in , , ,

MAENEO YATAKAYOAMUA MECHI YA FAINALI YA FA KATI YA CHELSEA NA ARSENAL.

Arsenal inaenda katika uwanja wa Wembley ikiwa imeshinda mechi sita
(6) mfululizo ambazo amechezea katika uwanja huo.

Hii inawapa nguvu kubwa ya kujiamini kwa Arsenal katika uwanja wa Wembley.

Wenger anapigana kuwa kocha mwenye mafanikio makubwa katika michuano
hii kama kocha aliyechukua mara nyingi kombe hili.

Rekodi hii inaweza ikawa haimuumizi kichwa kwa sasa ila hatma yake
ndani ya kikosi cha Arsenal ndicho kitu ambacho ƙkitakuwa kinamuumiza
kichwa kwa sasa ingawa kwenye paji lake la uso haoneshi ishara yoyote
juu ya kuumizwa na hili suala.

Kivyovyote vile Arsene Wenger atakuwa anajua kabisa matokeo ya mechi
hii yatakuwa yanaamua hatima yake katika klabu ya Arsenal.

Majeraha kwa baadhi ya mabeki wa kati itakuwa pengo kubwa kwao?

Hakuna jibu la moja kwa moja kwenye hili ila ukweli ni kwamba
ƙkukosekana kwa Laurent Koscienly , Gabriel Paulista na Mustafi ambaye
anaonekana na hati hati ya kucheza itakuwa ni hali ngumu kwenye kikosi
cha Arsenal. Kwa sababu mabeki hawa wamekuwa mhimili mkubwa katika
safu ya ulinzi ya Arsenal.

Hii itampa nafasi kubwa Per Metersecker kuanza katika mechi yake ya
kwanza msimu huu. Ni kweli Per Metersecker ni mzoefu pia ni kiongozi
mzuri lakini tatizo anakosa match sharpeness kutokana na kutokucheza
na timu kwa muda mrefu.

Ila katika eneo jingine kukosekana kwa hawa wachezaji kutawapa nafasi
wachezaji watakaocheza katika eneo hilo kucheza kwa kujitolea ili
kuhakikisha pengo hilo halionekani. Katika kipindi kama hiki wachezaji
hushikamana kucheza kwa nguvu kwa sababu hujua wachezaji wao muhimu
hawapo .

Kitu ambacho kinatia faraja Holding ameshakuwa na uwezo mzuri wa
kucheza mechi kubwa uwepo wake unaweza usitie hofu kutokana na uwezo
wake aliouonesha kwenye mechi zilizopita.

Arsenal Wenger anatakiwa aendelee kutumia mabeki 3 katika mechi hii ?

Mafanikio aliyoyapata katika mechi tisa alizotumia huu mfumo na kuweza
kushinda mechi nane unampa nafasi kubwa sana kwake leo kuutumia huu
mfumo na kumpa matokeo chanya.

Tatizo linakuja leo Per Metersecker anaingia kama ingizo jipya kwenye
huu mfumo na hana kasi ambayo haimpi umadhubutu wa kuwadhibiti
washambuliaji wa Chelsea kama Costa na Hazard ambao wanakasi.

Ubora wa kiungo cha Chelsea kinaweza kuamua mechi ya leo ?

Chelsea wameimarika vizuri eneo hili na wanaelewana vizuri sana.

Kila kitu kizuri kinaanzia kwenye eneo hili, kwa sababu Kante na Matic
au Fabregas ndiyo wachezeshaji wa timu ya chelsea maeneo yote.

Hawa ndiyo wanaofanya kina Hazard, Moses na Marcus Alonso kucheza vizuri.

Kipi wakifanye Arsenal ili wafanikiwe kutotoa uhuru kwa Chelsea ?

Kitu pekee kitakachowasaidia Arsenal ni wao kuhakikisha wanacheza kwa
kasi na kushtukiza , kucheza kwao kwa kasi kutawafanya viungo wa
Chelsea kuwa katika eneo lao zaidi na wanapokuwa katika eneo lao
hakuwapi nafasi ya kuchezesha timu kwa kiwango kikubwa.

Hazard ndiye mchezaji wa kuchungwa zaidi kwenye mechi hii ?

Hakuna shaka Hazard ndiye mchezaji ambaye anatengeneza radha tamu ya
Chelsea, yeye ndiye analeta uwiano mzuri kati ya eneo la kiungo na
ushambuliaji kwa kucheza huru katika eneo hilo.

Hii itawapa nafasi kina Pedro , Willian na Costa kuwa na nafasi nzuri
ya kufanya chochote katika lango la Arsenal.

Kipi wakifanye Arsenal kupita ukuta mgumu wa Chelsea ?

Kati ya vitu ambavyo vitaipa nafasi kubwa Arsenal ni wao kumchezesha
mshambuliaji wa kati ambaye ana kasi , hii itawafanya mabeki wa
Chelsea kukabia kwa ndani na kuwanyima uwezo wa wao kusukuma timu,
kukabia kwao kwa ndani kutawapa nafasi Arsenal kuwa na mipira mingi
katika eneo la hatari ya Chelsea, kuwepo kwa mipira mingi katika eneo
la hatari la Chelsea kutawapa nafasi Ozil na Sanchez kuwa na uwezo wa
kuitumia vizuri, hivo kuanza kwa Welbeck kutakuwa na faida kuliko
Giroud.

Martin Kiyumbi

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

JOSE MOURINHO NA MANCHESTER UNITED NI VITABU VYA KISHUJAA

Tanzania Sports

UMEKUWA MSIMU WA MAFANIKIO MAKUBWA KWA SIMBA