in , , ,

Mkude alifaa kulipwa milioni 17 na siyo Tshishimbi

Moja ya vitu ambavyo vimetokea wiki hii na kuonesha tofauti ya wachezaji wetu wazawa hapa nyumbani na wachezaji wageni wanaokuja kucheza kwenye ligi yetu ni suala la Papy “Kabamba” Tshishimbi.

Mchezaji ambaye yuko karibu sana na mioyo ya mashabiki wa mpira hapa Tanzania hasa hasa mashabiki wa Yanga. Ni mchezaji ambaye alizaliwa na dimba la kati kwake yeye ni rahisi sana kulitawala.

Anajua hilo, anajua kuwa yeye ni mchezaji mzuri kwenye ligi yetu. Anajua kuwa anauhakika mkubwa wa kupata namba kwenye timu nyingi hapa nchini na kikubwa zaidi anajua kuwa anapendwa na mashabiki wengi sana hapa nchini.

Hizi ndizo silaha alizozingua na ndizo silaha ambazo aliamua kuzitumia wiki hii kwenye anga ya mpira wetu wa Tanzania. Mkataba wake na Yanga ulikuwa unaelekea mwishoni kumalizika.

Papy “Kabamba” Tshishimbi alijitengenezea hitaji kwanza moyoni mwake, hitaji ambalo alilisambaza kwa wengine na hao watu kuona kuwa hitaji hili ni sahihi kabisa kutokana na kiwango chake pamoja na mapenzi anayoyapata kwa mashabiki.

Papy “Kabamba” Tshishimbi aliamini kuwa anaweza kulipwa milioni 17 za kitanzania kwa mwezi kama mshahara wake. Pesa ambazo ni chache sana kwenye biashara ya mpira wa miguu lakini ni pesa ambayo haijazoeleka kutolewa kwenye ligi yetu.

Papy “Kabamba” Tshishimbi alitengeneza hitaji hili moyoni mwake, moyo wake ulihitaji kiwango hiki cha mshahara . Taratibu hitaji lake akalisambaza kwa wahitaji wa huduma yake yani vilabu vya mpira wa miguu.

Ndipo hapo ukawa mwanzo wa tetesi za yeye kwenda Simba kucheza kwa sababu pesa hii ilionekana ni kubwa kwa Yanga na ilikuwa ngumu kwa Yanga kufanikisha kwa sababu ya kuachana na GSM ambaye kwa asilimia kubwa ndiye ambaye ameshughulikia masuala ya mishahara ndani ya Yanga.

Papy “Kabamba” Tshishimbi alitengeneza hitaji kubwa ambalo lilionekana linamfaa sana na yeye aliwaaminisha wengi kuwa hitaji hili linamfaa sana na alistahili.kupata pesa zile.

Kuna kitu kimoja ambacho Papy “Kabamba” Tshishimbi katuonesha na kinatakiwa kiingwe na wachezaji wetu wazawa wa hapa nyumbani Tanzania, kitu chenyewe ni kujitengenezea thamani kubwa .

Papy “kabamba” Tshishimbi kajitengenezea thamani kubwa ambayo wengi tumeona anastahili kuwa nayo. Swali la kujiuliza Papy “Kabamba” Tshishimbi ni mchezaji bora kuzidi wachezaji wetu wa ndani?

Yani hakuna mchezaji wa ndani ambaye ana kiwango kikubwa ndani ya uwanja? Kiwango ambacho kinaweza kumtia kiburi na kujipandisha thamani kwenye soko la usajili kwa kuamini kuwa anastahili thamani hiyo kubwa?

Hapa ndipo tofauti ya wachezaji wetu wazawa na wachezaji wageni wanaokuja kwenye ligi yetu inapoanzia . Wachezaji wetu wazawa hawajawahi kufikiria wanastahili kulipwa milioni 17, ila wachezaji wa nje wanajiona na thamani hiyo hata kama wana viwango vya kawaida ukilinganisha na kiwango cha wachezaji wetu wa ndani.

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Mikel Arteta

Arteta apona Corona

Tanzania Sports

CORONA: Barcelona mazungumzoni kukata wachezaji wake mishahara