in , , ,

Wamarekani wazing’arisha Ligi za Ulaya

Stan Kroenke

KILA msimu mpya unapowadia katika Ligi za nchi za Ulaya kumekuwa na ongezeko la wachezaji kutoka Mataifa mbalimbali. Wachezaji hao wananunuliwa kwa ghali, kulipwa mishaara minono pamoja na kuingia mikataba mikubwa yenye tija kwa klabu husika. Kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, Europa League, Conference League, kote huko kumeonekana kunufaishwa na fedha za Kimarekani ambapo wachezaji wanashindanishwa na kupigania fedha za Marekani. 

Katika Ligi za Ufaransa, Hispania, England, Italia, Ujerumani kumekuwa na wachezaji kadhaa wanaowakilisha utaifa wa Marekani, lakini sehemu kubw aya nguvuya fedha ya Wamarekani inatoa mchango mkubwa katika maendeleo ya soka barani Ulaya.

Mwaka 2025 umedhihirisha ongezeko la nguvu za uwekezaji wa Kimarekani katika Ligi za Ulaya. Miongoni mwa uthibitisho huo ni michezo ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya uliozikutanisha Inter Milan na Barcelona. Katika mchezo wa nusu fainali ambao ulilazimika kwenda katika hatua ya dakika za nyongeza baada ya dakika 90 kukosekana mshindi ambapo timu zilitoshana nguvu kwa mabao 3-3 kati ya Inter Milan Italia na Barcelona ya Hispania. Kwenye mchezo huo ambao ambao ulitakiwa kupatikana mshindi umeonesha kuwa mchango wa wawekezaji hao umeongeza chachu ya ushindani kwenye ngazi ya klabu. 

TANZANIASPORTS inaangalia suala muhimu ambalo limesababisha nafasi ya Marekani kwenye mchezo wa Soka. Inafahamika kuwa marekani si taifa kubwa kwenye suala la mchezo wa soka, lakini imepitia mlango mwingine wa uwekezaji katika kutoka mchango wake wa kukuza soka pamoja na kujikusanyia faida za kibiashara kupitia mchezo huo. 

Umiliki wa klabu ya Inter Milan

Mbali ya wachezaji wa soka kuwa na mchango mkubwa katika maendeleo yake nchini Marekani, pia upo mwingne kutoka kwa wamiliki wa vilabu ikiwemo Inter Milan. Msimu huu umeshuhudia mmiliki wa Inter Milan kwa mara ya kwanza akiongoza timu yke kufika hatua ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Inter Milan iliwahi kutwaa taji la Ligi yaMabingwa Ulaya na kutinga mara kadhaa fainali , lakini ikiwa kwenye umiliki tofauti. 

Mmiliki wa Inter Milan ukiwa ni msimu wake wa kwanza ana kila sababu ya kushangilia mafanikio ya klabu hiyo. Mmiliki huyo ni kampuni ya Okatree Capital Management. Kampuni hiyo ya Marekani ilichukua umiliki wa klabu ya Inter Milan Mei 22, 2024 baada ya aliyekuwa Rais wa klabu Steven Zhang kushindwa kulipa mkopo wa Dola Milioni 426 aliochukua kutoka kampuni hiyo. 

Mkopo huo ulitolewa na kampuni hiyo mwaka 2021 ili kuendesha shughuli na masuala mbalimbali ya klabu ya Inter Milan. Tangu walipochukua umiliki katika klabu hiyo mambo yalianza kubadilika hasa katika uendeshaji, morari na utulivu mkubwa ambao uliwapa uhakika wa mapato na kutenga bajeti nzuri kwa ajili ya kupigania mafanikio.

Tangu klabu hiyo ilipochukuliwa na wamiliki toka Marekani, uongozi mpya ulifanya kazi nzuri na ziada kuhakikisha klabu hiyo inarudi kwenye zama zake za mafanikio. Hatua ya kutinga fainali yaLigi ya Mabingwa Ulaya, pamoja na kuwania ubingwa wa Serie A ikichuana na Napoli ni dhahiri tiu hii imerudi kwenye zama za utawala wa soka nchini Italia. Inter Milan na Napoli zinatofautiana pointi chache katika mbio za ubingwa wa Serie A msimu huu.

Ka mtazamo wa wamiliki wapya wa Inter Milan, hatua ya kufika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya inaoneha namna ambavyo wamedhamiria kutawala katika mashindnao ya Ulaya, kuanzia Ligi ya Mabingwa, Europa League, na Conference League.

Familia ya Glazer Manchester United

Klabu ya Manchester United nayo imetinga hatua ya fainali ya Europa League baada ya kuitupa nje klabu ya Atletic  Bilbao ya Hispania. Katika mchezo wa kwanza Man United walishinda mabao 3-0 na hivyo mchezo wa marudiano umehimitishwa kwa jumla ya ushindi wa mabao 7. 

Familia ya Glazer ndiyo inamiliki hisa kubwa katika klabu ya Man United ikishirikiana na mmiliki mwenza Jim Ratcliffe. Timu hiyo imekuwa na mwendo wa kusuasua na wakati mwingine imelazimika kubadili makocha ili kutafuta namna bora ya kurudi kwenye mafanikio kama miaka ya nyuma. Cmchezo wao wa marudiano haukuwa na maumizi mengi ya nguvu kwa sababu ingekuwa vigumu kwa Bilbao kuibuka mshindi kwenye Dimba la Old Traford. 

Ushindi wao kutinga fainali ya Europa League unadhihirisha kuwa usimamizi wa Kimarekni umekuwa ukileta matunda katika mchezo wa soka na kutawala kwenye Ligi hiyo ya pili kwa maarufu baada ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya.

Chelsea katika mikono ya Wamarekani

Kana kwamba haitoshi, klabu ya Chelsea ikiwa chini ya kocha Enzo Maresca imetinga hatua ya fainali ya mashindano ya Conference League. Hii inakuwa timu ya tatu kutoka England ikiwa inatawala kwenye mashindano ya Ulaya msimu huu. Katika hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, Arsenal iliwakilisha vyema Ligi Kuu England ingawaje haikufua dafu mbele ya miamba ya Ufaransa, PSG. Chelsea nayo inakuwa timu nyingine kutamba Ulaya ikiungana na Man United na Tottenham Hotspurs kwenye mashindano ya Conference League. Chelse Ainamilikiwa na raia wa Marekani Todd Boehly. Hii inadhihirisha kuwa mchango wa Marekani kwenye mashindnao ya soka na maendeleo yake barani Ulaya si ya kubezwa.

Katika mazingira hayo wamiliki wengine kama vile FSB wa Liverpool wamenyakua taji la England. Pengine si habari kubwa lakini inadhihirisha mchango wa Marekani kwenye soka la Ulaya.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

39 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

Zamu ya EPL kutamba kwenye UEFA

Tanzania Sports

Ni hasira za Real Madrid sokoni Ulaya