in

Mastaa wa kigeni kubaki Simba na Yanga?

simba yanga

LIGI Kuu Tanzania Bara imepata bingwa wake. Msimu wa 2019/2020 unaelekea ukingoni. Macho na masikio yamekuwa yakitupwa kwenye vikosi vya Yanga na Simba kila msimu.

Wapo wachezaji wa kigeni waliosajiliwa katika klabu hizo mbili za jijini Dar es salaam walikuwa gumzo mwanzoni mwa msimu wa 2019/2020 ambapo walitabiriwa kuwa ubingwa wake utapatikana kwa vita kali.

MEDDIE KAGERE

Mshambuliaji huyu amekuwa mwiba kwenye kikosi cha Simba. Inaonekana wazi Simba wakimkosa mshambuliaji huyu wanakuwa kwenye wakati mgumu mno. Baada ya kuibuka mfungaji bora msimu uliopita ni dhahiri mwamba huyu amebaki kuwa nyota wa kikosi cha Simba.

Anakubalika kwa viongozi, wachezaji na mashabiki. Anamudu kucheza mifumo 4-4-2 na -5-4-1. Changamoto yake ni pale anapocheza na John Bocco. Mara nyingi anaonekana mudu kucheza kama mshambuliaji wa mwisho, lakini akipangiwa wa pili husababisha mgongano.

Meddie, ana kasi, nguvu, pumzi, mashuti, shabaha, na akili ya ufungaji iko imara. Udhaifu wake habadiliki kulingana na mbinu, hivyo kumlazimisha kocha ajipange kuchezesha timu namna inavyomsaidia Meddie. Bocco kwa upande wake, ana mashuti, nguvu, kasi na zaidi uzuri wake anamudu kuendana na mbinu za kocha. Ndiyo maana wakati kwingine timu ya taifa anacheza winga wa kulia mwenye jukumu la kumsaidia nambari 9 Taifa Stars.

Lakini akiwa Simba anahitaji sana kasi ya Meddie. kwa ujumla Meddie Kagere ni alama halisi ya ubora wa wachezaji wa kigeni. Ameng’arisha nyota ya wachezaji wa kigeni.

DAVID MOLINGA

Ni mchezaji ambaye amekuwa gumzo mara nyingi katika mechi za Ligi Kuu tangu alipotua Yanga akitokea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Awali hakupewa umuhimu na washabiki kama mmoja wa nyota wanaoweza kutamba msimu.

Wengi walidhani Molinga ndiye atakuwa nyota zaidi kuliko wengine lakini hali haikuwa hivyo. Bado anasua sua. Mfumo ambao anamudu zaidi ni ule wa 4-4-2 na 4-3-3, lakini hawezi kucheza kama mshambuliaji pekee kwenye mfumo wa 5-4-1 au 4-3-2-1. Muundo wa mashambuliaji wa pamoja kitiu ndiyo chchu ya kuona uwezo wake.

Hadi Ligi inakwenda ukingoni, bado mashabiki wanasubiri kuona kiwango cha nyota huyu na sababu za alyekuwa kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera kupendekeza asajiliwe. Molinga alikuwa mmoja wa wafungaji Bora watano wa Ligi kuu ya DR Congo msimu uliopita. Je David Molinga atabaki kikosini? Hapana. Anastahili kuuzwa.

LAMINE MORO

Dala huyu alisajili na Yanga msimu huu wa 2019/2020 kutoka Ghana. Lamine Moro amekonga nyoyo za washabiki wa Yanga kutokana na kujituma na kutoa maelekezo kwa safu ya ulinzi na kiungo. Udhaifu wa nyota huyu ni matumizi makubwa ya nguvu katika soka la kisasa.

Hilo limesababisha awe analimwa kadi nykundu mara kwa mara. Udhaifu mwingine haonekani kumudu -3-4-3 kwa sababu mabeki wa pembeni wanaposhiriki kucheza kama mawinga wanaacha nafasi ambayo inamwelemea. Jambo jingine hana kasi ya mchezo, kupandisha mashambulizi, jicho la kiufundi bado dhaifu. Anamudu kucheza mifumo 4-4-2, 4-3-3 au 5-4-1 kwa sababu mabeki wote wanabaki nyuma.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 25 ataweza kutawala safu ya ulinzi ya Yanga iwapo atapunguzwa matumzi ya nguvu na kuhamishia kwenye ufundi na maarifa. Anastahili kubaki Yanga.

GERSON FRAGA

Huyu ni miongoni mwa wachezaji wapya waliotua kwa mabingwa wa soka Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba. Gerson Fraga Vieira ni beki  wa kati. Ni nyota ambaye alitarajiwa kuonyesha makali yake ikizingatiwa anatokea taifa ambalo linasifika kwa kucheza kandanda duniani, Brazil. Fraga hajaonesha chache za ajabu katika Ligi Kuu Tanzania Bara. Amekuwa beki mbadala katika safu ya ulinzi, lakini bado mchango wake unahitajika kutathminiwa tena. Anafaa kuruhusiwa kuondoka.

TAIRONE SANTOS DA SILVA

Naye kama alivyo kwa Fraga, ni raia wa Brazil. Simba wanao wachezaji watatu kutoka Brazil akiwemo Da Silva. Nyota huyo ana umri wa 30 alisaini mkataba wa miaka miwili akitokea ya Atlético Cearense FC. Usajili wao ulilenga kuifanya Simba kuwa timu ya kimataifa na yenye kuvutia wachezaji nyota kutoka kila pembe ya dunia. Da Silva hajafakia hata nusu matarajio ya mashabiki wa  Simba. Vilevile soka la Tanzania halijawahi kuhitaji kiungo kabaji kutoka nje. Da Silva naye anastahili kuondoka Simba.

WILKER DA SILVA

Hayupo kwenye orodha ya wafungaji bora Ligi Kuu Tanzania Bara. Hayupo kwenye orodha ya wachezaji machachari wa Simba. Badala yake Simba imeendelea kuwategemea John Bocco na Meddie Kagere ambao wamekuwa chachu ya mafanikio katika kikosi cha mabingwa hao kwa miaka ya karibuni. Wilker alitarajiwa kuziba pengo la Emmanuel Okwi lakini hajafanikiwa. Anastahili kuuzwa.

SHIBOUB SHARAF ELDIN

Ni kiungo aliyesajiliwa Simba msimu huu 2019/2020. Nyota huyo alishateka nyoyo za mashabiki wa Simba mwanzoni kwa kufunga mabao na ufundi wa kutengeneza pasi za mabao. Kiungo huyo kutoka Sudan naye alitarajiwa kufanya makubwa Ligi Kuu Bara msimu huu, lakini hajafanikiwa kabisa. Amekuwa mchezaji ambaye mchango wake si mkubwa, huku umri wake unamtupa mkono akiwa amevuka miaka 30. Anastahili kuondolewa Simba.

PATRICK SIBOMANA

Nyota mwingine mpya aliyeingia kwa kasi katika klabu ya Yanga akitokea nchini Rwanda. Sibomaana anaweza kucheza winga wa kushoto na mshambuliaji wa pili (namba 10). Alitafuta namba ya kudumu katika kikosi cha Yanga, lakini hakuwa na mwendelezo. Aliingia Ligi Kuu Bara kwa mara ya kwanza, wengi walitarajia angeonyesha kiwango kikubwa lakini hakufikia matarajio ya wana Yanga. Hata hivyo anastahili.

FAROUK SHIKHALO

Nyanda kutoka nchini Kenya aliyesajiliwa kuziba pengo la Claus Kindoki wa DR Congo. Shikhalo ni golikipa mzuri ambaye alishawishiwa kuja Yanga na kocha wa zamani wa Yanga. Ndani ya klabu ya Yanga alitarajiwa kuchuana na Metacha Mnata. Lakini bado ameshindwa kujihakikishia namba moja kwani Metacha amemzidi maarifa. Shikhalo anastahili kubaki kikosini Yanga.

Report

Written by Mark Mpangala

*Markus Mpangala ni Mhariri, Mwandishi wa Makala Maalumu, Mwanahabari,Mwanablogu,Mwanafasihi na Mwanasafu, ambapo kwa kipindi cha miaka 12 amefanya kazi katika vyombo vya habari mbalimbali vikubwa na vidogo nchini Tanzania katika Michezo, Siasa, Elimu na utalii. Pia ni mchambuzi mchangiaji wa masuala ya siasa na utawala bora katika idhaa ya Kiswahili ya Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC SWAHILI). Ni mhariri na mhamasishaji wa usomaji wa vitabu*

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
David Molinga

David Molinga tishio jipya kwa Simba

Simba 4 Yanga 1

Simba Atoa Kichapo kwa Yanga