in , , ,

Rodri amechukua Tuzo ya Carvajal na Ronaldo

KILELE cha utoaji wa Tuzo ya Mchezaji bora Ulaya kimehitimishwa jijini Paris nchini Ufaransa. Waandaaji wa tuzo za Ballon D’or wameshamtangaza mshindi wao Rodri ama Rodriguez ambaye ni kiungo mkabaji wa Manchester City. Ikumbukwe Manchesater City ndiyo mabingwa wa soka nchini England ama tuseme ni wababe wa EPL. 

Tuzo hiyo kwa mara ya kwanza kwa miaka ya karibuni inatolewa kwa mchezaji wa kiungo. Kwa miaka kadhaa aimezoeleka kuwa washambuliaji wamekuwa wakipewa tuzo hiyo huku maeneo mengine kama mabeki wa kati na pembeni kulia na kushoto pamoja na golikipa wakibaki watazamaji. 

Tanzania Sports

Ushindi wa Rodri una maana kubwa sana kwa wachezaji wa aina yake yaani wale wanaocheza eneo la kiungo mkabaji au kiungo mshambuliaji. Hali kadhalika ni muhimu kwa wachezaji wa nafasi nyingine. Mathalani miaka mingi imepita tangu beki wa Kati Fabio Cannavaro alipotwaa tuzo ya mchezaji bora wa dunia. Ilikuwa tuzo halali kwake, ingawaje pia ilikuwa ajabu kuona beki akitwaa tuzo ya uchezaji bora. 

Carvajal alikosaje tuzo?

Wengi wanazungumzia suala la winga wa Real Madrid, Vinicius Junior ambaye alitarajiwa kuchukua tuzo hiyo. Hata hivyo ukweli ni kwamba licha ya umahiri wote wa Vini Jr bado alikuwa na ushindani mkali ndani ya klabu yake ya Real Madrid. Beki wa kulia na nahodha msaidizi wa timu hiyo Dani Carvajal ndiye mshindani halisi wa Rodri. Katika sifa zilizotajw ana waandaaji wa tuzo hizo inaonesha wazi Carvajal ndiye alipaswa kuchuana na Rodri. 

Mapema mwaka huu Zinedine Zidane alijibu swlai katika mahojiano na vyombo vya habari baada ya mechi za hisani alisema wengi wanazungumzia Rodri lakini hawakuwa wakimwangalia Dni Carvajal kama mpinzani aliyepaswa na anastahili tuzo hiyo. Dani Carvajal anamzidi Rodri kwenye kipengele cha tuzo ya Ligi ya Mabingwa. 

Dani ametwaa La Liga, Super Cup, Ligi ya Mabingwa na Kombe la Mataifa ya Ulaya maarufu kama Euro. Katika kikosi cha Hispania, Rodri na Caravajal walikuwa pamoja na hivyo walitwaa kombe hilo huku Dani akiwa miongoni mwa makapteni wa Rodri. Kwa maana hiyo Dani alimzidi Rodri kwenye kipengele cha mafanikio binafsi kwa kuwa ametwaa taji la nyongeza la Ligi ya Mabingwa. Rodri naye ametwaa EPL na Euro na tuzo za uchezaji bora wa mechi kadhaa.

Rodri na tuzo ya Ronaldo

Cristiano Ronaldo anajulikana duniani kote kwa umahiri wake. Ni mchezaji ambaye alionesha makeke makubwa tangu alipokuwa Sporting Lisbon na baadaye akasajiliwa na Manchester United chini ya aliyekuwa kocha mahiri kipindi hicho Sir Alex Ferguson. Ujio wa Cristiano Ronaldo katika Ligi ya EPL uliongeza mvuto zaidi na ushindani wa tuzo ulikuwa mkubwa. Cristiano Ronaldo ndiye mchezaji pekee kutoka EPL aliyetoboa na kunyakua tuzo hiyo miaka 15 iliyopita yaani mwaka 2008. Ronaldo alitwaa tuzo hiyo baada ya kuiwezesha Manchester United kushinda taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya. 

Rekodi ya viungo EPL

Kwa kipindi cha miaka 15 sasa EPL ilikuwa inasotea tuzo hiyo. Lakini pia kwa kipindi miaka hiyo hakuna kiungo mkabaji wa EPL aliyefanikiwa kunyakua tuzo ya mchezaji bora wa Ulaya wa Ballon D’or. Hivyo Rodri anakuwa kiungo wa kwanza wa EPL kuzawadiwa tuzo ya uchezjai wa bora wa Ulaya.

Kwanini Vini Jr amekosa tuzo?

Zinatajwa sababu nyingi za kinidhamu na kadhalika lakini yote hizo ni porojo mtupu. Hakuna chuki dhidi ya Vini Jr kwani katika vipengele kadhaa amezidiwa na wachezaji wawili niliowataja hapo juu. Vini Jr hakufanikiwa kutwaa Kombe la Copa America akiwa na timu ya Taifa ya Brazil. Kama Brazil wangechukua taji la Copa America maana yake ushindani ungekuwa wa watu watatu, Rodri, Dani Carvajal na Vini Jr. 

Lakini hata ingizo la Jude Bellingham utaona kuwa aliachwa mbali na Dani Carvajal kwani hakufanikiwa kunyakua taji la Euro licha ya kufika fainali alikopoteza na Hispania. Kwahiyo waandaaji nao wanashangaza walivyompandisha Jude Bellingham kwani alikuwa na mataji matatu na tuzo binafsi, lakini katika uzito wake naye hakufua dafu mbele ya Dani Cravajal. Labda swali lingekuwa ni kwanini waandaaji wa Ballon D’or hawajampa tuzo Dani Carvajal? Hadi kufikia hapo utaona Real Madrid wanayo haki yote kushangaa lakini penye ushindani mmoja huibuka bingwa.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

Eric Ten Hag aliidharau Man United

Tanzania Sports

Tunazijua Vyema Sheria, Au Ni Mijadala Tu