kabisa – moja kuwa na fedha, kama ilivyo kwa Roman Abramovich wa Chelsea au Familia ya Glazers wa Manchester United, na jingine kabisa kuzitumia fedha kuwekeza wakati klabu hawajafanya uzalishaji kivile, tena wakijiendesha kwa hasara wakati huu wa Covid-19.

Kocha Mkuu Dean Smith amekuwa kwa muda akitamani sana kumchukua Watkins lakini kitendo cha Callum Wilson kujiunga Newcastle United kutoka Bournemouth, kiliharakisha usajili wa mshambuliaji huyo kutoka Brentford.

Tanzania Sports
Ollie Watkins

Ikiwa hiyo ilimaanisha kulipa zaidi kidogo kuliko ilivyotarajiwa, basi ndivyo ilivyokuwa kuweza kumpata mchezaji muhiomu aliyemtaka Smith. Kocha huyo alidhani kwamba Wilson angekuwa mchezaji wa Villa wiki jana, lakini tanzaniasports.com inaelewa kwamba baada ya dau la pauni milioni 21 (pauni milioni moja zaidi ya la Newcastle) ilitokea kwamba Newcastle walimchukua kwa vile mchezaji mwenyewe alitaka kwenda kaskazini ya nchi na aliweka wazi matamanio yake hayo.

Bournemouth waliheshimu matakwa yake, kutokana na kuwatumikia kwa uaminifu, wakamruhusu aondoke na kwenda alikotaka licha ya kupokea ada kidogo zaidi ya waliotoa Villa. Villa walisikitishwa kumkosa kwani walikuwa wametoa madau matatu wakiamini kwamba wangefanikisha jambo lao lakini halikuwa.

Mpango wao wa awali ulikuwa kumsajili pamoja na Watkins, kwa hiyo usajili wa Watkins unamaanisha kwamba halikuwa chaguo la pili. Smith alisisitiza haja ya kupata mshambuliaji mwingine kabla ya msimu kuanza.

Hatua hiyo inamridhisha Mkurugenzi wa Michezo mpya, Johan Lange ambaye sasa walau anaweza kupumua kwa ahueni baada ya mwezi wake wa kwanza klabuni hapo. Villa walilenga kutumia kima kidogo kwenye usajili, lakini sasa kinaweza kupanda hadi zaidi ya pauni milioni 33 ikijumuishwa na posho nyingine kwa mchezaji huyo.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Wananchi

Yanga wanajichafua wenyewe

Jezi mpya ya Yanga

Ni duka la Yanga au GSM ?