in

Yanga wako sahihi usajili?

Bernard Morrison

Maswali yamekuwa mengi juu ya usajili wa timu ya Yanga ambayo siku ya jumatatu imewakata wachezaji 14 huku wawili wakiwa katika mazungunzo ya kuongeza mkataba wao.

Walio katika mazungunzo ni Kelvin Yondani na Juma Abdul ambao wameonekana wanaweza kusaidia timu hiyo msimu ujao.

Yanga ambayo tayari imesajili wachezaji wanne huku Azam nao washasajili wanne kelele zaidi wanahoji imekuaje wamekata wachezaji wengi .

Tuanzie hapa kwanza kidogo niliwahi kusemakuwa Yanga wamesajili kwa kufuata benchi la ufundi ambalo liliteuliwa mwaka uliopita .

Pili wachezaji waliosajiliwa hakuna shaka kila mmoja amemuona alicho kifanya .

Yanga wamesajili Bakari Nondo Mwamnyeto huyu beki wa kati anakuja kuwapa ‘Challenge’ Lamine Moro na Kelvin Yondani ambaye wakimaliza maelewano ya mkataba na nina uhakika atabaki.

Nondo tumeona kile alichokifanya ni beki bora sana katika ligi hii na ni mchezaji wa timu ya taifa ya Tanzania.

Tanzania Sports
Yanga

Uwezo wake kila mtanzania anajua na amemuona hivyo kama akicheza Yanga na hakuonesha uwezo ila Yanga na benchi lao la ufundi wamesajili wakati akiwa katika kiwango kizuri.

Waziri Junior huyu alifanya vizuri sana akiwa Mbao FC aliweza kufunga magoli 14  tukijumrisha na yale ya  ‘Play off’.

Junior amesaini dili la miaka miwili akiwa ni mchezaji huru baada ya mkataba wake wa mwaka mmoja kukamilika ndani ya Mbao FC.

Ndani ya Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2019/20 alijenga ushikaji na nyavu akifunga jumla ya mabao 12 akiwa ni namba moja ndani ya kikosi hicho.

Mchezo wa mwisho kuvaa jezi ya Mbao FC ilikuwa  Agosti Mosi, mbele ya Ihefu kwenye mchezo wa ‘playoff’ uliochezwa Uwanja wa Kirumba ambapo alifunga mabao mawili.

Timu yake ya Mbao aliyokuwa anaitumikia awali akiwa ni nahodha imeshushwa jumla itashiriki Ligi Daraja la Kwanza kwa faida ya mabao ya ugenini ambayo Ihefu wameipata.

Mchezo wa kwanza Ihefu ilishinda mabao 2-0 Mbeya na jana ilifungwa mabao 4-2 na kushinda kwa faida ya mabao ya ugenini.

Uwezo wake ulikuwa wa hali ya juu sana Watanzania wameona kile alichokifanya.

Yanga wameona kuwa nafasi ya beki wa kushoto imekuwa ngumu kidogo hivyo wamemsajili Yassin Mustapha nyota wa Polisi Tanzania siku ya  Agosti Mosi, amesaini dili jipya kuitumikia Yanga.

Mchezaji huyo aliyekuwa ananolewa na Malale Hamsini anakuwa ni wa tatu kutambulishwa rasmi ndani ya kikosi cha Yanga.

Walijua kabisa kuwa katika sehemu ya kiungo mkabaji kunatatizo sana hivyo wamechukua kiungo Zawad Mauya kutoka Kagera Sugar.

Wote hao kazi zao zimeonekana na hakuna ubishi kuwa wamecheza vizuri katika msimu huu uliomalizika hivi karibuni.

Swali la kujiuliza ni kweli hapa Bongo walimu huwa wanapewa nafasi kubwa kusajili kama jibu umepata kwa wachezaji hao ambao tumeona wamesajiliwa unafikiri Yanga wamekosea wapi?

Baada ya kujiuliza maswali yote hayo kwa jitihada walizo fanya kwa wachezaji wa ndani unadhani machuguo hayo sio sahihi ukiacha ushabiki ?

Kwa pamoja ukijiuliza maswali hayo utapata jibu halisi kuwa ni wachezaji waliofanya vizuri na walistahili kusajiliwa na timu zenye mwanga mbele yao.

Lakini pia swali la kujiuliza je wachezaji hao wameona umuhimu wa kujiunga na timu ya Yanga watafanya makubwa au watabweteka, kupanga ni kuchagua siku zote.

Bado usajili unaendelea na kuna tetesi kuwa Salum Aboubari na Farid Mussa wote watajiunga na Yanga.

Labda baada ya kuwaondoa wachezaji kama vile David Molinga, Patrick Sibomana naEric Kabamba huenda wakaleta wachezaji walio bora zaidi yao, tetesi zinasema kuwa nyota Tuisila Kisinda na Tunombe wote kutoka AS Vita watatua Jangwani baada ya usajili wa leo.

Report

Written by Amini Nyaungo

For the past 9 years, I have been working as the Sports news Journalist in online and print media this experience help me to be utilized by the different sports events where I have got chances to the media as the football pundit in different media in Tanzania.

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Mbwana Samatta

Mambo 10 yaliyomkabili Samatta EPL

BM

Nani muhuni kati ya Morrison, Yanga na Simba?