in

Yanga wakata nyota 14, Morrison ndani?

Dar young africans

Timu ya Yanga imetangaza majina 14 ya wachezaji walioachwa huku ikishuhudia ikimbakisha winga msumbufu Benard Morrison.

Wachezaji ambao wameachwa huru na mikataba yao kuisha ni  pamoja na David Molinga, Mrisho Ngassa, Papy Tshishimbi, Jaffar Mohamed, Tariq Seif, Andrew Vicent, na Issa Banka.

Wachezaji ambao mikataba yao bado iko na atimu inazungunza nayo ni pamoja na Ali Mtoni, Muharami Issa, Ali Ali, Yikpe Gislain, Patrick Sibomana, Eric Kabamba na Rafael Daud.

Wachezaji ambao wanabaki na kuendelea na kuitumikia timu  ya Wananchi ni pamoja na Farouk Shikalo, Ramdhani Kabwili, Metacha Mnata, Haruna Niyonzima, Lamine Moro, Feisal Salum, Juma Mahadhi, Adeyun Saleh, Said Makapu, Balama Mapinduzi, Deus Kaseke, Ditram Nchimbi, Abdullaziz Makame, Benard Morrison  na Paul Godfrey.

Yanga inaendelea na mazungunzo na baadhi ya wachezaji ili wabaki ndani ya timu hiyo ni pamoja na Juma Abdul, Kelvin Yondani ambao mikataba yao imeisha na timu inataka kuendelea nayo.

Timu  hiyo imesha sajili wachezji wanne ikiwemo beki Bakari Nondo, Yassin Mustapha, Wazir Junior na Zawadi Mauya.

Wachezaji wanaotazamiwa kuingia wakati wowote ni pamoja na Tunombe, Tuisilaa Kisinda na Jesse Were.

Report

Written by Amini Nyaungo

For the past 9 years, I have been working as the Sports news Journalist in online and print media this experience help me to be utilized by the different sports events where I have got chances to the media as the football pundit in different media in Tanzania.

What do you think?

72 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Wazir Junior

Wazir Junior ni Adam Salamba mpya?

Mbwana Samatta

Mambo 10 yaliyomkabili Samatta EPL