in

David Molinga tishio jipya kwa Simba

David Molinga

Kuelekea mechi ya watani wa jadi, Simba na Yanga itakayochezwa jumapili ya tarehe 12/7/2020 kuna baadhi ya wachezaji ambao wanaonekana kuimarika kuelekea mechi hii, mmoja ya wachezaji hao ni David Molinga.

David Molinga ambaye siku za nyuma alikuwa ametofautiana na kocha msaidizi wa Yanga Charles Boniface Mkwasa na akaonekana pia kutofautiana na mashabiki wa Yanga, lakini tangu tofauti zao wazimalize, David Molinga anaonekana msaada kwa Yanga. Kiufundi upi ubora wa David Molinga kuelekea mechi ya watani wa jadi?

TAKWIMU ZAKE

David Molinga amekuwa na takwimu nzuri kwa hivi karibuni. Katika mechi nne za mwisho David Molinga amefunga magoli 3 na kutoa pasi moja ya mwisho iliyozaa goli, kwa hiyo David Molinga katika mechi 4 zilizopita amehusika kwenye magoli 4 .

David Molinga pamoja na kuwa na wastani wa kuhusika na goli moja kwenye kila mechi, pia David Molinga amekuwa akifunga magoli muhimu sana kwenye hayo magoli. Mfano alitokea benchi na kufanikiwa kufunga magoli 2 kwenye mechi dhidi ya Namungo ambayo walikuwa nyuma ya magoli 2, alisawazisha na kuipa timu yake alama 1.

Tanzania Sports
David Molinga, tishio kwa ngome ya Simba

Kwenye mechi dhidi ya Kagera Sugar ambayo ilikuwa mechi ya robo fainali ya Azam Federation Cup alifunga goli moja ambalo liliiwezesha timu yake kuingia nusu fainali ya kombe hili la Azam Federation Cup, pia kwenye mechi ya Kagera Sugar iliyochezwa juzi Bukoba, David Molinga alifanikiwa kutoa pasi ya mwisho ya goli, kwa hiyo amekuwa akihusika katika nyakati ngumu.

2: MAGOLI YA VICHWA

Yanga imekuwa ikitumia sana mipira mirefu kwa nyakati mbalimbali. Msimu uliopita Yanga walikuwa na Makambo ambaye alikuwa na uwezo mkubwa wa kufunga magoli ya vichwa, lakini tangu aondoke amekosekana mtu ambaye ana uwezo wa kufunga aina hii ya magoli, lakini hivi karibuni David Molinga amekuwa akifunga sana magoli ya vichwa, mfano katika magoli yake matatu yaliyopita, magoli mawili kafunga kwa mpira wa kichwa. Hii inaweza kuleta wasiwasi katika kikosi cha Simba kwa sababu Simba wamekuwa dhaifu sana kwenye mipira ya kichwa katika eneo lao la ulinzi.

3: KUTENGENEZA UWAZI

Moja ya faida kubwa ya kuwa na David Molinga ni uwezo wa kutengeneza uwazi (spaces) ndani ya uwanja. Amekuwa ni aina ya wachezaji ambao wana uwezo wa kutosimama eneo moja la mbele, ni rahisi kwake kushuka chini kufuata mipira, kwenda kulia au kushoto mwa uwanja kitu ambacho kinasababisha mabeki wa timu pinzani kumfuata kila anapozunguka, wanapokuwa wanamfuata hutengeneza uwazi mkubwa katika eneo la nyuma ya uwanja, uwazi huu unaweza kutumiwa na wachezaji wa mbele wa Yanga.

4: KUZUIA

Moja ya faida kubwa ambayo kwa sasa mpira wa kisasa ni kuona kila mchezaji anashiriki kwa kiasi kikubwa katika kuzuia. David Molinga kwenye hili amefanikiwa kwa kiasi kikubwa. Amekuwa aina ya washambuliaji ambao wanaweza kukabia juu, kupambana na mabeki wa kati katika kugombania mpira. Pia ni ngumu kwa mabeki kuwa huru kiasi kikubwa wakati ambao yeye yupo mbele, mabeki hukosa uhuru wa wao kusogea mbele kwa ajili ya kuanzisha mashambulizi kwa sababu yeye David Molinga amekuwa kama beki wa kwanza kwenye timu.

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Magoli ya Meddie

Yuko wapi Meddie Kagere?

simba yanga

Mastaa wa kigeni kubaki Simba na Yanga?