in , ,

KAMA TUNGEJIFUNZA KWA MBEYA SUPER CUP NA MUUNGANO MUFINDI

Muundo wa mashindano hayo unaweza kuyahusisha na kile kinachoendelea kwenye mashindano ya Ngao ya Jamii….

MICHUANO ya soka jijini Mbeya maarufu kama Mbeya Super Cup ni miongoni mwa mashindano mazuri yanayowapa wachezaji,makocha na viongozi eneo la kuboresha uendeshaji wa mpira nchini Tanzania. Ifahamike suala la mashindano madogo au maarufu kama Bonanza ni sehemu ya kukuza michezo hasa inaposhirikisha timu zenye hadhi ya Ligi Kuu au nyingine zilizopo kwenye mkondo wa kupanda ngazi kutoka hatua moja kwenda nyingine, mfano daraja katika Ligi. 

Mbeya Super Cup ni mashindano yanayosimamiwa na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera. Ni mashindano yanayotumika kuziandaa timu zinazotoka mkoa wa Mbeya kushiriki mashindano ya Ligi Kuu na Daraja la kwanza. 

Mwaka 2023 mashindano haya yanashirikisha zaidi ya timu 9 kutoka nchi za Malawi na Zambia ambazo zitachuana vikali kuanzia Julai 18 mwaka huu. 

Hii ni fursa ambayo inatumika kukuza vipaji vya wanasoka wa timu hizo pamoja na kuuziana vipaji kati ya timu za Mbeya na Zambia na Malawi. Ili kukuza Mbeya Super Cup kumekuwa na majadiliano ya kuzialika timu za mkoa wa Songwe kushiriki mashindano hayo. 

Timu zinazoshiriki ni Mbeya City, Prisons, Ihefu, Ken Gold na Mbeya Kwanza.

Kila nchi duniani kuna mabonanza. Real Madrid na Arsenal wana mashindano yao ambayo hualika timu ya kucheza nayo kila msimu na kudumisha uhusiano baina yao. 

NINI MAANA YAKE?

Ukiangalia muundo wa mashindano ya Ngao ya Jamii ni wazi yamekuwa Bonanza, na bahati mbaya Bingwa amepewa nafasi ya chini. Kama nungeambiwa nipendekeze njia ya kuunda mashindano hayo, ningewaambia TFF haifai bingwa wa Ngao ya Jamii kuanzia nafasi ya chini, badala yake zingeshindana timu zingine ili inayoshinda ndiyo inakwenda kucheza na Mshindi wa Ngao ya Jamii. Mfano Yanga walitakiwa kuwekwa kando wasubiri mshindi wa timu ambayo ingeshinda hatua za awali kisha kupambana na bingwa mtetezi. 

NJIA MBADALA

Kwa vile mashindano haya yamebadilishwa kutoka mchezo wa Bingwa wa Ligi Kuu na Mshindi wa Pili (ikiwa wa Ligi Kuu ametwaa pia Ngao) basi ingewezekana kuwa na mashindano ya kuziandaa timu zetu za Tanzania na kutumia mashindano ya namna hii. Kwa mfano tunaweza kutumia mashindano ya pre-season ya Mbeya Super Cup kama njia ya kualika timu kutoka nje ili kuongeza chachu kwa timu zetu na nje. Kwamba Ngao ya Jamii ingewezekana kuanzisha mashindano yanayohusisha timu nne za juu za Ligi Kuu, kisha mbili za Zanzibar na nyingine za kualikwa toka nchi mojawapo Afrika Mashariki au mahali pengine.

FURSA KWA WADHAMINI NA VILABU

 Tayari hii ni fursa ambayo inaweza kutumika vizuri na wadhamini kushiriki kuziandaa timu zetu kwa mashindano ya kimataifa. Vilevile ni fursa kwa vilabu kupata mechi za maandalizi ya msimu na kuimarisha mipango ya Makocha na timu kwa ujumla. 

MCHEZO WA HISANI

Kwa mfano zipo tetesi kuwa huenda kukawa na mchezo wa hisani ambao utakaohusisha wachezaji wa kigeni na wazawa. Taarifa hizo zinadaiwa kufikishwa kwa wadau ili waweze kutoa maoni namna ya kufanyika kwa mchezo huo. Tunarudi palepale kuwa kiu ya mashindano ya kutosha na yenye tija inahitajika na kuwawezesha wachezaji kuwa unatimamu wa miili. Ikiwa wazo hilo la mchezo wa hisani litapatiwa kipaumbele maana yake tunaweza kuyaangalia mashindano ya Ngao ya Jamii nje ya dhana ya kufungua pazio la Ligi Kuu na kuyageuza kuwa kisima cha kuboresha mpira wetu na kuweka muundo mpya kuliko wa sasa.

KUTORUDIA MAKOSA YA KOMBE LA MUFINDI

Tanzania tumekuwa na fursa nyingi za mashindano lakini tunaanzisha na kuyazika kirahisi sana Jambo ambalo linasikitisha.

Mashindano ya Mbeya Super Cup yanaturudisha kwenye Bonanza la Kombe la Muungano Mufindi ambalo lilipata umaarufu chini ya usimamizi wa Yassin Daudi. Ni mashindano yaliyohusu huko Mufindi lakini yakatanua mbawa zake kwa kualika timu kutoka visiwani Zanzibar. Sio Siri mashindano haya yalipata umaarufu na yalionekana kuwa sehemu nyingine ya kuibua vipaji lakini nayo yameachwa yafe kiajabu ajabu tu. 

Muundo wa mashindano hayo unaweza kuyahusisha na kile kinachoendelea kwenye mashindano ya Ngao ya Jamii. Ikiwa tunahitaji eneo la mfano la kutumia kuendesha mashindano basi yapo mengi. Tunaweza kutumia mashindano ya Kombe la Muungano Mufindi, Mbeya Super Cup pamoja na hilo wazo la Mchezo wa hisani kwa wachezaji wa kigeni na wazawa.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

MAMBO MATANO YANAYOMKABILI KOCHA MPYA AZAM 

Tanzania Sports

Ajabu! Man United hata unahodha hauna mwenyewe