in

Manara, Muro na Nugaz nani zaidi?

Tanzania ndio sehemu pekee Afisa Habari anafahamika zaidi kuliko mchezaji mpira ndani ya timu, hii nadra sana kwa nchi zilizoendelea katika michezo.

Hebu tujiulize nani anamfahamu Afisa Habari wa Manchester United, Arsenal, Liverpool au Chelsea, usitumie ‘Google’ jibu moyoni tu wakati unasoma makala hii, kisha nenda ‘Google’ kaangalie kama hujatumia dakika tano au sita kumjua.

Hii ni mifumo ambayo inatumika zaidi huku Afrika, hasa Tanzania  kutokana na kuwa nyuma kabisa katika maendeleo ya utawala wa soka, yaani Ofisa Habari anafahamika zaidi kuliko hata Kocha wa timu?

Natambua mtakuwa na minong’ono mingi, kuna wengine utawasikia huo ndio mfumo tuliojichagulia, kama ni huo mbona mambo mengi mnaiga kwa walioendelea.

Wakati mwingine inawezekana ikawa utoto kuendekeza haya mambo ya kuwapa ‘Airtime’ sana hawa watu wanaojiita maafisa habari.

Huo kwa upande mmoja wa shilingi lakini upande wa pili kama soka linaenda kwa kupitia hao na kila kitu kiko sawa basi waacheni waendelee kubwabwaja mbungi ipigwe.

Labda nikueleze kitu Afisa Habari wa Arsenal na timu nyingine zilizoendelea wanachokifanya ni kubuni mambo mbalimbali ya kihabari na kimkakati kwa ajili ya watu wao, kutoa habari ambazo huwa hazina mikwaruzo kama zetu.

Tanzania Sports
Picha maarufu ya Haji Manara

Mimi nishawahi kumuona mwandishi ambaye bado hajajulikana akampigia Afisa Habari wa timu moja kubwa Tanzania akamjibu kuwa haongei na waandishi wadogo, huu ni utoto wa hao watu.

Tuje katika mada tunayotaka kuongea sana, Yanga na Simba moja ya vilabu vinavyotoa Maafisa Habari waliokuwa na sauti kubwa kwa soka la Tanzania.

Nawasifu wanafanya vizuri sana lakini hawafanyi yale yanayohusu weledi wao, kwani kazi kubwa kwao kuandaa mambo mbalimbali yanayohusu habari ili timu inufaike kwa kipato kupitia tasnia yao.

Lakini tuwe wakweli yupi kati ya hao nani anayefanya hivyo na kuingizia kipato klabu?

Jibu hakuna ila kwa mfumo ulivyo wa Kiafrika wanafanya vizuri sana.

Ukweli ni kwamba Maafisa habari wengi wamepita katika vilabu vya Simba na Yanga ila wapo walioweka  alama na wataenziwa sana.

Japo kuna Maafisa Habari wa muda mrefu ambao wanafanya vizuri kuanzia muda huo hadi sasa.

Hawa wawili sitaki kuwaingiza huko nakumbuka Thobias Kifaru wa Mtibwa Sugar tangu nipo shule ya msingi hadi leo bado naheshima yake, huyu tangu 1999 namsikia hadi leo amedumu Mtibwa na bado anafanya vizuri.

Masau Bwire yeye ameanza na timu ya JKT Ruvu 2003 kabla haijaitwa Ruvu Shooting hadi leo na miongoni mwa wanaoitikisa tasnia hiyo.

Haya turudi kwa mapacha (Simba na Yanga) wawili hawa waliozaliwa 1935 na 1936 hawa ndio wanaoitikisa sana tasnia hii. Ukweli ni kwamba hata mie nafurahi, achana na juu hapo nilipoanza kuwachana ila wanachangamsha sana.

Haji Manara, huyu ni Mkuu wa Kitengo cha habari pale Simba huenda asiwe mjuzi sana katika kuandika na mipango ya kuingiza kipato kwa timu kutumia mkono wake japo naye ni Mwandishi wa habari kabisa ila anatumia vizuri mdomo wake na huenda kupitia watamazaji uwanjani ni majibu ya kazi yake.

Simba wamepita wengi kina Ezekile Kimwaga, Clifford Ndimbo na Marehemu yule dada yetu Mungu amrehemu ila Manara bado yuko juu yao.

Ameanzisha misemo mingi ya kuwafanya shabiki wa Simba apate hamu ya kuingia uwanjani.

Simba ilipoingia katika michuano ya kimataifa msimu wa mwka 2018/19 aliwapanga mashabiki zake na akasema ‘This is Simba’  ikawa kama wimbo wa taifa pale huku akiweka vijembe mbalimbali kwa Yanga ambao ndio watani wao hivyo sio ugomvi.

Akasema Yanga ‘Kwasukwasu’ yaani huwa neno likikaa mdomoni analisema na linaitika kweli, sio ugomvi baina ya Yanga na Simba ila ndio utamaduni.

Akiwataja Yanga kama ‘Vyura’ kutokana na kuwa karibu na bonde la mto Jangwani maji ya kijaa kunakuwa na kasheshe.

Manara ilibaki kidogo aondolewe katika nafasi yake msimu uliopita ila baada ya kuingia Senzo alijua umuhimu wake na akasema hadharani abaki na kweli anafanya vizuri.

Yanga na Simba msemaji asiyekuwa na maneno sio muhimu sana mambo mengine ya weledi tutajua mbele kwa mbele ila kwanza tutoe radha ya maneno.

Ndio maana baada ya muda walipokuja wasemaji wa Yanga wasiokuwa na maneno ‘game’ ilipooza sana.

Dismas Ten aliingia Yanga hakuwa na maneno ila yeye alijikita katika weledi zaidi na alifanikiwa kwa kiasi kikubwa ukinambia nani bora kati ya wote naweza kumtaja Dismas Ten, ila nikirudi katika mambo yetu ya kitamaduni Haji Manara atabaki kuwa juu mawinguni.

Jerry Muro huyu alikuwepo kipindi cha Yanga ya Manji alitengeneza kitu kizuri tunaita vita ya maneno dhidi ya Haji Manara na alinogesha sana.

Wakati yeye Afisa Habari Yanga ilikuwa inafanya vizuri sana akaibuka na maneno mengi kwa Simba akawaita ‘Wamatopeni’ kwa kuwa hawakwenda kushiriki michuano ya kimataifa, aliwaita ‘Wamchangani’ yote hayo juu ya kutoshiriki michuano ya kimataifa.

Kwangu mimi Muro kwa vita ya meneno alimuweza Manara kwa kiasi kikubwa na uwezo wao umelingana kwa maneno ya kejeli yote hiyo ikiwa katika kuwafurahisha mashabiki wake.

Mara Yanga wanamleta Hassan Bumbuli kuwa mkuu wa Idara ya habari, ila anaonekana hana maneno sana Yanga wamefikiria wakaona kuna mtu anaweza kuongea vizuri kutoka katika kipindi cha Kambi popote Antonio Nugaz ambaye naye anauwezo ule ule.

Akaingia naye Yanga kweli msimu wa kwanza ameweza kurudisah heshima kwa wanayanga kuingia uwanjani na kauli yake ‘Wape salam’ ambayo imebamba na huenda ndio iliyokuwa bora msimu huu.

Nugaz hana tofuati sana na Manara kwa maneno pia huenda asiwe mzuri katika kuandika ila kwa kutumia mdomo wake anaweza kuleta kitu kizuri ndani ya timu hiyo.

Imefikia hatua watu wakashindanisha msemo wa Nugaz ‘Wape Salam’ na ule wa Manara  ‘This is Simba’ kwa ubora na jinsi ulivyoteka nyoyo za shabiki zao.

Hawa Maafisa Habari wa timu hizi ndio maarufu zaidi kuliko wachezaji na ndio mfumo tuliojiwekea hivyo tuendelee nao hadi hapo utakapoingia ule weledi wenyewe wa uendeshaji SOKA kama siyo michezo yote kimaadili.

Hii ndio orodha yangu bora ya Maafisa Habari wa mchezo wa mpira wa miguu Tanzania,  Haji Manara, Jerry Muro, Antonio Nugaz, Masau Bwire,  Tobias Kifaru na Dismas Ten.

Wewe unaweza kuandika orodha yako hapo nani moja, mbili hadi namba ya mwisho.

Report

Written by Amini Nyaungo

For the past 9 years, I have been working as the Sports news Journalist in online and print media this experience help me to be utilized by the different sports events where I have got chances to the media as the football pundit in different media in Tanzania.

What do you think?

74 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
fikiria thamani ya jezi nambari 10

Thamani ya jezi namba 10 imebaki ileile?

Lengo likiwa lilelile kuwavutia watu kufika uwanjani

Ali Kiba, Samatta, uso kwa uso Taifa