in , , ,

Arteta apona Corona

Mikel Arteta


*Fainali UCL shaka kubwa

Hatimaye moshi mweupe umetoka, matumaini yamerejea baada ya wiki mbili za masikitiko klabuni Arsernal kutokana na kocha wao na mchezaji wao wa zamani, Mikel Arteta kuambukizwa virusi vya Corona.

Lakini sasa, kocha huyo Mhispania aliyeambukizwa wakati wa mechi ya Ligi ya Europa dhidi ya Olyimpiakos, anasema amepona na anajihisi vyema, akiwa na sifa njema na buheri wa afya.

Palikuwapo ukimnya mkubwa juu ya maendeleo ya kocha huyo kiafya, hasa ikizingatiwa kwamba maelfu ya watu – hasa wa Ulaya, wamepoteza maisha kutokana na ugonjwa huo uliositisha mchezo pendwa wa soka katika nchi karibu zote.

Arteta anabainisha kwamba ilimchukua siku tatu au nne baada ya ‘kupigwa’ na virusi hivyo vilivyoanzia Wuhan, China, kuanza kujihisi nguvu. Arteta (37) alitokea kuwa kocha wa kwanza katika Ligi Kuu ya England (EPL) kupata virusi hivyo, nayo ilikuwa Machi 12.

Aliripoti kujihisi vibaya baada ya kuwa imethibitishwa kwamba mmiliki wa Olympiakos, Evangelos Marinakis wa Ugiriki alikuwa na virusi hivyo, na walikutana naye timu yake walipopambana na Arsenal jijini London na Arsenal kutolewa. Mmiliki huyo alisema alipata virusi hivyo Machi 10.

Arteta alisema hayo wakati akihojiwa na kituo cha televisheni cha Hispania akasema; “Ilinichukua siku tatu au nne kuana kujihisi vyema, nikiwa na nguvu zaidi na kuacha dalili zote za Corona mbali. Nipo vizuri sana sasa, najua nimeshapona kabisa,” akasema Arteta.

Kambi ya mazoezi ya Washika Bunduki wa London ilifungwa baada ya habari hizo, na kila mchezaji akatakiwa ajitenge nyumbani kwake, lakini kila mmoja aendelee na mazoezi na walipelekewa vifaa husika huko kwa ajili ya kujifua kuja kumalizia msimu wa ligi tarehe itakapopangwa.

Wachezaji wa Arsenal walikuwa warudi kwa mazoezi kuanzia Jumanne hii, bada ya kukamilika kwa siku 14 za kujitenga na umma kutokana na uchunguzi na kuthibitika kuathirika kwa Arteta, lakini baada ya majadiliano ya daktari wa Arsenal, wenzake wa klabu za EPL na uongozi, wameamua kuahirisha, kwani hata hivyo serikali imezuia mikusanyiko na ligi haitarudia kabla ya Aprili 30.

“Kutokana na matokeo ya hali ya sasa, tumeona wazi kwamba haitakuwa sawa, na hatutakuwa tunawajibika vyema kuwataka wachezaji warudi wakati huu. Kwa hiyo timu ya kwanza ya wanaume, akademia nay a wanawake watabaki nyumbani ili kuendelea kuokoa maisha,” taarifa ya klabu ilisema.

Arteta anaeleza alivyoanza kujihisi akisema alipata simu kutoka kwa bodi ya wakurugenzi baada ya mazoezi, akiwa kwenye gari yake, akiambiwa kwamba rais huyo wa Olympiakos alikuwa na virusi vya Corona na kwamba kila mmoja aliyekutana naye alikuwa hatarini.

“Basi mie nikaenda na kuwaeleza kwamba sikuwa najihisi vyema na kwamba kuna watu wengine pia ambao walikutana na watu wa jamaa huyu. Tulikuwa nag emu dhidi ya Manchester City siku iliyokuwa inafuata na ni wazi hatungeweza kuwatia watu wengi zaidi hatarini bila kusema kitu.

“Ni wazi, wale waliokuwa wamekutana nami walilazimika kwenda katika karantini na hatimaye mchezo ule ukaahirishwa.,” akasema Arteta ambaye inaelezwa kwamba katika wiki ya pili ya karantini yake alikuwa ameanza kufanya kazi mbalimbali, akichora ramani ya mipango ya kikosi chake baada ya kuwasili.

Katika maendeleo mengine, Shirikisho la Soka la Ulaya (Uefa) linapata mtihani wa jinsi ya kumalizia Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL) na huenda likaamua kwamba ichezwe mechi ya mkondo mmoja tu na vivyo hivyo kwa Ligi ya Europa baada ya kuahirisha mechi za mtoano za michuano hiyo mikubwa kwa bara la Ulaya.

Huku soka ya Ulaya ikiwa imeahirishwa kwa sababu ya balaa la virusi vya Corona vinavyosababisha ugonjwa wa Covid-19, hakuna uwezekano wa michuano hiyo kwenda kama kawaida na kufikia mwisho kwa mujibu wa ratiba ya kawaida mwishoni mwa Mei mwaka hu una kufunga pazia la msimu.

Katika UCL, mechi nne za 16 bora zimeshamalizika, wakati mechi za mkondo wa pili kwa nyingine ni bado. Katika Ligi ya Europa, mechi sita za mkondo wa kwanza zimechezwa lakini bado mbili.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

Corona: Ni wakati wa viongozi kuchukua hatua madhubuti

Tanzania Sports

Mkude alifaa kulipwa milioni 17 na siyo Tshishimbi