in , , , ,

Bila kanuni na taratibu ni hasara Ligi Kuu

KANUNI zinapotungwa kusimamia uendeshaji wa shughuli Fulani huwa na lengo la kulinda na kusimamia miongozi muhimu yenye kuleta tija. Ligi Kuu Tanzania imekuwa na kanuni mbalimbali za Ligi Kuu, Ligi Daraja la Kwanza, Ligi Daraja la Pili, Ligi Daraja la tatu Pamoja na zile zinazihusiha wadau wote wa mchezo wa soka. 

Katika kanuni hizi kila mdau anayetumikia taasisi au klabu ya michezo anakuwa chini ya miongozo iliyokubaliwa na wote ili kuhakikisha kunakuwa na uwanja sawa, utaratibu na mambo ya uwazi yanaeleweka, katika kuzingatia hilo Shirikisho la Soka Nchini Tanzania lina dhamana kubwa kusimamia na kuendeleza mchezo wa soka kwa maslahi ya taifa letu. Kumekuwa na malumbano, ukiukwaji wa kanuni Pamoja na taratibu zingine unaofanywa na wadau au watumishi wa sekta hiyo hali ambayo inasababisha kuishi kwa mazoea ya ‘busara’. Katika kipengele hicho cha busara kimesababisha baadhi ya watu Kutenda mambo kinyume cha taratibu huku wakiomba busara itumike pale wanapohitaji kujiokoa.

Katika muktadha huo kila mdau wa soka anayeagiza kutimiza Masharti ya kikanuni na taratibu anakuwa na hisia kuwa wapo baadhi yao wanabebwa na viongozi wa ngazi za juu wakiwa wamekiuka kanuni na taratibu. Klabu za soka za madaraja yote zinaagiza kuzingatia sheria zilizowekwa ili kuwa na hadhi Pamoja na haki kwa kila upande. Ligi Kuu Tanzania inasifika kwa maendeleo mazuri yaani inapanda kwa kasi kutokana na mafanikio ya klabu zake Pamoja na timu za Taifa. 

Kwa mfano katika timu ya taifa imeshiriki mashindano ya AFCON mara tatu mfululizo sasa ikiwa na maana mabadiliko ya soka yametendeka huku kila upande ukiwa unafurahia hali hiyo. Hali kadhalika katika upande wa klabu tumeshuhudia zikishiriki vyema kwenye mashindano ya CAF na kutetemesha vilabu vikubwa na vingine vya kati na vidogo bila kuvitaja majina. katika msimu wa 2024/25 mwakilishi wa Ligi Kuu pia ametinga fainali ya Kombe la Shirikisho na hivyo kuipa thamani zaidi Ligi Kuu Tanzania kuliko ilivyokuwa zamani. 

Unapopanda ngazi katika mafanikio ya soka ndivyo hadhi ya klabu , ligi au timu ya taifa ndivyo inavyozidi kufuatiliwa. Wataalamu wa mpira duniani wanatuambia kuwa ligi inaposhiriki mara kwa mara kwenye mashindano ya kimataifa inatoa fursa kwa wachezaji wa kigeni na wataalamu wengine kutamani kuja kuchezea vilabu husika ili kutangaza vipaji vyao iwe vya ukocha ua uchezaji, au masuala la utimamu wa afya. 

Hata hivyo wanasisitiza kuwa kama kuna sehemu inapaswa kuangaliwa kwa makini ni upande  wa usimamizi wa ligi yenyewe. Mfano katika usimamizi lazima sheria ichukue mkondo wake bila kuathiriwa na ukubwa au udogo wa timu. Kwahiyo timu yoyote inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania inawajibika kwanza kutimiza wajibu wa kisheria na kikanuni ili kufanikisha malengo yake ya kisoka Pamoja na kuendeleza mchezo wenyewe.

Pia klabu inapoamua kudai haki yake ya msingi pale inapohisi kukiukwa inapaswa kutambua wajibu wake katika kulinda hadhi na kukuza thamani ya Ligi Kuu Tanzania. Katika muktadha huo, kila timu ya Ligi Kuu inatakiwa kuzingatia kanuni kwamba haisababishi hasara kwa klabu zingine wala wadau au wateja wao. 

Mechi inapoashirishwa hasara kubwa inakwenda kwa wadau mfano mashabiki ambao wanekuwa wameshalipia viingilio vya mchezo huo, watu wa masoko pia wanapata hasara, wafanyabiashara wanapata hasara, sekta ya utalii ambayo hutazama michezo ya Ligi Kuu kama sehemu ya utalii hupata hasara, televisheni yenye haki ya kuonesha michezo hiyo nayo hupata hasara, wafanyabiaashara wanaochukua mikopo benki au mikopo binafsi katika taasisi za kifedha kwa lengo la kuuza bidhaa katika siku ya mchezo nao wanakuwa kwenye kundi la watu wanaopata hasara kubwa. 

Katika mazingira hayo ‘busara’ inapotumika kupita kiasi inazaa mazoea. Pia mazoea hayo yakizidi huwa yanasababisha makundi au maelfu ya watu kuanza kuepuka kuingiza fedha zao kuwekeza katika biashara ya mchezo wa soka. 

Hapa tunazungumzia maeneo ambayo biashara hiyo huinua wafanyabiashara wa ngazi tofauti. Fikiria kituo cha telebisheni ambacho kimepoteza mud ana kulipwa fedha za matangazo ya biashara, maana yake mteja wao hajapata huduma ya eneo alililolipia yaani kuonekana kwenye runinga siku ya mchezo na kuwafikia wadau wengi. 

Kisha mteja huyo anaidai televisheni kurudia kutanagza tangazo lake katika mchezo mwingine ambao haukuwa sehemu ya makubaliano hayo. Kutokana na muda kuwa finyu televisheni inalazimika kulipa fida ya mud awa kuchezwa kwa tangazo katika mechi inayofuata ambayo si sehemu ya makubaliano. Kwa vyovyote vile mazingira hayo yanasababisha hasara kwa televisheni kama ilivyo kwa wafanyabiashara wengine ambao wanapoteza mitaji midogo na mikubwa hivyo hasara yake huanza kuepuka kutumia fedha nyingi katika michezo muhimu ya Ligi Kuu kwa sababu hawana uhakika kama fedha zao zitaheshimiwa. 

Taasisi yoyote ambayo inaanza kwa kupuua mahitaji ya wateja wake maana yake inapunguza kiwango cha mapato Pamoja na kuwa kimbiio la watu au taasisi zinazotaka kufanya kazi nazo. Mazingira ya namna hii ni rahisi kuona wateja wakubwa wakianza kuwa na mashaka juu ya sababu za kutotumika kanuni na sheria badala yake mazoea ya ‘busara’ kutumika yanaathiri ukuaji na maendeleo ya mchezo wa kandanda. 

Matumizi ya busara si mabaya hadi pale mazoea yanapochukua nafasi hadi kupuuza sababu za msingi zinazosimamia sekta husika. Kila mmoja ataomba ‘busara’ itumike, na inageuka kuwa Ligi ya ‘Buasara’ na ‘mazoea’ hali ambayo inarudisha nyuma mchango wa wadau Pamoja na mashabiki ambao wanaweza kukosa ari kisha wakaanza kupungua viwanjani. Tuepuka hasara hii.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

Ni hasira za Real Madrid sokoni Ulaya

Tanzania Sports

Yanga kufaidika na Ubingwa wa Simba CAF CC!