in , ,

Zidane anasajili wachezaji wake Real Madrid

Msimu uliopita (2021/2022) wakati Jude Bellingham akiwa Borussia Dortmund alipewa mwaliko wa kutazama mechi ya Real Madrid kwenye dimba la Santiago Bernabeu…

IPO habari moja ya kuchekesha katika usajili wa Real Madrid, kwamba laiti uongozi wa timu hiyo ungemsikiliza wakati alipopendekeza Eden Hazard asajiliwe mapema, basi wangekuja kupiga apesa ndefu na Chelsea. Zinedine Zidane aliwahi kuhojiwa kuhusu chipukizi wapya waliokuwa wanacheza katika Ligi Kuu ya Ufaransa, na wakati huo Eden Hazard alikuwa anang’ara pale klabu ya Lille. 

Bila kumung’unya maneno alimjibu mwandishi aliyemhoji kwamba kama kuna kitu alitamani wakati ule ni kumwona nyota wa Lille ya Ufaransa, Eden Hazard akisajiliwa na Real Madrid. Viboba wa Real Madrid waliipata habari hiyo, lakini wakawa wagumu kwa mtindo uleule uliowafanya wamkose Ricardo Kaka akiwa kinda kisha wakaja kupigwa pesa nyingi alipohama AC Milan uzeeni. 

Hazard naye kwa upande wake alikuwa wazi kuwa mtu anayependa kufanya naye kazi na shujaa wake ni Zinedine Zidane. Akaongeza kuwa anatamani kuchezea Real Madrid siku moja. Lakini mabosi wa Real Madrid walimsajili nyakati za mwisho akiwa ametumika vilivyo Chelsea. Matokeo yake Hazard hakuwapa kile walichotakiwa kupewa akiwa kwenye kilele cha ubora.

Sasa habari mpya inamhusu Jude Bellingham nyota mpya wa Real Madrid. Kama walivyo wachezaji wengine wakongwe wanatumika kama mashujaa au wa mfano kwa wachezaji chipukizi. Jude Bellingham anampenda Zinedine Zidane. Na Zidane anafahamu hilo kuwa yeye anaigwa na wachezaji wengi. 

Msimu uliopita (2021/2022) wakati Jude Bellingham akiwa Borussia Dortmund alipewa mwaliko wa kutazama mechi ya Real Madrid kwenye dimba la Santiago Bernabeu. Heshima hiyo ilikuwa ni mwaliko kutoka kwa Zinedine Zidane na mgeni huyo alipaswa kwenda kuketi kwenye eneo la heshima la Zizzou. Bellingham bila kupoteza muda na kwa shangwe na nderemo alisafiri kutoka Ujerumani hadi Hispania kwenda kutazama mechi za Real Madrid akiwa mgeni wa Zidane. 

Heshima zote akapewa na akaketi kwenye eneo lenye heshima ya Zidane kwenye uwanja wa Santiago Benarbeu. Hatujui mazungumzo kati ya Zidane na Bellingham yalikuwaje lakini katika mahojiano ya hivi karibuni amekiri kuwa siku ile alijisikia hamasa kubwa kupewa heshima na Zidane hadi kualikwa kwenda Santiago Bernabeu. 

Kana kwamba haotishi baada ya safari hiyo ambayo unaweza kusema ya kawaida, Jude Bellingham amesajiliwa na Real Madrid Juni mwaka 2023. Huwezi kupuuza nguvu za Zinedine Zidane ambaye anahudhuria karibu kila mechi kwenye samba la Santiago Bernabeu licha ya kutokufundisha timu yoyote. 

Ni kama vile Zidane anataka wachezaji wake wa kusajiliwa. Ni kama vile Zidane anaweza kutabiriwa kuwa Rais wa Real Madrid. Ndoto ya urais wa Real Madrid anayo pia Luis Figo, kwa hiyo Zidane anafanya kimya kimya. Angalia tena usajili wa Real Madrid ni ule ambao umekaa ‘kimwonekano wa Zidane’. 

Tanzania Sports

Brahim Diaz na Fran Garcia wamerudishwa Santiago Bernabeu. Hawa ni vijana waliopewa nafasi na Zinedine Zidane. Brahim alikwenda kwa mkopo AC Milan alikokaa miaka miwili, halafu Fran Garcia alikuwa Castilla na aliwahi kucheza mechi kadhaa timu ya wakubwa chini ya Zidane kabla ya kwenda Rayo Vallecano. Sasa wote wawili wamerudi. Angalia usajili wa Arda Guller, mchezaji kinda kutoka Fenerbance mwenye umri wa miaka 18 ni swahiba wa Mesut Ozil. 

Lakini kinda huyo tena amelitaja jina la Zinedine Zidane kuwa sababu nyingine ya kwenda Real Madrid. Wanampenda Zidane, wanashawishika na Zidane. Uchezaji wa Arda Guller na aina ya wachezaji walioletwa kikosini hadi hivi leo wote wamekaa ‘kimuono wa Zidane’. 

Ni kama vile Zidane anausajili wake. Kwanini? Juni mwaka 2024 mwalimu wa Zidane atakuwa kocha wa timu ya Taifa ya Brazil. Carlo Ancelotti alipokuwa kocha wa Real Madrid kwa mara ya kwanza msaidizi wake alikuwa Zidane. Baadaye Zidane akaelekea Castilla. Miezi michache baada ya kufukuzwa Rafa Benitez, ikawa zamu ya mwanafunzi wa Ancelotti, yaani Zinedine Zidane. 

Kiufundi Zidane na Acaloetti wanao mfanano wao. Sasa hivi mjadala ni nani atakuwa kocha mpya wa Real Madrid baada ya Zinedine Zidane? Majina kama Raul Gonzalez, Guti, Xabi Alonso, Jose Mourinho. Hata hivyo Zinedine Zidane anayo nafasi kubwa ya kuinoa tena Real Madrid kuliko wengine hao. 

Aina ya wachezaji wa Zidane ni wale wa vipaji, visheti wa hali ya juu. Brahim,Arda Guller, Jude Bellingham na beki wa kushoto Fran Garcia hawa wote ‘wanaucheza wa Kizidane’, isipokuwa Joselu pekee ingawa naye hucheza “kikarim Benzema” (swahiba wa Zidane). Ni kama vile Zidane anashiriki pakubwa kusuka timu mpya ya Real Madrid nyuma ya pazia. Kama ndivyo, ni rahisi kupewa timu kwa mara tatu lakini kuna stori nyingi za kuchekesha kati ya usajili wa Real Madrid na Zidane.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

72 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

JUA LIMEZAMA KWA DAVID DE GEA

Bei za wachezaji wa England zimekuwa zikikuzwa

Wanasoka wa England wanadai kupita kiasi – na si ajali