MSHAMBULIAJI Harry Kane amejituliza Bayern Munich licha ya wazo lake la awali la kutana kurejea kwenye Ligi Kuu ya Rngland (EPL) na sasa anasubiri kupata mkataba mpya hapo Bayern.
Kane amesema kwamba matamanio yake ya kurudi Uingereza yametulia na sasa anataka aendelee kuwatumikia waajiri wake wa sasa. Alikuwa mshambuliaji nyota wa Tottenham Hotspur kabla ya kutimkia Ujerumani.
Mchezaji huyo amekamilisha nusu ya mkataba wake wa miaka minne aliosaini 2023 msimu wa kiangazi gharamna yake ikiwa ni pauni milioni 86.kwa sasa ana umri wa miaka 32, akiwa amefunga mabao 103 katika mechi 106 alizocheza katika klabu hiyo kubwa ya Ujerumani. Alisaidia klabu yake kutwaa Kombe la Bundesliga msimu wa 2024/5.
Nahodha huyo wa England anasema kwamba kwa sasa hana tena hamu ya kurudi kuchezea England, tofauti na ilivyokuwa kipindi kifupi kilichopita, bali anachofikiria sasa ni kuongeza kandarasi hapo hapo Bayern.
“Kwa upande wa kubakia hapa muda mrefu zaidi, ni wazi kwamba naliona hilo. Nilizungumza wazi hili wiki kadhaa zilizopita. Hatujadili tena mambo hayo na Bayern ningependa kuzungumza kwa uwazi na uaminifu juu ya hatima yangu hapa.
“Ni wazi kwamba inategemea mwaka kesho na huko mbele na tunafanikiwa lipi Pamoja. Kuhusu Ligi Kuu ya England, sijui. Ungeniuliza kitambo nilipojiunga Bayern, ningekuambia kwamba ningerudi (EPL) lakini sasa naweza kusema Hapana, sitarudi,” akasema Kane.
Kane ni mfungaji bora kwa Spurs na Timu ya Taifa ya England – Three Lions na amekuwa mchezaji aliyefikia idadi ya mabao 100 haraka zaidi . hata hivyo amekuwa mkavu wa vikombe hadi alipokuja kutwaaa akiwa Ujerumani.


Comments
Loading…