in , , ,

MAENEO AMBAYO YALIWAPA NGUVU YA USHINDI SPURS DHIDI YA ARSENAL JANA

Kwa mara ya kwanza Spurs anamaliza juu ya Arsenal baada ya miaka 22
mfululizo kumaliza nyuma ya Arsenal kwenye ligi.

Kumaliza kwao mbele ya Arsenal kunamaanisha kuwa mwaka huu hakutakuwa
na St. Totteringham’s Day. Siku ambayo wapenzi wa Arsenal husherehekea
baada ya kumaliza mbele ya Spurs.

Ni ukweli usiopingika kuwa Spurs kwa misimu ya hivi karibuni imekuwa
ikionekana bora sana na Mauricio Pochettino amefanikiwa kwa kiasi
kikubwa kuijenga Spurs kama timu ya ushindani wa kugombea kombe na
siyo kugombea kuwepo katika nafasi nne za juu ili ipate nafasi ya
kushiriki mashindano ya klabu bingwa ya ulaya yani UEFA.

Mechi ya jana Spurs alikuwa na nafasi kubwa sana ya kupata goli katika
kipindi cha kwanza kwa sababu walitawala nafasi kwa kiasi kikubwa na
kupata nafasi nyingi za wazi kama aliyoipata Delle Alli kwa kichwa
chake kwenda nje na ile aliyoipata Christian Ericksen.

Eric Dier na Victor Wanyama walijenga ukuta imara pale katika ya
uwanja, hawa wawili waliifanya Spurs ianze kujizuia katikati mwa
uwanja kitu ambacho hakikuwapa nafasi Arsenal ya kupata mashambulizi
mengi.

Kuanzia kujilinda katikati na kuwazidi nguvu za mwili viungo wa
Arsenal kulikuwa kunawapa nafasi kubwa Christian Ericksen na Delle Ali
kuja katikati mwa uwanja na kuchukua mipira kisha kuanzisha
mashambulizi.

Christian Ericksen na Delle Alli hawakuwa na kazi kubwa ya kuwasaidia
Victor Wanayama na Eric Dier kuzuia kwa sababu walikuwa imara sana
kwenye kuzuia.

Hivo Christian Ericksen na Delle Alli walisaidia kwa kiasi kikubwa
kuleta uwiano mzuri kati ya eneo la kiungo na eneo la ushambuliaji kwa
maana ya kwamba walikuwa na nafasi ya wao kuwa wanakuja kuchukua
mipira katikati ya uwanja na kuanzisha mashambulizi ambayo kwa kiasi
kikubwa Harry Kane hakuwaangusha maana jana alizidi kuwa mwiba kwa
mabeki wa Arsenal.

Na mechi ya jana ilimfanya afikishe goli 6 katika michezo mitano
amɓayo amekutana na Arsenal na hii inaonesha Harry Kane amekuwa na
ɓahati kuɓwa sana ya kuifunga Arsenal.

Mfumo wa kutumia mabeki watatu kwa upande wa Arsenal umekuwa una
matokeo ya kupanda na kushuka na kwa mechi ya jana kati ya vitu
ambavyo vilisababisha Arsenal wapoteze mchezo ni kule kutumia mabeki
watatu.

Kwanini nasema hivo ??

Jana Oxlaide Chamberlain alicheza kama kiungo mshambuliaji wa pembeni
na siyo RightWingBack kitu hiki kilimpa nafasi Son aweze kuwa huru
katika kushambulia kwa sababu hakuwa na mzigo mkubwa wa kukabwa.

Ulikuwa mzigo mzito kwa Gabriel kumkaba Son bila msaada wa Oxlaide
Chamberlain ambaye alikuwa anatumia muda mwingi akiwa mbele na
kujisahau kurudi nyuma hata wakati anarudi alikuwa anarudi akiwa
amechelewa.

Kwa upande wa Gibbs msaada mkubwa kwake ulikuwa katika kujilinda, yeye
na Monreal walitengeneza ulinzi mzuri lakini upande ule haukuwa na
uwiano mzuri wa kushambulia na kujilinda. Gibbs hakuwa ameweka uwiano
katika ilo kitu kilichosababisha beki wa kulia wa Spurs kuwa na
majukumu machache kwenye ulinzi na kuwa na majukumu mengi kwenye
kushambulia. Kitu kilichosababisha kupiga presha kubwa sana katika
eneo la ulinzi wa Arsenal.

Kumwanzisha Giroud katika mfumo ambao unahitaji washambuliaji wepesi
wenye kasi , wasiopoteza mpira na kutotumia nafasi wanazopata ilikuwa
karata ambayo haikufanikiwa kwa Arsenal

Maana walikuwa wanaanza kujikaba mbele kwa kupoteza nafasi nyingi kitu
kilichowafanya mabeki wa Spurs kutopata bughuza muda mwingi.

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

SABABU KWANINI SPURS WATASHINDA DHIDI YA ARSENAL

Serengeti boys

SERENGETI BOYS ITUPE FUNZO KWENYE MAENDELEO YA SOKA LA VIJANA