Uongozi ni daraja muhimu kwenye maendeleo ya taasisi yote duniani. Vilabu vya michezo ambayo vimekuwa vina uongozi imara wenye maono ndivyo vimekuwa hai na endelevu katika mafanikio ya kimichezo na kibiashara. Kwa siku za hivi karibuni vilabu ambavyo vimekuwa bina viongozi vijana ndio vimekuwa na mafanikio kwa Zaidi kuliko vyenye viongozi wa makamo. Kwa kipindi cha nyuma katika nchi ya Tanzania ilikuwa imejengeka dhana ya kwamba viongozi wa vilabu ama vyama vya michezo wanatakiwa wawe tu watu wa makamo na dhana hii ikafanya vijana kuogopa kugombea nafasi katika vilabu na hata kwenye vyama vya michezo.
Mabadiliko yaliyotokea katika nyakati za hivi karibuni kwa baadhi ya vilabu ambavyo vimefanya mabadiliko na kuweka viongozi wapya hususani ambao ni vijana vimejikuta vinapata maendeleo kimichezo na kibiashara. Tukichukulia mfano klabu ya Yanga ilipoamua kubadilisha uongozi na kuweka muundo wa kisasa ambao unakuwa na raisi wa klabu pamoja na watendaji wake imejikuta inapata maendeleo makubwa sana.
Ilipochagua raisi wa klabu mhandisi Said Hersi ambaye ni kijana ambaye alikuwa ajafika hata umri wa miaka 36 wakati anakabidhiwa madaraka imefanikiwa kuwa klabu iliyoongeza mapato yake kutokana na viwango vya udhamini ambavyo imekuwa navyo. Mhandisi Hersi ameajiri watendaji wengi wa klabu hiyo vijana wenye umri mdogo ambao wamekuwa wabunifu na kuifanya klabu hiyo izidi kuvutia kibiashara. Chini ya uongozi wake klabu hiyo imefanikiwa kuwa mshindi wa pili katika kombe la shirikisho na pia kufika katika hatua ya robo fainali katika mashindano ya klabu bingwa ya Afrika katika msimu uliofuatia.
Klabu ya Inter Milan ilikuwa imeanza kupotea kwenye soka la kimataifa na hata la ndani ya nchi ya Italia ambapo mafanikio makubwa ya mwisho yalikuwa waliyoyapata katika msimu wa 2009-2010 ambapo walishinda mataji 3 ikiwemo la klabu bingwa ulaya lakini baada ya hapo wakaanza kuanguka mpaka uwekezaji kutoka nchi ya China ulipochukua klabu hiyo na kasha kuweka uongozi chini ya kijana mwenye umri mdogo ndipo tunaona kwamba klabu hiyo inafanya vizuri katika ligi za ndani mpaka za nje.
Klabu ya Real Madrid mafanikio yake katika ulimwengu wa soka yalianza mnamo mwaka 1943 pale ambapo klau hiyo iliamua kumpatia uraisi wa klabu hiyo kwa Santiago Bernabeu. Awali kabla ya kuwa raisi wa klabu hiyo bwana Bernabeu alikuwa ni mchezaji mahiri wa klabu hiyo, pia aliwahi kufikia daraja la kuwa nahodha wa klabu hiyo wakati anacheza, aliwahi kufikia daraja la kuwa meneja wa klabu hiyo. Alichukua uongozi wa klabu hiyo katika nyakati ngumu. Uongozi wake ulionyesha dalili za wazi kutaka kuacha alama kubwa kwenye soka la timu hiyo na maono yake yalionekana mbali kwani maamuzi ya kwanza aliyoyachukua baada ya kuwa raisi wa klabu hiyo ni kuamua kuanza kujenga uwanja wa klabu hiyo.
Uwanja huo kwa siku za mbeleni ukaja kupewa Jina Lake. Bwana Bernabeu aliamua kuajiri wataalamu wa biashara na utawala ambao walikuwa wanampa ushauri wa namna gani ataweza kuiendesha klabu hiyo kibiashara tofauti na vilabu vingine vilivyokuwa vinajiendesha kwa nyakati hizo. Wataalamu hao wa biashara waliweza kumpatia hata majina gani ya wachezaji ambao kama wakinunuliwa basi klabu ya Real Madrid itatengeneza faida.
Inasemekana wataalamu hao ndio wakampa njia ya kuweza kumshawishi mchezaji hodari wa kutoka taifa la Argentina ambaye tayari alishakuwa ameshafanya mazungumzo ya awali na klabu ya Barcelona kukubaliana kwamba ataichezea klabu hiyo hapo namzungumzia bwana Alfredo Di Stefano. Usajili wa wachezaji mkubwa ulianza baada ya kujenga uwanja mkubwa na wa kisasa kwa wakati huo. Alisajili mastaa kama vile Ferenc Puskás aliyekuwa mshambuliaji hatari kutoka taifa la Hungary na mfaransa Raymond Kopa.
Baada ya kufanya usajili huo akaamua kuanza kufikiria njia ya kujenga jina la klabu yake kimataifa ili kutanua wigo wa biashara na wataalamu wake wakamuambia kwamba aanze kupambania mataji ya kimataifa na hapo ndipo safari ya klabu hiyo kuanza kuchukua mataji makubwa ya kimataifa ikaanza.
Katika miaka ya 1950 mfanyabiashara maarufu aitwaye Louis Edwards ambaye biashara yake kubwa ilikuwa maduka ya nyama (butcher) katika jiji la Manchester aliamua kutafuta namna ya kuweza kununua hisa za klabu ndogo katika mji huo kwa nyakati hizo. Alifanya maamuzi magumu kwenda kutafuta daftari lenye majina ya wanahisa wote wa klabu hiyo na kasha kunakili majina yao kumbuka nyakati hizo hakukuwa na kompyuta wala mashine ya kutoa nakala kivuli (photocopy).
Kwa nyakati hizo Klabu ya Manchester United hisa zake nyingi zilikuwa zinamilikiwa na wajane ambao walipata umiliki baada ya wengi wa wanaume kufariki katika vita wakipigania taifa lao. Akatafuta kiongozi mmoja wa halmashauri ya jiji ambaye alizunguka huku na kule kupita kuwashawishi wamama hao wauze hisa zao na wakakubali. Baada ya kuchukua umiliki kamili wa klabu hiyo mwaka 1964 akaamua kumuacha kocha mzoefu wa miaka 20 bwana Matt Busby aendelee kuifundisha klabu hiyo.
Matt Busby ambaye alikuwa tayari ameshaanza kujenga msingi wa mashabiki wa klabu hiyo aliachwa aendelee na majukumu yake na katika mojawapo ya mambo ambayo mwekezaji bwana Louis Edwards aliyafanya ni kuongeza posho kwa wachezaji. Alifanya maamuzi hayo katika nyakati ambazo ilionekana kama posho kwa wachezaji inatakiwa iwe ni kidogo.
Mwanzoni mwa miaka ya 1970 manchester ilishuka daraja baada ya Busby kustaafu na licha ya kushuka daraja bado ilibaki na mtaji wake wa mashabiki wengi ambao iliwatengeneza hapo awali. Kwenye miaka ya 198 klabu iliachiwa chini ya uongozi wa Martin Edwards ambaye ni mtoto wa Louis Edwards. Martin Edwards ni mbunifu wa mbinu za kutengeneza pesa na alizidi kuifanya klabu ya Manchester kuwa ni klabu ambayo inatengeneza pesa nyingi sana. Mwishoni mwa miaka ya 1980 wakampatia ukocha na umeneja wa timu bwana Alex Ferguson na kumpa nguvu nyingi ambaye aliiletea mafanikio makubwa klabu hiyo.
Comments
Loading…