SASA ni bayana Real Madrid intakiwa kuanza maandalizi ya msimu mpya baada ya kupoteza taji lake kwa wapinzani wao Barcelona. Ndoto za kutetea taji hilo zilimalizika mwishoni mwa wiki iliyopita na sasa kocha wao Carlo Ancelotti anatarajiwa kukimbilia nchini Brazil ambako ametangazwa kuwa atakuwa kocha mkuu kuanzia Mei 26 mwaka huu. Real Madrid wapo katika mchakato wa kupata kocha mpya Pamoja na kuunda kiksi chao ili kuelekea kwenye mashindano ya Klabu bingwa dunia. TANZANIASPORTS inakuletea uchambuzi wa kina kuhusiana na mwenendo wa klabu hiyo kuelekea mashindano ya klabu bingwa dunia Pamoja na maendalizi ya msimu mpya kuanzia benchi la ufundi hadi wachezaji mbalimbali ambao wamepangwa kusajiliwa klabuni hapo. Katika mkakati huo Real Madrid inaelekea kuingia kwa hasira sokoni jambo ambalo linatarajiwa kutumika kama sehemu ya kufanya marekebisho makubwa katika klabu hiyo.
Kocha mkuu
Real Madrid wapo kwenye msako wa kocha mkuu baada ya kuthibitishwa kuwa Carlo Ancelotti anandoka klabuni hapo. Majina manne ambayo yamekuwa yakitajwa ni Xabi Alonso ambaye anaondoka katika klabu ya Bayer Leverkusen, Jurgen Klopp ambaye ni mkuu wa klabu za Red Bull, Raul Gonzalenz kocha wa kikosi cha Castilla cha Real Madrid na Zinedine Zidane. Hata hivyo jina la Xabi Alonso ndilo linapewa kipaumbele zaidi kuliko wengine. Inaelezwa kwamba kocha huyu ameamua kuondoka Leverkusen na mwelekeo wake ni klabu ya Real Madrid. Inaelezwa kuwa ni suala la mud awa Real Madrid na Xabi Alonso mwenyewe kutangaza rasmi juu ya kuchukua mikoba ya Ancelotti. Sababu za kutajwa zaidi Alonso ni kutokana na makubaliano ambayo amewahi kuingia na Leverkusen kwamba endapo klabu yoyote kati ya alizowahi kuchezea zikimhitaji basi uongozi wa Leverkusen unatakiwa kumruhusu. Endapo Real Madrid watafanikiwa kumwajiri Xabi Alonso maana yake kibarua hicho kitaanza kwenye mashindano ya Klabu Bingwa dunia kuanzia mwezi Juni mwaka huu.
Trent Alexander-Arnold

Beki huyu wa kulia ameshaagana na klabu yake ya Liverpool na kwamba hatoongeza mkataba wake na hivyo kuondoka klabuni hapo. Licha ya kuzomewa na mashabiki wenye hasira mwishoni mwa wiki lakini amuzi wa Trent ulishachukuliwa na mwelekeo wao ni Kwenda kucheza klabu ya Real Mdarid. Klabu hiyo imekuwa ikihusishwa mara kwa mara na usajili wa nyota huyo lakini hapakuwa na taarifa rasmi juu ya usajili wake. Trent amekuwa akihusishwa na kwendda Real Madrid kwa muda mrefu ambapo sasa kwa kuwa ni mchezaji huru anaweza kutangaza uamuzi wa kujiunga na klabu hiyo. Taarifa za vyombo vya Habari zinasema kuwa uwezekano wa Trent kujiunga na Real Madrid ni mkubwa mno na ataungana na rafiki yake Jude Bellingham. Endapo Trent atatanagzwa kujiunga na Real Madrid ataungana na wachezaji wengine wa Uingereza ambao wamewahi kuichezea klabu hiyo kama vile Michael Owen, Steve Mcmanaman, Jonathan Woodgate na David Beckham. Ujio wa Trent unatarajiwa kutatua changamoto ya beki wa kulia ambako Dani Carvajal amekuwa majeruhi wa muda mrefu huku umri wake ukimtupa mkono, na kuilazimisha Real Madrid kumpanga Lucas Vazquez katika nafasi ya beki wa kulia kutokana na uwezo wake ambao amekuwa akitumia kama winga wa kulia.
Cristian Romero
Katika kukabiliana na changamoto ya safu ya ulinzi, Real Madrid imeripotiwa kufukuzia sahihi ya beki wa kati wa klabu ya Tottenham Hotspurs, Cristian Romero rai awa Argentina. Usajili wa Romero unatajwa kuungwa mkono na Xabi Alonso ambaye anapenda ufanisi wake awapo uwanjani. Nyota huyo amekuwa katika klabu ya Tottenham Hotspurs kwa miaka kadhaa lakini hajafanikiwa kutwaa medali za ubingwa na hivyo kuripotiwa kuchoshwa na maisha ya klabu hiyo. Kwa mujibu wa taarifa za michezo inaonesha kuwa Romero atakuwa ongezeko sahihi katika safu ya ulinzi ambayo imekumbana na wakati mgumu msimu huu. Eder Militao, David Alaba, Antonio Rudiger ni mabeki wa kati ambao wamekuwa majeruhi kwa muda mrefu hivyo kuilazimisha klabu hiyo kumwita kinda Raul Asencio kutoka kikosi cha vijana kucheza kama beki wa kati, huku kiungo mkabaji Aurien Tchouameni akilazimika kucheza kwenye nafasi ya beki wa kati. Real madrid inategemea usajili huu utaondoa aibu waliyokumbana nayo msimu huu ambapo walivuliwa ubingwa katika hatua ya robo fainali na Arsenal kwa kutandikwa jumla ya mabao 5-1.
Namba 9
Haina ubishi kuwa nafasi ya mshambuliaji wa kati ni muhimu kwa klabu hiyo licha ya kumsajili Kylian Mbappe. Kiufundi wachezaji watatu wamechezeshwa katika nafasi ya namba 9, ambapo ni Rodrygo Goes, Vini Junior, na Mbappe. Lakini kwa asili wachezaji wote haw ani mawinga na kiungo washambuliaji. Hata hivyo Real Madrid wana uzoefu wa kutumia wachezaji wa ina hiyo na kuwachezesha kama washambuliaji kamili kama ilivyokuwa kwa Karim Benzema, Gareth Bale, au Cristiano Ronaldo. Katika hekaheka za usajili huenda kocha mpya akahitaji mshambuliaji wa kati ambaye atakuwa na uwezo wa kuongzoa safu hiyo kama inavyotakiwa kuliko hali ya sasa ya mgawanyo na mpishano kati mawinga ambao hucheza kushoto nae neo la namba 9 kwa Pamoja. Mfumo huo umesababisha Rodrygo Goes ahamishiwe upande wa wing awa kulia ili kutoa nafasi kwa Mbappe kucheza namba 9 nuku nyuma yao akiwemo Jude Bellingham kama nambari 10 wao.


Comments
Loading…