in

Nani muhuni kati ya Morrison, Yanga na Simba?

BM

Hapa ndipo mwanzo wangu wa kufikiria kwenye suala hili linaloendelea la Bernard Morrison na usajili wake. Jana imedhitibika kuwa Bernard Morrison amesajili katika klabu ya Simba.

Usajili ambao umezua maswali mengi sana kwa sababu kwa taarifa za awali zinadai kuwa Bernard Morrison alisajili na Yanga kwa mkataba wa miaka 2, mkataba ambao unaisha mwaka 2022.

Kwa maana hiyo Simba wamemsajili Bernard Morrison akiwa ni mchezaji wa Yanga bila kuzungumza na Yanga. Hii ni kwa mujibu wa malalamiko ya viongozi wa Yanga.

Bernard Morrison kwa mdomo wake ameshawahi kukiri kuwa hana mkataba na klabu ya Yanga. Alisajili mkataba wa awali wa miezi 6 ambao ulikuwa unaisha mwezi wa saba mwaka huu.

Kwa maana hiyo Bernard Morrison amesajili Simba akiwa ni mchezaji huru asiyekuwa na mkataba kama ambavyo Yanga wanavyodai kuwa ana mkataba nao.

Simba hakuna walichokisema mpaka sasa hivi kuhusiana na sakata. Swali kubwa ambalo tunatakiwa kujiuliza hapa ni kwanini Simba Sc wamekaa kimya kwa kiasi kikubwa?

Wanajua Bernard Morrison hana mkataba na Yanga ndiyo maana wamejiamini mpaka wameenda kumsajili bila kuzungumza na klabu ya Yanga? Na kama wanajua Bernard Morrison hana mkataba na Yanga nani kawaambia?

Au kama wanajua ana mkataba na Yanga kwanini wameamua kusajili bila kuzungumza na Yanga? Kipi kinawapa kiburi kiasi hiki? Haya ni maswali ambayo tunatakiwa kujiuliza kwenye sakata hili kwa upande wa Simba .

Kwanini Yanga wanadai wanamkataba na Bernard Morrison?  Wanatudanganya? Naamini wanatudanganya? Kabla ya kupata jibu ya hayo maswali tujiulize pia ni kweli Yanga wana mkataba na Yanga na kwanini wamejiamini hivo?

Kama Yanga wamejiamini kuhusu kuwa na mkataba na Bernard Morrison kwanini Bernard Morrison anajiamini kuwa hana mkataba na Yanga? Anafikia hatua mpaka anaongea kwenye vyombo vya habari kwa kujiamini kuwa hana mkataba na Yanga.

Kipi kinachompa kiburi cha yeye kujiamini kiasi hicho? Ni kwa sababu kuwa ni kweli hana mkataba na Yanga? Au kuna kitu kingine cha ziada nyuma yake?

Pande zote tatu, Bernard Morrison,  Yanga na Simba zinatufanya kwa pamoja tubaki na maswali ambayo hayana majibu vyema. Bado tumevifichwa kwa kutotambua ukweli ni upi?

Ukweli ni kuwa Yanga hana mkataba na Bernard Morrison unaoisha 2022? Nani anatufanyia uhuni hapa ? Bernard Morrison , Yanga au Simba ? Hili ni swali gumu ambalo mamlaka ya mpira kama TFF na FIFA zinatakiwa kutupa majibu sahihi.

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

70 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Bernard Morrison

Yanga wako sahihi usajili?

AJIBU

Ajibu aweka alama kwa Mkapa