UPO wakati mwingine timu kutoka Ligi Kuu tano zenye nguvu huwa zinatikisa kwa muda Fulani kasha zinapoteana kwenye ramani ya ushindani. Timu za Ligi Kuu Hispania kwa mfano zinasifika kutamba kwenye mashindano mbalimbali ya Ulaya. Mfano kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya timu ya Real Madrid ndiyo baba lao. Kwenye Europa League timu ya Sevilla ndiyo inachukuliwa kama baba lao, kwa maana ya kuwa inayochukua kombe hilo mara nyingi zaidi kuliko zingine. Pia timu hizo zinatajwa kuwa na uwezo mkubwa linapofika suala la kucheza fainali ya kutwaa kombe l Ulaya.
Hata hivyo tathminiya TANZANIASPORTS inaonesha bayana kuwa msimu huu 2024/2025 kuna mabadiliko makubwa ambapo timu za EPL zimeonesha umahiri na kutawala zaidi. Umekuwa msimu ambao umewapa nafasi ya kutinga hatua kubwa na kudhihirisha kuwa zipo tayari kwa kupigania makombe la zilivyo za Hispania.
LIGI YA MABINGWA ULAYA
Haya ni mashindano makubwa nay eye mvuto zaidi barani Ulaya. Bingwa mwenye mataji mengi katika mashindano haya ni Real Madrid. Timu hiyo imechuka taji hilo mara 15 kuliko zingine. Timu zingine zinazofuata na ambazo zipo chini ya mataji 10 ni pamoja na AC Mila, Inter Milan, Man United, Liverpool, Nottingham Forest, Barcelona na nyinginezo.

Katika mashindano ya mwaka huu, klabu za EPL zimewakilishwa na Arsenal ambayo ilifanya kazi ya ziada kuivua ubingwa Real Madrid na kutinga hatua ya nusu fainali. Hata katika hatua hiyo Arsenal wamekumbana na vichapo vikali baadaya kukubali kipigo cha 1-0 nyumbanidhidi ya PSG, kabla ya kupoke akingine cha mabao 2-1 jijini Paris nchini Ufaransa. Arsenal ndiyo klabu pekee ya EPL ambayo msimu huu ilitinga hatua ya nusu fainali. Man City na Liverpool licha ya kupewa nafasi kubwa kwenye mashindano hayo lakini hazikufua dafu baada ya kutolewa na Real Madrid na PSG.
Arsenal ilikuwa imebeba matumaini makubwa kwa mashabiki wa EPL. Ni klabu ambayo ilijipanga kuchuana kwenye mashindano ya Ulaya msimu huu kutokana na kulikosa taji la EPL ka miaka mitano mfululizo chiniya kocha Mikel Arteta. Hata hivyo tathmini ya jumla inaoneha msimu huu timu z England zimekuwa na mwenendo mzuri na kuonesha ulikuwa msimu wao licha ya kulikosa kombe.
EUROPA LEAGUE
Manchester United wametinga hatua ya fainali baada ya kuitupa nje Atleic Bilbao ya Hispania. Katika mashindano hayo, Man United ina kila sababu ya kulibeba taji hilokama njiaya kufuta machozi kwnai hadi wanatinga hatua hiyo wanahsikilia nafasi ya 15 katika msimamo wa Ligi Kuu England. Jambo la kufurahisha zaidi katka mchezo wa fainali ya Europa League, Man United itakutana na Tottenham Hotspurs. Wakati Man Unitedikiibuka na ushindi wa jumla y mabao 7, wenzao Tottenham Hotspurs waliifuga mabao 2-0 klabu ya Bodo Glimt. Vijana wa kocha Ange Postecoglou wametinga fainali ya Europa League kwa jumla ya mabao 5-1. Hivyo mchezo wa fainali unazikutanisha timu z EPL ambazo zinafahamiana vyema. Pia wana uhakika wa kulibakiza kombe hilo katika ardhi ya England, kwa sbaabu timu zote mbili zilizotinga fainali zinatokea nchini humo.
CONFERENCE LEAGUE
Chelsea wanawakilisha Ligi ya England na wametinga hatua ya fainali. Kwahiyo nayo ni kati yatimu ambazo zinategemea kuibuka na kombe msimu huu endapoitatwa taji hilo. Katika mchezo wa marudiano Chelsea walishinda kwa bao 1-0 dhidi ya Djurgarden ya Sweden. Kwa ushindi huo Chelsea wanatarajiwa kupepetana na Rea Betis kwenye fainali ya Conference League. Katika mchezo wa fainali unatarajiwa kuwa wa kukata na shoka sababu timu zote mbili zimefika hapo kutokana na uwezo, ubora na ufundi wa wachezaji wao. Real Betis kutoka Hispania imeimarika zidi tangu ilipomsajili nyota wa Man United, Athony ambaye ameshirikiana na wengine kama nahodha Isco Alcaron kuing’arisha kwenye mashindano ya Ulaya. Real Betis wamefanikiwa kutinga fainali hiyo kwa jumla ya mabao 4-3 dhidi ya Fiorentina ya Italia. Mchezo wa Fainali wa Conference League utachezwa kwenye uwanja wa Manispaa ya Breslavia jijini Warsaw Mei 28 mwaka huu.
Kimsingi mashindano ya Ulaya msimu huu yalitawaliwa na timu z England na kulikuwa na kila sababu za kuchukua kombe hilo. Katika fainali mbili zijazo, Europa League na Conference League zinahusisha timu tatu za England. Kwamba Europa League kutakuwa na timu mbili za EPL huku kwenye fainali ya Conference kutakuwa na Chelsea peke yake.
Hivyo wana uwezo wa kushangilia mataji mawili ya ulaya msimu huu endapo watafanikiwa kunyakua dhidi ya wapinzani wao.
Comments
Loading…